CHADEMA haikamatiki udiwani kata ya Lwenzera-Geita:CCM wamemtelekeza mgombea wao

dr lwaitama "" sasa hivi tupo katika zama za kuiondoa ccm madarakani"" sasa wote tufanye mambo yetu kwa kuzingatia zama hizi na kujipanga kukiandaa chama cha mapinduzi kuwa chama makini cha upinzania from 2015
 
Taarifa imetulia sana mkuu,tunashukuru Mungu na awape ulinzi makamanda wote walio mstari wa mbele kuwakomboa wanyonge hao...aluta continue!!

Unaonaje basi kama ungemgonge like, atiwe moyo?
 
Kazi ya upinzani katika siasa ni kukosoa mapungufu/udhaifu wa chama tawala. Inakuwa ni kazi rahisi sana kujenga hoja kama serikali inayoongozwa na chama tawala ina mapungufu mengi, ya wazi yanayoonekana na kila mtu hata mwenye upeo mdogo. Udhaifu wa CCM katika miaka ya karibuni umekuwa mkubwa sana kiasi hata mwananchi wa kijijini kabisa mwenye upeo mdogo sana wa kuchambua hali halisi anauona. Kwa hali hii, mtu yeyote anahitaji tu kupangilia hotuba yake katika udhaifu huu na ni jinsi gani anajipanga kuuondoa ataonekana ni kinara.

seheme zote uko sahihi isipo kuwa hapo kwenye red umenichefua.....
 
taarifa imetulia kwa mpangilio na kiswahili bora kabisa.CHADEMA wanamtegemea MUNGU na ndiye aliye wapa uwezo, nguvu na ujasiri wa kunena wayanenayo. nguvu ya MUNGU ni mjuaye mimi itatuongoza hadi kuikomboa Nchi.
 
Huwa nashindwa kuelewa, kuleta uzi wa namna hii jamvini si kuwapa faida wapinzani wenu? Huwa kuna wakati hata internal strategies za chama zinamwagwa humu.

swali, je ujumbe hauwezi pia kuwa kinyume chake, yaani unaweza pia kuwa unawakatisha kabisa tamaa hao ccm kwamba hali yao na mbaya?
Sasa mipaka ya kujinadi na kutoa siri ni wapi kama hii inaweza kuwa siri ya kutunzwa? Naelewa umuhimu wa kutunza siri za Chama lakini kwa uzi huu Maelezo zaidi yanahitajika.
 
Kazi ya upinzani katika siasa ni kukosoa mapungufu/udhaifu wa chama tawala. Inakuwa ni kazi rahisi sana kujenga hoja kama serikali inayoongozwa na chama tawala ina mapungufu mengi, ya wazi yanayoonekana na kila mtu hata mwenye upeo mdogo. Udhaifu wa CCM katika miaka ya karibuni umekuwa mkubwa sana kiasi hata mwananchi wa kijijini kabisa mwenye upeo mdogo sana wa kuchambua hali halisi anauona. Kwa hali hii, mtu yeyote anahitaji tu kupangilia hotuba yake katika udhaifu huu na ni jinsi gani anajipanga kuuondoa ataonekana ni kinara.

Ahsante mkuu, kinacho nipa taabu nipa hao wachache wasio weza kuona mapungufu yao na bado ni ving'ang'anizi wa madaraka.
 
Kila la heri wapiganaji wetu tupo pamoko kila hatua na muendelee kutujuza yanayojiri cjajua pande za mpwapwa msalato na kule iringa mambo yakoje wadau
 
Hakuna kilicho haribika hapo mkuu,ccm wenyewe wanahudhuria kwenye mikutano na mikutano ya kampeni ni ya wazi..so huwezi ukadhibiti taarifa ya namna hii..kama huatipata Jf basi utaipata gazetini au utasimuliwa na walioko kule...hakuna internal strategies nilizo mwaga humu,niko makini na mwenyewe niko front line,so iknow what am exactly doing...au wewe ni gamba maana siri niliyoiweka ndani ya uzi ni ya magamba kumtelekeza mgombea wao,basi samahani mkuu ila ndo ukweli wenyewe

Nadhani kwa akili ya kawaida tu habari njema ambayo ungeileta hapa jamvini ni trend ya kampeni za chama chako sasa kuleta habari ya kutelekezwa kwa mgombea wa CCM maana yake unamwamsha adui ajipange upya.Yaani unaripoti kwa Nape ili apange kikosi vema cha kampeni. Ulikuwa ni ushauri kwako tu.Tatizo kila anayekuja na mawazo tofauti unamuona gamba,you need to change.
 
Hivi na sisi wahuku Mtwara tutafunguka lini ?,tujiongeze jamani ,mbona wenzetu wanaweza sisi tunashindwa nini kupata Kiongozi wa ukweli?
 
Makamanda hata huko Mtibwa Mvomero nako shishiem imeumia,mgombea wao ameongea jana jukwaani kwa dakika ziziso zidi 2. Hawa hawana wanachodai kwa sasa kila kona wametaitiwa. Mtibwa wamezindua jana kijiji cha kidudwe kwa mbwembwe za magali ila cha moto wamekiona
 
Back
Top Bottom