CHADEMA haikamatiki udiwani kata ya Lwenzera-Geita:CCM wamemtelekeza mgombea wao

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Timu ya kampeni ya chadema iliyo piga kambi katani Lwenzera chini ya mwenyekiti wa jimbo kamanda Mabula Kachoji kwa takribani wiki 2 sasa,imesababisha ccm kupotezana na kukoswa mwelekeo na kumwacha njiapandamgombea wao bwana Misango asijue la kufanya.

Wakati chadema wakiendelea na mikutano yao ya kampeni katani humo wakimnadi mgombea wao anayekubalika sana kamanda Ibuga,huku wakiendelea pia kutoa elemu ya uraia,kupokea wanachama wapya na wale wanaotokea ccm,ccm wameshindwa hata kuzindua kampeni zao na mstakabali mzima juu ya uchaguzi haujulikani.

Uwezo mkubwa wa kujenga hoja unaoonyeshwa na timu nzima ya kampeni katika mikutano yao umekuwa gumzo na kivutio kwa wakazi wa kata hii, na wengi wamekwenda mbali zaidi kwa kuhoji ni wapi chadema imekuwa ikipeleka watu wake kujifunza mambo ya siasa,hali hii imechagizwa pia na uwezo mkubwa wa kujibu maswali ya papo kwa papo ambao umekuwa ukionyeshwa na mgombea wa chadema.

'.........IBUGA(mgombea wa cdm) tunamfahamu sababu kazaliwa nakukulia hapa na hakuwa muongeaji, kaingia tu cdm sasa anaongea mbele ya halaiki kubwa ya watu, kwa hisia, tena kwa kujiamini....huko nyuma kabla ya mambo haya ya uchaguzi alikuja kijana anaitwa ALPHONSE MAWAZO akafanya mikutano mingi tu.....na hivi majuzi tulishuhudia sura ngeni kabisa kwenye uzinduzi wa kampeni zao lakini uwezo wa watu hawa katika kujenga hoja,kushawishi na kujieleza uko juu........HIVI HAWA CHADEMA CHUO CHAO CHA MAFUNZO YA SIASA KIKO WAPI NA WALIMU WANAWATOA WAPI.....?' Ni mazungumzo kati ya wazee wawili(mmoja akiwa ni mwalimu wa s/msingi) niliyo yanasa nilipokuwa jirani nao wakati tunafuatilia mkutano wa kampeni kule Membe(eneo maarufu sana kwa uvuvi wa samaki aina ya kamongo.

Nawasilisha.
 
Taarifa imetulia sana mkuu,tunashukuru Mungu na awape ulinzi makamanda wote walio mstari wa mbele kuwakomboa wanyonge hao...aluta continue!!
 
Ni kawaida ya ccm kutelekeza wagombea wao wanapoona mambo magumu.

Uliza Arumeru Mashariki jinsi walivyomtosa kijana Sumari baada ya matokeo yaliyomgaragaza kutangazwa... Kabla ya kutangawa matokeo wote walimwacha solemba, akabaki na mkewe.
 
Bado usajili mpya toka ukoo wa Wasira,usajili huo umetisha hata kabla kucheza mechi hiyo kwenye mazoezi tu.Hapo jitahidini zaidi na zaidi ili 2015 iwe kama kumsukuma mlevi, angalau kwa uchache tupate wabunge 230.
 
natamani nchi nzima ingehama ccm! ni bora kutokuwa na chama, kuliko kuwa ccm!
 
Taarifa imetulia sana mkuu,tunashukuru Mungu na awape ulinzi makamanda wote walio mstari wa mbele kuwakomboa wanyonge hao...aluta continue!!

Asante kamanda ,ubarikiwe nawe pia
 
Kazi ya upinzani katika siasa ni kukosoa mapungufu/udhaifu wa chama tawala. Inakuwa ni kazi rahisi sana kujenga hoja kama serikali inayoongozwa na chama tawala ina mapungufu mengi, ya wazi yanayoonekana na kila mtu hata mwenye upeo mdogo. Udhaifu wa CCM katika miaka ya karibuni umekuwa mkubwa sana kiasi hata mwananchi wa kijijini kabisa mwenye upeo mdogo sana wa kuchambua hali halisi anauona. Kwa hali hii, mtu yeyote anahitaji tu kupangilia hotuba yake katika udhaifu huu na ni jinsi gani anajipanga kuuondoa ataonekana ni kinara.
 
Timu ya kampeni ya chadema iliyo piga kambi katani Lwenzera chini ya mwenyekiti wa jimbo kamanda Mabula Kachoji kwa takribani wiki 2 sasa,imesababisha ccm kupotezana na kukoswa mwelekeo na kumwacha njiapandamgombea wao bwana Misango asijue la kufanya.

Wakati chadema wakiendelea na mikutano yao ya kampeni katani humo wakimnadi mgombea wao anayekubalika sana kamanda Ibuga,huku wakiendelea pia kutoa elemu ya uraia,kupokea wanachama wapya na wale wanaotokea ccm,ccm wameshindwa hata kuzindua kampeni zao na mstakabali mzima juu ya uchaguzi haujulikani.

Uwezo mkubwa wa kujenga hoja unaoonyeshwa na timu nzima ya kampeni katika mikutano yao umekuwa gumzo na kivutio kwa wakazi wa kata hii, na wengi wamekwenda mbali zaidi kwa kuhoji ni wapi chadema imekuwa ikipeleka watu wake kujifunza mambo ya siasa,hali hii imechagizwa pia na uwezo mkubwa wa kujibu maswali ya papo kwa papo ambao umekuwa ukionyeshwa na mgombea wa chadema.

'.........IBUGA(mgombea wa cdm) tunamfahamu sababu kazaliwa nakukulia hapa na hakuwa muongeaji, kaingia tu cdm sasa anaongea mbele ya halaiki kubwa ya watu, kwa hisia, tena kwa kujiamini....huko nyuma kabla ya mambo haya ya uchaguzi alikuja kijana anaitwa ALPHONSE MAWAZO akafanya mikutano mingi tu.....na hivi majuzi tulishuhudia sura ngeni kabisa kwenye uzinduzi wa kampeni zao lakini uwezo wa watu hawa katika kujenga hoja,kushawishi na kujieleza uko juu........HIVI HAWA CHADEMA CHUO CHAO CHA MAFUNZO YA SIASA KIKO WAPI NA WALIMU WANAWATOA WAPI.....?' Ni mazungumzo kati ya wazee wawili(mmoja akiwa ni mwalimu wa s/msingi) niliyo yanasa nilipokuwa jirani nao wakati tunafuatilia mkutano wa kampeni kule Membe(eneo maarufu sana kwa uvuvi wa samaki aina ya kamongo.

Nawasilisha.

Huwa nashindwa kuelewa, kuleta uzi wa namna hii jamvini si kuwapa faida wapinzani wenu? Huwa kuna wakati hata internal strategies za chama zinamwagwa humu.
 
Hakuna kilicho haribika hapo mkuu,ccm wenyewe wanahudhuria kwenye mikutano na mikutano ya kampeni ni ya wazi..so huwezi ukadhibiti taarifa ya namna hii..kama huatipata Jf basi utaipata gazetini au utasimuliwa na walioko kule...hakuna internal strategies nilizo mwaga humu,niko makini na mwenyewe niko front line,so iknow what am exactly doing...au wewe ni gamba maana siri niliyoiweka ndani ya uzi ni ya magamba kumtelekeza mgombea wao,basi samahani mkuu ila ndo ukweli wenyewe
 
nyie malizeni kazi makamanda wangu - nipo nipo dar nasubiria form za urais 2015 CDM hadi kitaeleweka.
 
Back
Top Bottom