CHADEMA haijatoa tamko lolote kuhusu mgao wa Maji na Umeme. Je, wamesahau wajibu wao kama chama kikuu cha upinzani?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Sijaona popote pale CHADEMA ambao ni chama kikuu cha upinzani kikizungumzia uwepo wa mgao wa maji na umeme.

Wakati wa Dr Slaa maswala yote yanayoleta sintofahamu kwa wananchi yalihojiwa kwa haraka sana bila kujali kuna makundi ya Friends of Lowassa au Lindi kuchele ndani ya CCM.

Je, Chadema ya J J Mnyika imekengeuka na kuwasahau wananchi?

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwa kuwa nyie sii wasikivu wakutosha, haifai kutetewa Kwa kila, jambo mnafaa mjifunze pia, ila pia kumbuka wanalo jambo la kitaifa Kwa sasa, ila bado wanawajali watanzania wote wasikivu na wasio wasikivu kama wewe.
 
Hahahaaaa........mimi ni msikivu bwashee!
 
Mbona ameshaongea Zitto.
Mnyika haaminiki na mihimili,huwa anawaandikia vipeperushi.
 
Sifa za chama kikuu cha upinzani imebadilika au bado zipo palepale?

Inamaana chama tawala hakiwezi kuwajali wananchi wake bila kelele za upinzani?
 
Sifa za chama kikuu cha upinzani imebadilika au bado zipo palepale?

Inamaana chama tawala hakiwezi kuwajali wananchi wake bila kelele za upinzani?
Ili wasizijali kelele zao wamejikita kuwafunga wapaza sauti ili kuviua vyama vyenye kuwanyima usingizi.
 
Mambo yako Zanzibar mjomba kama ilivyokuwa Chatto ati? Fuata nyuki ule asali. Kadhia za maji na umeme? Mambo ya bara hayo.

Bongo Nyoso!
 
Mleta mada uwena uruma ndugu kwani ujui kuwa tupo katika kesi sasa umeme unakujaje wakati kule sero haya umeme haupo tulia kidogo
 
Yapo mambo mazuri wanafanya lakini...
===
Wameanza lini kuelezea sera ama kushauri wananchi namna bora ya kujiletea maendeleo moja kwa moja? Uliwahi kusikia wanashauri watanzania wajiandae kukabiliana na ukame wa mwezi 10-12/ 2021 wakati taarifa wanazo toka mwezi wa nane? Ukiwauliza hivyo, wanajibu eti si wajibu wao?
 
waswahili hamjawaji kuwa na jema hata kidogo. wakitoa tamko, mtasema chedema wanatoa matamko kuendana na matukio.

nashauri wasitoe ili sote tuisome namba kimyakimya.
 
Sasa wapinzani wakiongea kweli mnawachukua na kuwaweka ndani na kuwasingizia kesi za ugaidi, endeleeni na rohombaya na chuki zenu huku mkilazimisha madaraka kwa nguvu
 
Sijaona popote pale CHADEMA ambao ni chama kikuu cha upinzani kikizungumzia uwepo wa mgao wa maji na umeme.

Wakati wa Dr Slaa maswala yote yanayoleta sintofahamu kwa wananchi yalihojiwa kwa haraka sana bila kujali kuna makundi ya Friends of Lowassa au Lindi kuchele ndani ya CCM.

Je, Chadema ya J J Mnyika imekengeuka na kuwasahau wananchi?

Maendeleo hayana vyama!
Eti wakati wa Slaa! Kwenye Covid Slaa alikuepo? Acha ujinga
 
Back
Top Bottom