CHADEMA haifai kuwa ni Chama Cha Siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA haifai kuwa ni Chama Cha Siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Nov 27, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kusema kweli Chadema kimepoteza muelekeo wa kuwa Chama cha siasa na badala yake kinaelekea kuipeleka Tanzania pahala pabaya ,sehemu ambayo itakuwa tabu sana kurudi huku tulikotoka kwenye amani na utulivu.

  Kwa muda huu Chadema inapuliza vuvuzela la machafuko Tanzania nzima ,kwa kuwa tu imepigwa bao la kisigino na kuachwa kwenye mataa.Nionavyo na mawazo yangu mgando ni bora chama hiki kifungwe au kiondoke kwenye medani za siasa na kuingia misituni kiendeleze mapambano ya kuing'oa CCM madarakani na sio kutumia siasa kama jukwaa la kuiondoa CCM kwani haitofanikiwa milele.

  Mimi nilipowaona wanang'ang'ania kuvaa magwanda ya kijeshi nilijua tu kuwa hawa sio wanasiasa aidha watakuwa na lengo lingine kabisa ambalo leo hii limeanza kuota kama uyoga.Maguo yale ya kijeshi hutumika kwenye vita kwa kuvaliwa na viongozi waandamizi ambao huwa ni wazamiaji wa shughuli za kuendeleza mapambano na Chadema walianza zamani kuwavaa viongozi wa serikali za Tz zilizopita kwa kuwakosoa na kuwaweka katika hali ngumu na hata kupelekea mabadiliko ya serikali katika ngazi za uwaziri.

  Chadema kama mmechoka na siasa bora mvunje chama na kurudi huko mnakotokea au ingieni msituni tujue kuwa mmekusudia.
   
 2. D

  Derimto JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Una akili chafu na maarifa yamekupiga chenga kama kweli wewe ni mzalendo halisi utajipanga kwa hoja na sio kwenda msituni unaenda msituni kufanya nini wakati ushindi ulikuwa wa wazi watu wanatakiwa kudai ushindi mchana kweupe na sio kiwoga na kukimbilia msituni
  MTAJI WA CHADEMA NI WATU WALIOKO MITAANI NA SIYO MSITUNI
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mujahidina bwana!
   
 4. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Janjaweed mko wengi sana.
   
 5. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Katika red, ya kwanza inadhihirisha wazi kuwa wewe ni mtaji mkubwa wa CCM, na hivyo kufanya kazi ya kuikomboa Tanzania kuwa si rahisi...! Lakini pia kwa kuwa umeonesha mwenyewe kuwa unjitambua kuwa hivyo, na kwa jinsi ninavyojua ilivyo kazi ngumu kumwelewesha asiyetaka kuelewa, basi sina muda wa kubishana nawe maana ni sawa na kupoteza muda....!
  Katika red, ya pili inatuonesha jinsi ulivyo shetani au sumu wa jamii ya Tanzania kwa ujumla....! Kwa hili nakushauri ujaribu kufuatilia kampeni za uchaguzi uliopita, na umsikilize JK kule Songea na Dr. Slaa akiwa kwenye mdahalo pale MOVEN PICK, Dar es Salaam...! Naamini huenda ukajua unakoelekea, japo najua ni kazi ngumu sana kwa mujibu wa aya hiyo hapo juu....! Vinginevyo, nakuachia Mungu kwa hayo yote....!
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CCM chama cha familia ya mwenyekiti. CCM huwa inaogopa nini mpaka isiruhusu hata wanavyuo kupiga kura kama iko imara!!!! ha ha ha ha.
   
 7. N

  NAHUJA JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 14,990
  Likes Received: 15,549
  Trophy Points: 280
  CHADEMA NI WEHU. kwanza huyo Slaa mwenyewe ana hasira kama nini. hivi yule angechukua urais si kuna siku watu tungechapwa viboko nchi nzima. kwanza hajui mahusiano na watu.
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hukukosea kama ulivyoainisha hilo Neno lenye Rangi Red! CHADEMA :whoo:
   
 9. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  CUF bana...baada ya kupewa tende na halua huko zanzibar sasa mmeanza kuleta sumu maeneo mengine!!
   
 10. d

  dotto JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HAkuna mwehu kama mwizi wa Richmond, EPA, MEREMETA!! N.K. KAma ungekuwa unakerwa na wizi huu ungekuwa japo na hisia za hasira. labda kama ni mshirika wa wizi huo>>
   
 11. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Dr.Slaa anahasira na wewe ambae bado unalalia Kitanda cha TEMBE na Choo Cha Passportsize! Amka CHADEMA :whoo:
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,640
  Likes Received: 21,852
  Trophy Points: 280
  Baada yakusoma hiyo red nimeona hakuna haja yakujadili lolote usemalo. Kwaheri
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Umeanza kauli yako katika hali ya kuonyesha unajali sana amani ya nchi, lakini umemalizia na uchochezi mkubwa wa kuitaka CHADEMA iingie mstuni, ikienda huko msituni itakuwa inampiga risasi nani? Kikwete au wananchi wa kawaida wasio na hatia? Mbona uwezo wetu wa kufikiria wakati mwingine unakuwa na utata kiasi hiki? Mtaji wa CHADEMA ni wananchi maskini ambao ndiyo wapiga kura, sasa kikiingia msituni kuwapiga risasi kitaungwa mkono na nani?

  kwa upande mwingine, ninakufahamu wewe Mwiba, kwa muda mrefu kama mshabiki wa CUF hasa ile ya upande wa Zanzibar. Kinachonisahangaza, ni kwanini umeona kwamba CHADEMA ndo wanatakiwa kwenda msituni na si CUF ambayo tangu 1995 imekuwa ikishinda Zanzibar lakini haipewi nafasi ya kuongoza? Huoni kama ushauri huo ulikuwa unaifaa sana CUF, ambao waliwahi kuwa na kauli mbiu ya mapanga shaa?

  Umetukosea sana CHADEMA, tafadhari tuombe radhi. Sisi hatukuwahi kuwa na mwelekeo huo wa kuleta vita.
   
 14. K

  KALAMAZOO JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA - CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO
  Hata kama kingekuwa sio chama cha wachaga,walichemsha kwa Padri Slaa.Alilisaliti kanisa,akaiba mke wa mtu,ana hasira,ni msema hovyo.hafaiiiii
   
 15. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kuna mdau mmoja alisema kuwa Tanzania inahitaji kiongozi Dikteta anayejua shida ya Watanzania
  na mwenye dhamira ya kweli kuwakomboa. Mara nyingine ni bora viboko vitembee kwa maslahi ya nchi na watanzania
   
 16. Ngolinda

  Ngolinda Senior Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasaa kumbe unajua mawazo yako ni mgando, then unataka tuchangie hoja yako?
   
 17. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ndallo,
  Ni kweli hujakosea. Slaa hawezi kucheka wakati ndugu zake miaka 50 baada ya uhuru wanalilia ngozi wakati wachakachuaji wanalalia vono na wanaishi kwenye maghorofa bei mbaya kwa fedha za kiufisadi na uwizi. slaa hawezi kucheka wakati wananchi walio wengi wanaishi hawana uhakika wa mlo wao wa siku. Anayecheka ni yule tu anayesaza bila kugharimia kwa jasho lako au ananufaika kwa migongo ya Mafisadi na mfumo mbovu. Slaa hawezi kucheka wakati kwa dhahiri kabisa wachakachuaji kwa makusudi wanapiga mabomu wananchi wake wanaotaka kuchagua viongozi wao kidemokrasia kama inavyotokea jana na leo kule Buseresere Chato na kwingineko kunakofanyika kesho uchaguzi wa Madiwani, uchaguzi ambao hata sababu za kuahirishwa ni kiinimacho. Anayechekelea hali hiyo ni yule ambaye ni mbumbumbu na shabiki tu wa mambo asiyejua kinachoendelea katika nchi yake au kwa makusudi tu kwa sababu ya kiushabiki au kiulaji hataki kuelewa kuwa mambo siyo sawa. Ningeweza kuendelea zaidi na zaidi. Tucheke panapostahili kucheka, tufurahi palipo na sababu ya kufurahi. Lakini tuwe na "Hasira kali" kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Ukombozi kwa dhana yake ni lazima uendane na hasira isipokuwa kwa wale wasiojua maana ya ukombozi au mchakato wa ukombozi. Hao ni wa kusamehewa bure wala msiwatukane kwa sababu tunawajibu wa kuwakomboa na wao pia.

   
 18. F

  Froida JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Propaganda za kijinga kabisa na zilizopitwa na wakati kaa endekeza mambo ya ukabila na kidini ukidhani ndio maendeleo ya nchi we mpuuzi kabisa hakuna atakeyedanganyika CDM ni chama cha wananchi ngoja kidogo utaona cheche zake muda si mrefu
   
 19. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #19
  Nov 27, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  CHADEMA si kama CUF kwamba watanunuliwa kwa Tende na Alua. Chadema ni nguvu ya Umma na wakati unakaribia.
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Asante dr wa ukweli umesema kila kitu wala sina cha kuongeza, tatizo wadanganyika walowengi wamefumbwa macho na hawawezi kuona hata kidogo na huu ndo unakuwa mtaji wa mafisadi. Most of our people have been brainwashed na kamwe nchi hii haitaendelea as long as ccm wako madarakani. Ni kikundi kidogo cha watu ambao hawataki kamwe keki yetu tule wote bali wafaidi wao na familia zao!
   
Loading...