CHADEMA Hai kimemvua uanachama aliyekua Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya Hai ndg James Mushi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Akitangaza kuvuliwa kwa uachama wa Chama hicho leo, mbele ya waandishi kaimu mwenyekiti wa Chama hicho wilaya ya Hai Dr Joe Nkya amesema kamati tendaji ya Chama wilaya ya Hai imechukua uamuzi huo baada ya kutokuridhishwa na matendo ya mwenyekiti huyo wa zama.

Amesema bwana James Mushi amekua akiwakashifu viongozi wa Chama hicho kuanzia Wilaya hadi Taifa kwa kutoa kauli za kejeli na matusi kinyume na katiba ya Chama. Pia amekua akikihujumu chama hicho katika sekta mbalimbali kwa ajili ya manufaa yake binafsi na washirika wake.

Amesema kuwa kamati tendaji imejiridhisha pasipo shaka kwamba bwana James ametenda makosa hayo hata alipokemewa aliendelea kukiuka maagizo ya Chama na hivyo kuanzia leo amefukuzwa rasmi ndani ya CHADEMA.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mh Helga Mchomvu amewashutumu madiwa watatu wa Chama hicho waliojiuzulu hivi karibuni kwa kununuliwa bila kujali kwamba wanawaongezea mzigo wananchi waliyowapa ridhaa ya kuwaongoza katika kata zao.

Mh Helga amesema kuwa madiwani hao walikua wameshaanza kuonyesha viashiria vya kwenda kinyume na maadili ya ki - upinzani hata katika uwajibikaji kwa muda mrefu.

Amesema kwamba madiwani hao wanawaongezea mzigo wananchi wao kwa kuingia kwenye uchaguzi ambao unagharimu fedha nyingi ambazo zingeingia kwenye matumizi mengine mfano kuongeza madawa Hospitalini nk.

Mh Helga amesema madiwani hao waliokubali kununuliwa hawajawatendea haki wapiga kura wao na kusema Chama km Chama kitaingia kwenye uchaguzi kwa kujiamini na kitashinda kwakua kimepeleka maendeleo katika Halmashauri katika maeneo yote kulingana na Bajeti ya serikali.

Katika mkutano na waandishi wa habari, baadhi ya madiwani wanaosadikiwa nao wako mbioni kuondoka ndani ya CHADEMA wamekanusha vikali kuondoka ndani ya CHADEMA na kusema wanaoneza uvumi huo ni mawakala wa CCM.

Wamesema ni kweli baadhi yao wamekua wakifuatwa hadi usiku wa manane baadhi ya watu wasiojulikana wakishirikiana na diwani mmoja aliyeachia ngazi kwa kigezo cha kupewa Mil 30 lkn wamekua wakiwakatalia.

Baadhi ya madiwani hao wameomba CHADEMA kuwawekekea ulinzi kwani wanahofia maisha yao kutokana na kufuatwa nyumbani usiku wa manane usiku wakishawishiwa wapokee mil 30 ili wajivue udiwani pamoja uanachama ndani ya CDM.
 
Hao wanaoletewa pesa kwanini wasizipokee tu halafu wakazipeleka kwenye kata zao mfano shule au hospitali halafu wanaendelea kubaki ndani ya chama kama kawaida.



Sent using Jamii Forums mobile app

Thubutu, upokee hela ya CCM kisha ugome kuhama. Ki ujumla ili kujiweka huru ni bora kugoma kuchukua hiyo hela na ikiwezekana ni kuwawekea mtego ili utumike na takukuru japo sidhani kwa suala la CCM takukuru watanya lolote.

Kitu kingine napata shaka kidogo sioni diwani mwenye ubavu wa kukataa 30m cash kwa ukata huu.
 
Thubutu, upokee hela ya ccm kisha ugome kuhama, sio ndio watakulawiti bila mate? Ki ujumla ili kujiweka huru ni bora kugoma kuchukua hiyo hela na ikiwezekana ni kuwawekea mtego ili utumike na takukuru japo sidhani kwa suala la ccm takukuru watanya lolote. Kitu kingine napata shaka kidogo sioni diwani mwenye ubavu wa kukataa 30m cash kwa ukata huu.
Lakini hawa wanapaswa kuelewa hakuna msaliti atakaeishi kwa amani!

Wamkumbuke Yuda Iskariote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh !!, milioni 30 kwa diwani !!??

Ni ngumu sana kuziachia iwapo shida ya diwani huyo ni fedha tu !!

Hata akimaliza miaka yake mitano, kamwe hawezi kuzipata hizo kama kiinua mgongo chake changanya na posho za miaka yake yote mi5 + mishahara yake yote !!

Ama kweli Chama Cha Makinikia, CCM ni noma kwelikweli na wanaendesha uhayawani wa kiwango cha kutisha sana..

Cha kujiuliza, ni kuwa, hizi fedha wanakuwa wanazitoa wapi kuwahonga watu eti tu waache nafasi zao za uongozi wa kuchaguliwa ? Na ili iweje eti ?

Je, hii inawezekana ndiyo kazi maalumu ya Dotto (Pay Master General) mpwa wa Magufuli à pale hazina ktk fuko la fedha za wananchi kuidhinisha malipo haramu ya namna hii ???
 
"Amesema bwana James Mushi amekua akiwakashifu viongozi wa Chama hicho kuanzia Wilaya hadi Taifa kwa kutoa kauli za kejeli na matusi kinyume na katiba ya Chama. Pia amekua akikihujumu chama hicho katika sekta mbalimbali kwa ajili ya manufaa yake binafsi na washirika wake."

wahenga wanauliza aliitwa na kuhojiwa na kujitetea??

"Wamesema ni kweli baadhi yao wamekua wakifuatwa hadi usiku wa manane baadhi ya watu wasiojulikana wakishirikiana na diwani mmoja aliyeachia ngazi kwa kigezo cha kupewa Mil 30 lkn wamekua wakiwakatalia."

wahenga wanauliza TAKUKURU haipo jamani??na je, kesi yao imefika huko hata kwa polisi imefika??

"Mh Helga amesema kuwa madiwani hao walikua wameshaanza kuonyesha viashiria vya kwenda kinyume na maadili ya ki - upinzani hata katika uwajibikaji kwa muda mrefu."

je,kama chama mlipoona dalili hizo mlichukua hatua gani??
 
"Amesema bwana James Mushi amekua akiwakashifu viongozi wa Chama hicho kuanzia Wilaya hadi Taifa kwa kutoa kauli za kejeli na matusi kinyume na katiba ya Chama. Pia amekua akikihujumu chama hicho katika sekta mbalimbali kwa ajili ya manufaa yake binafsi na washirika wake."

wahenga wanauliza aliitwa na kuhojiwa na kujitetea??

"Wamesema ni kweli baadhi yao wamekua wakifuatwa hadi usiku wa manane baadhi ya watu wasiojulikana wakishirikiana na diwani mmoja aliyeachia ngazi kwa kigezo cha kupewa Mil 30 lkn wamekua wakiwakatalia."

wahenga wanauliza TAKUKURU haipo jamani??na je, kesi yao imefika huko hata kwa polisi imefika??

"Mh Helga amesema kuwa madiwani hao walikua wameshaanza kuonyesha viashiria vya kwenda kinyume na maadili ya ki - upinzani hata katika uwajibikaji kwa muda mrefu."

je,kama chama mlipoona dalili hizo mlichukua hatua gani??
Uongoo. uongooo. na propaganda zenu ufipa zitawaaangamizaaaa. kwa nini msitamke visingizio vingineee??? kwani kuhama chama sikila mtu anautashi wake?? je kama mnauhakika kwamba wananunuliwa kwa nini msiwe mnawapeleka takukuru?? au mnawaonya mapema??
Tumechoka propaganda za ufipa hapa jukwaaaniii.
 
Nje ya mada kabisa....

Nahisi labda unasumbuliwa na Lowassa & Lissuphobia syndromes

Tafadhali, mwone daktari mapema kabla hazipanda kichwani !!
Read between the lines.. Huyo Mushi yeye alikuwa wa kwanza kuihama chadema tangia mwanzoni mwa wiki, leo eti mnatangaza mmemvua uanachama..

Watu makini wanakimbia hicho kichaka cha waizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom