CHADEMA Geita wamtolea uvivu Shibuda;Wataka aondolewa CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Geita wamtolea uvivu Shibuda;Wataka aondolewa CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanta, Jul 1, 2011.

 1. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CHAMA CHA DEMOKARASIA NA MAENDELEO (CHADEMA WILAYA YA GEITA)
  OFISI YA WILAYA -CHADEMA
  KALANGALALA- GEITA
  Email: geita@chadema.or.tz Website: www.chadema.or.tz
  Date: 1[SUP]st[/SUP] July, 2011

  Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Wilaya ya Geita kimetoa tamko kali juu ya mwenendo wa kauli na msimamo wa Mh. John Shibuda, mbunge wa Maswa Magharibi anapokuwa akichangia hoja mbalimbali awapo Bungeni na Nje ya Bunge. Kupitia kikao cha tamko la chama kilichokaa mnamo tar.30.06.2011 majira ya saa 4 :30 asubuhi ndani ya ofisi ya Chadema wilaya ya Geita kilichowahusisha viongozi wote wa majimbo ya Geita,Nyang`hwale na Busanda kikiongozwa na uongozi wa Baraza la mashauliano la Chadema wilaya ya Geita kimeadhimia kwa pamoja na kuwa na tamko moja la kuushauri uongozi wa ngazi za juu za chama na vikao vyake kumwajibisha Mh. Shibuda (MB) kwa kumfukuza kabisa ndani ya chama chetu cha Chadema kutokana na mwenendo mbovu ambao amekuwa akiuonyesha tangu alipochaguliwa kama mbunge wa Maswa magharibi kupitia Chadema.

  Sisi sote tukiwa ni viongozi wa Chama cha Chadema wilaya ya Geita tukiwawakilisha wanachama wote na wapenzi wa Chadema ndani ya wilaya ya Geita na sehemu zingine ndani ya Tanzania tumekuwa tukifuatilia mwenendo wa Mbunge huyu na kumwona kuwa si mwanachadema kwa uhalisi wake bali ni mtu tu asiyekuwa na imani yoyote ile ya sera na falsafa za chama chetu ambazo zinalenga kuwatetea Watanzania kuondokana na sera mbovu za CCM zisizotekelezeka na ambazo zimewafanya watazania waendelee kubaki katika lindi la umasikini uliopindukia ndani ya taifa lililojaliwa utajili wa kila namna, bali Mh, Shibuda ameonekana kuwa ni mtu aliyekosa maslahi yake kupitia CCM pale aliposhindwa kula za maoni na kukimbilia Chadema ili kutimiza kupata maslahi yake binafsi na kushibisha tumbo lake.

  Sisi kama Chadema Geita tunamwona Shibuda kama Kansa, au kirusi ama fungusi nda ya mwili mzuri wa Chadema ambavyo vyote kwa pamoja visipoondolewa mara moja vinaweza kuufanya mwili mzima wa Chadema ukaendelea kuathirika,kudhoofu na hatimaye kufa kabisa na kusababisha ile ndoto nzima, imani na matumaini ya Watanzania waliokwisha jenga imani juu ya kutetewa na kukombolewa kupitia sera safi za chadema kuwa zimezima kabisa. Hii inatokana na Mh,Shibuda kutokuwa na mwelekeo mmoja na Chama chetu kuelekea kutetea sera mbadala zinazolenga kurudisha uwajibikaji wa serikali kiuongozi na kirasilimali fedha katika kuwaendeleza Wananchi wanyonge wa nchi hii.

  Bunge la Mwezi wa pili mwaka huu Shibuda alionekana akitoa hoja kwa staili yake ya ngonjela na mashairi akitoa kauli za vijembe kupingana na sera na mtazamo wa chadema kuwatetea na kufikisha kero zao kwa watawala kwa njia ya maandamano na alifikia hata kuwabeza wabunge vijana wa wa Chadema wakiwemo na viongozi wa kitaifa huku akishangiliwa na wabunge wa CCM. Haikuishia hapo hata kabla ya hapo Shibuda alipingana na msimamo wa Wabunge wa Chadema juu ya kususia hotuba ya Mh, Rais wakati wa uzinduzi wa Bunge na hata pale wabunge wa Chadema walipoweka msimamo wa kususia chakula cha jioni kilichoandaliwa na ikulu ya Dodoma ili kupongezana baada ya uchaguzi yeye alionekana kwenye chakula hicho,na kila anapoulizwa hutoa kauli za ajabu ajabu.

  Haikuishia hapo, Bunge hili la budgeti pia ameonyesha kituko cha maajabu sana pale alipoonekana kupingana vikali kwa vijembe vikali juu ya azimio na sera ya Chama iliyokuwepo hata kwenye ilani ya uchaguzi ya Chadema_2010 na hata kupitia bajeti ya kambi rasimi ya upinzani iliyowakilishwa ndani ya bunge la bajeti ya 2011/2012 ambayo pia ilikuwa na mapendekezo hayo hayo ya kufuta sheria ya posho kwa wabunge wote na watumishi wote wa umma kwa kuboresha mishahara kwa watumishi wote wa umma kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za watawala ili kurudisha uwajibikaji wa kizalendo kwa utumishi wa umma na kuondoa ufujaji wa fedha za walipa kodi wa wa Tanzania,huku akijiita yeye ni mbunge wa maslahi jamii na kuwaita wabunge wengine wa Chadema kwamba ni wabunge maslahi binafsi.

  Sisi wana chadema wa Geita tunamuona Mbunge huyu wa Chadema hayuko kabisa na Chadema katika lengo moja la sera mbadala za Chadema za kuwakomboa watanzania bali yupo kwa ajili ya kutetea maslahi yake na kuwafurahisha Wana CCM na Serikali yao kama anavyodai siku zote kwamba hapendi CCM ife kwani Chadema itakosa mtani wa Jadi. Sisi wana Chadema tunakosa imani kabisa na Mheshimiwa huyu kwani hata mwenendo wake ndani ya chama chake cha Mapinduzi awali haukueleweka kabisa, kwa maana hiyo bwana huyu akiachwa ndani ya chama chetu atazidi kujenga ubinafsi na mgawanyiko na kuendelea kudhoofisha chama chetu katika adhima yake ya kuwakomboa Watanzania masikini wa Nchi hii kwa kuwa ni mtu ambaye anaoonekana kutobadilika kabisa na hataki kubadilika hata kidogo.

  Mwisho kabisa Chadema Geita kinashahauri vikao vya juu kutodharau na kupuuza juu ya mawazo ya viongozi wa chini na Wanachama kwa ujumla tunaoona na kusikia hata Watanzania wa kawaida wakikosa kabisa imani kutoka kwa mbunge huyu ma kumwona kama pandikizzi la CCM ili kukivuruga Chadema kuelekea kutimiza azima ya kuwakomboa Watanzania katika kuondokana sera za kibinafsi,kidikteta,na kinyonyaji za chama cha Mapinduzi na Serikali yake.

  Chama Geita kinapendekeza na kutoa angalizo kwamba endapo mtu huyu ataachwa bila kupewa adhabu kali ya kufukuzwa ndani ya Chama atakuwa mwiba mkali siku za usoni na tunatoa angalizo tusije tukaikumbuka ile methali ya wahenga waliposema `MAJUTO NI MJUKUU" wakati tumeshapitwa na wakati.

  Taarifa hii imeandikwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Geita kwa niaba ya Uongozi wote na Wanachama wa Wilaya ya Geita

  Rogers J Ruhega Geita

  +255 787 236 056

  My take;
  Ni kweli inabidi huyu jamaa aitwe wamkanye au afukuzwe kabisa,tunafahamu maoni ya mtu si vizuri kuyapinga lakini kwa tamko lake juu ya suala la posho ni wazi kwamba haendani na msimamo wa chama.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja...
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,873
  Trophy Points: 280
  mimi pia .......
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Zitto amenena vyema kwamba kuwa kinyume na taratibu za chama ni kosa la kuonywa na si kubwa sana ila kuwa kinyume na sera za chama chako ni 'straight red card offence'. Huyu jamaa ameshindwa kuficha kabisa u-CCM wake na mbaya zaidi kadri siku zinavyoyoma ndivyo anazidi kukengeuka.
  Alianza kunitibua pale alipohudhuria dhifa (mnuso) Ikulu wiki za mwanzo kabisa wakati CDM ilikuwa kwenye msimamo wa kutotambua matokeo yaliyompa urais Kikwete, since then huyu jamaa ni gunia la misumari kwenye chama yaani habebeki, hashauriki wala haonyeki.
   
 5. k

  kazuramimba Senior Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jamani mwacheni shujaa shibuda mbona zitto alipokuwa anafanya uozo hakusemwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake naunga mkono hoja ya Shibuda zile posho ziongezwe ndi ndogo sana.
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  AFUKUZWE kabisa kwa kutaka posho
   
 7. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  No objection!
   
 8. l

  lynndago Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila mtu ana haki ya kutoa maoni. hayo ni maoni yake yaheshimewe.
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  na picha linaendelea.
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkimfukuza mmejimaliza wenyewe ! jamaa ameisha wazidi ujanja huyo mwacheni tu alete upinzani wa kweli ndani ya CDM
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ww kila kitu huwa unaunga mkono, huna unachokataaga. Na weza kuja namtaka bintiyo kwa muda, unasema naunga mkono !
   
 12. K

  Kitwanad Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na we mwana magamba hebu tuondokeshee nuksi zako hapa!!!!! unapenda 'kirusi' shibuda aharibu chama eh. umechemka. hawezi achwa hivi hivi tu...adhabu kali inamgoja.
   
 13. S

  Stany JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Afukuzwe kwenye chama mapema,hil ni gugu kati ya ngano
   
 14. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna hatuna nyingine yoyote anayostahili kuchukuliwa Msaliti kama huyu zaidi ya kumfukuzia CCM kwenye Uozo wenzake
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Afukuzwe mara moja.Tunataka na mikoa na wilaya nyingine watoe matamko kumhusu huyu Shibuda.
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja...........afukuzwe kabisa....nimemkumbuka kilanga...aliwahi kutoa angalizo juu ya chadema kumpokea mtu huyu pamoja na Rev kishoka
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Afukuzwe mara moja.Tunataka na mikoa na wilaya nyingine watoe matamko kumhusu huyu Shibuda.

  Hizi ndizo hoja anazopenda yule engineer Bukuku wa CCM
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  maoni ya mtu na sera za chama ni vitu viwili tofauti
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hizi ndizo hoja anazopenda yule engineer Bukuku wa CCM
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mpako hapo alipofikia Shibuda inatosha. Wakati umewadia sasa kwa CHADEMA kumwonesha mlango wa kutokea na asirudi nyuma hata siku moja. Hata kama uchaguzi ukirudia jimbo likaenda kwa ccm sawa maana ni afadhi kuwa wabunge bora wachache kuliko lundo la type ya Shibuda. Arudi ccm kule kunamfaa sana maana hawasimamii chochote.
   
Loading...