Elections 2010 Chadema fuateni haya pamoja na yote yaliyotokea

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Baada ya matokeo kutangazwa nini chama cha CHADEMA kinatakiwa kufanya ili kisipoteze muelekeo wake.

  1. Kwa kuwa baada ya rais kuapishwa sheria inakataza kufungua kesi ya kupinga matokeo, basi wanachama na wanasheria wa CHADEMA watafute ushahidi wa kutosha na kuwashitaki kwa kwa wananchi ili wajue ukweli kuhusu zoezi hilo lilivyokuwa. Naamini wananchi watawaelewa na kutoa hukumu sahihi miaka mitano ijayo. Hii inawezekana kama operation Sangara ilivyofanikiwa.
  2. Kuacha kuhamasisha vurugu, na misimamo yenu iwe wazi ili kila mwanachama na mfuasi wa CHADEMA ajue wazi msimamo upi ni wa chama na upi ni wa kupika ili kukiharibia chama.
  3. Chama kujitambua kuwa safari ya mageuzi ndiyo imeanza na ushindi ulipatikana ni sehemu ya juhudi ya viongozi waliopo sasa, hivyo basi kukaa chini na wabunge wote wateule wa chama kijipanga jinsi ya kuweza kukiinua chama.
  4. Wabunge wake kuwa chachu ya maendeleo, bunge la 2005 kulikua na wabunge watano tu wa kuchaguliwa ukitoa wale wa viti maalum. Cheche walizotema bungeni leo hii imezaa wabunge zaidi. Wang'oe, wafichue harufu yoyoye ya ufisadi.
  5. Wapigane kufa na kupona apatikane tume huru ya uchaguzi ili kukwepa kudhulumiwa haki yao na wananchi waliowapigia kura.
  6. Kuandaa mitaji mingine ya kisiasa. Leo tuna Dr. Slaa ambaye sasa ana miaka 65, miaka mitano baadae atakuwa ni mzee hivyo kukiweka chama rehani kwa kumtegemea umaarufu wa mtu mmoja. Angalia alikuwepo Mrema, Lipumba na Mbatia ambao wameshapoteza mvuto wa kisiasa na vyama vyao ndiyo hivyo vipo shimoni.
Mwisho itambue kuwa kuwa chama hicho kinawindwa kwa udi na uvumba kife,kisambaratike au kikose mwelekeo kabisa ili ipatikane ahueni kwa chama tawala.
Wana JF changieni mengine hayo ndiyo yangu kwa chama cha CHADEMA.A
 
.
Mawazo mazuri sana ndugu na pia watafute sababu za kushuka umaarufu kwa wale wote ambao walishawahi kugombea urais na kukosa kupitia kambi ya upinzani ili kujua ni njia zipi wapitie ili waendelee kung'ara na kuzidi kukuimarisha chama.
 
Tatizo siyo chadema na viongozi (watu) ilonao, kwa mtazamo wangu tatizo ni mfumo mzima wa jinsi watanzania tulio wengi wa kufikiri na kutekeleza yale tunayofikiri.
 
Chadema wana haki ya kupinga uchaguzi huu naomba niweke sehemu ya uamuzi wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Attorney General & Others v. Dr. Amani Walid Kaborou (1996} TLR 156 ambapo Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu Nyalali, Robert Kisanga na Lameck Mfalila ilitoa uamuzi juu ya umuhimu wa kuendesha uchaguzi huru na haki. Na vilevile ilisema wazi kuwa hakuna kinga yoyote ile ya kikatiba dhidi ya maamuzi ya Tume ya Uchaguzi ambayo ni kinyume cha sheria. Nitajitahdi kuiweka hukumu nzima ili watu wajisomee. Naomba radhi kwa makosa yanayoonekana kwani katika kuitoa katika pdf mfumo umeshindwa kufanya kazi inavyotakiwa.

We now come to our reasons in support of our findings on ground number one in both memoranda of appeal concerning the validity of the Tamko Rasmi. We begin naturally by considering whether courts of law have jurisdiction to inquire into the validity of the Tamko Rasmi in view of the provisions of sub-article (12) of article 74 of the Constitution. That sub-article as amended by Act 4 of 1992 states:

'No Court shall have jurisdiction to inquire into anything done by the Electoral Commission in the exercise of its functions according to the provisions of this Constitution.'

On the face of it, it appears that the Constitution expressly prohibits the courts from inquiring into the validity of such things like the Tamko Rasmi, but on a deeper consideration of the principles that underlie the Constitution, it is obvious that such an interpretation of the Constitution is wrong. One of the fundamental principles of any democratic constitution, including ours, is the Rule of Law. The Principle is so obvious and elementary in a democracy, that it does not have to be expressly stated in a democratic constitution. However, perhaps for purposes of clarity, there is an express provision to that effect under the Constitution of the United Republic of Tanzania. It is Sub-Article (1) of Article 26 which states:

'Every person is obliged to comply with this Constitution and the laws of the United Republic.'

In the light of this principle, we respectfully agree with the sub- mission of Mr Werema Learned Senior State Attorney to the effect that Sub-Article (12) of Article 73 of the Constitution cannot be interpreted so as to protect unconstitutional or illegal acts or deeds, see the recent famous case of Anismic Ltd v. Foreign Compensation Commission (1).
Since Tanzania has reverted to dejure multi- party democracy, it is time the same was similarly articulated here. We are satisfied and we find that the High Court in this country, like the High Court in England, has a supervisory jurisdiction to inquire into the legality of anything done or made by public authorities such as the Tamko Rasmi. As a collorary, this Court has similar jurisdiction to do so in a matter properly before it, as in the present case.

We now come to our reasons in support of our finding to the effect that the Electoral Commission is empowered to make and issue the Tamko Rasmi but under the circumstances of this case, the Tamko Rasmi is invalid. It is patently clear that the Electoral Commission derives its powers under the Constitution and the Elections Act, 1985 as amended from time to time. Under para (b) of sub-article (6) of article 74 as amended by Act 4 of 1992, read together with ss (2) of s 4 of the Elections Act, 1985 as amended by Act 6 of 1992.

In our considered opinion, we are satisfied that on a true and proper interpretation of the above cited provisions of the Elections Act, the Electoral Commission is empowered to make regulations not only in furtherance of specific provisions of the Act, but also in furtherance of the purposes of the whole Act. From the scheme of the Act as manifested in the various provisions of the Act, including the provisions for secrecy of the ballot and for polling agents, counting agents, one person one vote, one candidate one seat, as well as those provisions concerning election campaigns and election offences, it is evident that the overriding purpose of the Elections Act is to secure the election of the President of the United Republic and the members of the parliament of the United Republic in a free and fair election. It is also implicit from the provisions of the Constitution.

Majaji wakaendelea kusema

As we have already stated, we concur with the reasons given by Mchome J, and we have additional reasons for upholding his finding. First, weare satisfied that the established rule of interpretation embodied in the Latin Maxim 'Expressio Unius EST Exclusio Alterius' that is, where matters are expressly stated, then any other matters of the same class not so expressly slated are excluded, does not apply to s.108 because that section provides defences to matters which are not expressly stated therein. Second, taking into account the principle which underlies the Constitution and the Elections Act, 1985 that elections shall be free and fair, we are of the considered opinion that an election which is generally unfree and unfair is not an election at all as envisaged by the Constitution and the Elections Act, and consequently anything which renders the elections unfree or, and unfair is in law valid ground for nullification of such purported D election. We are further of the considered opinion that any law which seeks to protect unfree and unfair elections from nullification would be unconstitutional.
 
Mzee inauma sana pale watu wanapoamua kisha watu wanafanya wanavyojisikia. Nionavyo mimi uelewa wa sasawa wananchi ni mkubwa sana lakini tatizo lipo kwenye uwasilishaji wa matokeo/maamuzi hayo ya wananchi.
 
Back
Top Bottom