Elections 2010 Chadema fuateni haya pamoja na yote yaliyotokea.

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,173
3,328
Baada ya matokeo kutangazwa nini chama cha CHADEMA kinatakiwa kufanya ili kisipoteze muelekeo wake.

  1. Kwa kuwa baada ya rais kuapishwa sheria inakataza kufungua kesi ya kupinga matokeo, basi wanachama na wanasheria wa CHADEMA watafute ushahidi wa kutosha na kuwashitaki kwa kwa wananchi ili wajue ukweli kuhusu zoezi hilo lilivyokuwa. Naamini wananchi watawaelewa na kutoa hukumu sahihi miaka mitano ijayo. Hii inawezekana kama operation Sangara ilivyofanikiwa.
  2. Kuacha kuhamasisha vurugu, na misimamo yenu iwe wazi ili kila mwanachama na mfuasi wa CHADEMA ajue wazi msimamo upi ni wa chama na upi ni wa kupika ili kukiharibia chama.
  3. Chama kujitambua kuwa safari ya mageuzi ndiyo imeanza na ushindi ulipatikana ni sehemu ya juhudi ya viongozi waliopo sasa, hivyo basi kukaa chini na wabunge wote wateule wa chama kijipanga jinsi ya kuweza kukiinua chama.
  4. Wabunge wake kuwa chachu ya maendeleo, bunge la 2005 kulikua na wabunge watano tu wa kuchaguliwa ukitoa wale wa viti maalum. Cheche walizotema bungeni leo hii imezaa wabunge zaidi. Wang'oe, wafichue harufu yoyoye ya ufisadi.
  5. Wapigane kufa na kupona apatikane tume huru ya uchaguzi ili kukwepa kudhulumiwa haki yao na wananchi waliowapigia kura.
  6. Kuandaa mitaji mingine ya kisiasa. Leo tuna Dr. Slaa ambaye sasa ana miaka 65, miaka mitano baadae atakuwa ni mzee hivyo kukiweka chama rehani kwa kumtegemea umaarufu wa mtu mmoja. Angalia alikuwepo Mrema, Lipumba na Mbatia ambao wameshapoteza mvuto wa kisiasa na vyama vyao ndiyo hivyo vipo shimoni.
Mwisho itambue kuwa kuwa chama hicho kinawindwa kwa udi na uvumba kife,kisambaratike au kikose mwelekeo kabisa ili ipatikane ahueni kwa chama tawala.
Wana JF changieni mengine hayo ndiyo yangu kwa chama cha CHADEMA.A
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom