CHADEMA flip flopping at its best! Jisomee mwenyewe uone

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
92
Naam zifuatazo ni baadhi ya wuote ambazo nimezitoa katika vyombo viwili tofauti (gazeti la majira na tanzania daima la mbowe)

"Binafsi sioni umuhimu wa kuundwa kwa kamati hii, kwa ajili ya kuchunguza mikataba ya madini kutokana na sababu mbalimbali, lakini sababu kubwa hata historia inaonesha, hakuna ripoti au taarifa yoyote ambayo imetolewa kutokana na kamati hizo kuundwa na hii kamati ya Jaji na Zitto ni ya tano," alisema Bw. Lissu

HAPO HAPO SLAA(ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema) AKASEMA :

Sisi CHADEMA tunaona ni vyema Zitto akakubali kuwa mjumbe wa kamati hiyo, na pale tutakapoona vinginevyo, tutashauriana," alisema Dk. Slaa alipozungumza na Tanzania Daima kwa simu kutoka Dodoma.

TENA LISSU AKAJA AKASEMA "
"Kutokana na Kamati ya Rais kukosa nguvu, sioni hata sababu ya Bw. Zitto kuwamo, kwani ni sawa na kuwa katika ofisi ambayo huna kazi ya kufanya na kibaya zaidi, wajumbe wenzake wengi hawatafanya kazi kama wananchi wanavyotarajia kutokana na wengi wao kuwa maswahiba wa viongozi wanaotuhumiwa kutumia nafasi zao kuingia mikataba ambayo haina manufaa kwa Watanzania,"

HALAFU MSIKIE TENA SLAA ALIVYOSEMA :
"Hayo yanayosemwa si tamko la chama, kila mmoja ana haki ya kutoa maoni yake kutokana na sababu zao, lakini msimamo wa chama tunakubaliana na Zitto kuwepo kwenye kamati hiyo, hakuna mgogoro wa aina yoyote."

HALAFU KIDOGO TENA AKASEMA"
"Pia mimi kama Katibu Mkuu wa CHADEMA, sijapokea malalamiko yoyote kuhusiana na suala hili," alisema Dk. Slaa.

ONA SASA LISSU ALICHOSEMA TENA"
"Kama kweli alisema ukweli kuwa mikataba yote imepitiwa na haina matatizo, kwa nini Rais ameunda Kamati ya kufutalia mikabata hiyo, kwa mantiki hiyo utagundua wazi kuwa wabunge waliongopewa na Bw. Karamagi na kwa maana hiyo, hoja za Upinzani kutaka Kamati Teule, ilikuwa na nguvu na ya msingi kwa manufaa ya wananchi wote,"

SLAA AKARUDI TENA NA KUSEMA"
"Hatufanyi hivyo kwa sababu Zitto yupo katika kamati hiyo, tunataka kujua wajumbe waliochaguliwa kuunda kamati hiyo wana sifa gani," alisema Dk. Slaa.

OUT OF QUOTATIONS
Taarifa nyingine kutoka ndani ya CHADEMA zinaeleza kuwa, Rais Kikwete alimtaarifu Zitto kuhusu uteuzi huo, siku kadhaa kabla hajawahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, takriban wiki mbili zilizopita.

CONCLUSION YA BWANA SLAA
"Slaa katika ufafanuzi wake huo alisema, kauli kama ya Chacha ni maoni binafsi ya mwanachama wa CHADEMA na si msimamo rasmi wa chama, kwani kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa chama chao, wasemaji ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu ambaye ni yeye, na kusema kuwa mwanachama mmoja mmoja ana haki ya kutoa maoni yake."

KIFUNIKO"

Alitoa kauli hiyo baada ya jana gazeti la Mtanzania kuandika habari yenye kichwa kisemacho; ‘Zitto matatani tena' iliyokuwa ikieleza kuwapo kwa upinzani ndani ya chama hicho cha upinzani baada ya kuteuliwa kwake kuwa mjumbe katika kamati hiyo.

Gazeti hilo, lilikariri maneno yanayodaiwa kuwa yalizungumzwa na kada mwingine wa chama hicho cha upinzani, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.

Chacha, mmoja wa wabunge machachari, alidaiwa kutoa maoni hayo wakati alipokuwa akizungumza na mbunge mwenzake mmoja, na akashauri Zitto ajitoe katika kamati hiyo.

Slaa katika ufafanuzi wake huo alisema, kauli kama ya Chacha ni maoni binafsi ya mwanachama wa CHADEMA na si msimamo rasmi wa chama, kwani kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa chama chao, wasemaji ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu ambaye ni yeye, na kusema kuwa mwanachama mmoja mmoja ana haki ya kutoa maoni yake (Ndio Slaa endelea kugandamiza wanachama wako, maana wewe na mbowe tu ndio wenye haki ya kutoa kauli, ebu waambie hao halafu wafuate na hawa wa JF)
KUNANI NDANI YA CHADEMA ????

SOURCES: News Archives - The Free Media of 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

NA

http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4622
 
Good job kaka, wata tamani kumeza maneno yao mwaka huu!!.
 
Naam zifuatazo ni baadhi ya wuote ambazo nimezitoa katika vyombo viwili tofauti (gazeti la majira na tanzania daima la mbowe)


HAPO HAPO SLAA(ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema) AKASEMA :

Sisi CHADEMA tunaona ni vyema Zitto akakubali kuwa mjumbe wa kamati hiyo, na pale tutakapoona vinginevyo, tutashauriana,” alisema Dk. Slaa alipozungumza na Tanzania Daima kwa simu kutoka Dodoma.


Slaa katika ufafanuzi wake huo alisema, kauli kama ya Chacha ni maoni binafsi ya mwanachama wa CHADEMA na si msimamo rasmi wa chama, kwani kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa chama chao, wasemaji ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu ambaye ni yeye, na kusema kuwa mwanachama mmoja mmoja ana haki ya kutoa maoni yake[/SIZE][/COLOR] (Ndio Slaa endelea kugandamiza wanachama wako, maana wewe na mbowe tu ndio wenye haki ya kutoa kauli, ebu waambie hao halafu wafuate na hawa wa JF)
KUNANI NDANI YA CHADEMA ????[/COLOR]

SOURCES: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/17/habari1.php

NA

http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4622

Unafanya kazi nzuri ya mabwana(masters) wako eeeheh

Soma vizuri kauli ya Slaa "CHADEMA tunaona ni vyema Zitto akakubali kuwa mjumbe wa kamati hiyo, na pale tutakapoona vinginevyo, tutashauriana", unaelewa maana yake?

Soma katiba ya CHADEMA uone wasemaji wakuu wa chama ni wakina nani lakini utaona katika katiba hiyo pia wanachama wana haki ya kutoa maoni.

Mwanakijiji, mtafute Lissu ufanye naye mahojiano tujue ukweli na UNDANI wa alichokisema DDC Mlimani, mi siliamini kabisa MAJIRA!

CHADEMA mko wapi? Njooni mtoe ufafanuzi

Asha
 
Watanzania Mtakuwa wataalamu wa Bla bla sasa, hata hili nalo mnataka kusema ni rocket science, tume imeundwa kuangalia mambo kwa mapana, hii tume haina uhusiano wa karibu sana na Karamagi, Msabaha, Yona, Kikwete,Majogo, na Mawaziri wengine wote waliopitia pale wizara ya madini!

Tume hii tuangalia kwa mapana masilahi ya taifa;

Chonde Chonde wanaCHADEMA na wanaCCM, msione kama nchi hii ni ya kwenu wenyewe, ni yetu pia sisi tusiokuwa na pa kusemea!!!

We make us tired of these politics!!!
 
KadaMpinzani,

Mjomba sijaona kitu cha kushangaza hapa zaidi ya wewe kuwapandisha chati CHADEMA kuwa ni chama chenye demokrasia ya kweli. Unajua ktk mfumo wa demokrasia viongozi wa chama kimoja wanaweza kuwa na msimamo tofauti ktk hoja moja na wakauweka wazi bila kufuata Upepo kama tunavyoyaona CCM.

Huko Marekani majuzi kulikuwa na swala la kuwapa Kibali cha kuishi wazamiaji (Alliens) toka Mexico. Ndani ya vyama vyote viwili - Democratic/Republican kulikuwa na viongozi waliokuwa wakipingana ktk msimamo wao kuhusiana na hoja hiyo. Na hata ilipofikia wakati wa kupiga kura upande mmoja ule unaopinga walishinda lakini wajumbe wake walitoka vyama tofauti pamoja na kwamba hili lilikuwa pendekezo na ilani ya Republican chini ya Utawala wa Bush.

Ingekuwa Bongo na hasa CCM swala hili lingepita bila kupingwa kwa sababu sisi hatuna viongozi ila watawala, wasemacho wao ndio uamuzi wa mwisho. Kwa hiyo bob, kama nimeelewa vizuri maelezo hayo hapo juu nadhani ulichoshindwa kuelewa ni kwamba DR. Slaa anaeleza msimamo wa chama (wengi wape) pamoja na kuwa wapo wajumbe waliopinga.

Bila shaka ingekuwa busara kwetu kutazama kwa undani faida ya kamati hiyo na kuchambua maelezo ya pande zote mbili INAYOUNGA MKONO/INAYOPINGA kwa sababu wote hawa wanagongana kimawazo kama wawakilishi wetu sisi na sio kufuata mkondo utadhani kundi la ng'ombe wakipelekwa malishoni.

Hongera sana Chadema kwa kuwa na mgongano wa kimawazo ambao sisi tumeweza kuuona nje tofauti kabisa na itikadi za Kitawala ambako asemacho mkubwa hakina Upinzani.

Kada mtapata taabu sana CCM mwaka huu kwani hamkuzoea kupata Upinzani ndani ya chama ama nje. Asemacho mzee hakina Upinzani kama alivyosema Mzee wetu |Mwalimu Augustine Moshi ktk chaguzi zenu kuwa ukisema HAPANA humaanisha hapana mwingine.
 
Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa




na Ratifa Baranyikwa



IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.
Kwamba baadhi ya wajumbe hao, walihusika katika utiaji saini mkataba wa Buzwagi na mmoja wa wajumbe wa kamati ni rafiki mkubwa wa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni jambo linalotia shaka kuhusu kuteuliwa kwao katika kamati hiyo.

Hayo yalibainishwa jana katika kongamano la wanavyuo la kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani, lililohudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali, wakiwemo madaktari, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati na wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Kongomano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa DDC mkabala na Mlimani City, karibu na kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Wachangiaji wengi katika mdahalo huo, walieleza kuwa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Kikwete ni kiini macho cha kuwaghilibu Watanzania, ili wasiendelee kuhoji kuhusu utata unaodaiwa kuwepo kwenye mikataba ya madini, kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wote hawana sifa za kuunda kamati hiyo.

Wa kwanza kuelezea udhaifu wa kamati hiyo, alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibroad Slaa, ambaye alidai kwamba, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni swahiba mkubwa wa Waziri Karamagi ambaye hawezi kumtia matatani rafiki yake (Karamagi).

Dk. Slaa alimtaja mjumbe huyo kuwa ni Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), ambaye mwaka jana alialikwa bungeni na Karamagi na akatambulishwa mbele ya Bunge kuwa ni rafiki yake.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi.

“Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

“Hawa watu walikuja kufanya nini bungeni? Tunafuatilia walikuja kufanya nini… hatutaki kamati kiinimacho, kamati hii haitokani na Zitto peke yake, mwishoni mwa wiki ijayo tutatoa taarifa nyingine juu ya hiyo kamati na ndiyo maana tunasema hakuna wa kumfunga paka kengele kwa sababu wote wanafahamiana,” alisema Dk. Slaa.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

“Tuna historia ya ‘ku-miss use’ hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?” alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang’enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

“Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa,” alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

“Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

“Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?” alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

“Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power’, mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi,” alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisisitiza msimamo wake kuwa amekubali uteuzi huo na kwamba atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele.

Alisema sekta ya madini inaonyesha kuwa sekta inayokuwa, lakini mchango wake kwa pato la taifa hauongezeki.

Baadhi ya watu wengine mashuhuri waliozungumza katika mdahalo huo na kuunga mkono kuwepo kwa shaka dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo, ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye pia alisisitiza mshikamano wa wasomi na kutumia usomi wao ili kuleta maendeleo.

Wengine ni mwanahabari mkongwe, Makwaiya wa Kuhenga, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu, Susan Lyimo na Dk. Azaveli Lwaitama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao wote walisisitiza nguvu ya pamoja katika kuleta mapambano ya kifikra.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela, Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM), Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Pia wamo Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
 
Kikwete amkaanga Zitto




na Charles Mullinda



SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa mjumbe katika Kamati ya Kupitia Mikataba ya Madini, dalili za awali zimeonyesha kuwa, uteuzi huo utamgharimu kisiasa mwanasiasa huyo kijana.

Habari za uhakika zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili, zinaeleza kuwa uteuzi wa Zitto katika kamati hiyo umewashitua baadhi ya viongozi wakuu serikalini na tayari wamekwishawaagiza wapambe wao kumshughulikia mbunge huyo.

Imeelezwa kuwa, wasiwasi huo wa wakubwa serikalini, unatokana na shaka kwamba, Zitto anaweza kuwa mwiba kwa udhaifu utakaobainika katika mikataba hiyo, kwa kuanika hadharani kila kitakachogunduliwa na kamati, hata kama atatakiwa kutofanya hivyo.

Hata hivyo, wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa, hatua ya Rais Kikwete kumteua Zitto kwenye kamati hiyo, inalenga kuwapa mwanya wanamtandao kumshughulikia mbunge huyo anayeonekana kuitikisa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Habari zaidi zinaeleza kuwa, Rais Kikwete ameshitushwa na mwenendo wa mambo ndani ya serikali na katika CCM, na kwamba kwa kiasi kikubwa umaarufu wa serikali yake umekuwa ukipungua, huku ule kambi ya upinzani ukizidi kuongezeka.

Kwamba Rais Kikwete kwa siku kadhaa amekuwa katika hali ya woga, hasa baada ya matukio ya kuzomewa kwa mawaziri wake, huku viongozi wengine wa serikali wakipigwa mawe na kuzodolewa na wananchi wanaoonekana kukata tamaa na uongozi wa serikali yake.

Taarifa nyingine zilizopatikana kutoka ndani ya kundi la wanamtandao zinaeleza kuwa, woga alionao Rais Kikwete dhidi ya kupanda kwa umaarufu wa kambi ya upinzani katika siku za hivi karibuni, ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na Zitto, umemfanya abuni mbinu mpya za kukabiliana na hali hiyo.

Mbinu ya hivi karibuni inayoelezwa kuwa imebuniwa na Rais Kikwete kuanza kumshughulikia Zitto, ni kumshirikisha katika tume hiyo ili akose sauti kubwa ya kukosoa udhaifu uliomo ndani ya mikataba ya madini.

Wachambuzi wa duru za kisiasa wanadai kwamba, serikali baada ya kushindwa kumbana Zitto kupitia Bunge, ambako Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliongoza mikakati hiyo kwa kuwaita wabunge wa CCM na kuwataka waweke msimamo wa pamoja wa kumshughulikia mwanasiasa huyo, na kwa kauli moja waliafikiana kumsimamisha kufanya shughuli za Bunge, Rais Kikwete alianza kupata hofu dhidi ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, hasa baada ya umaarufu wa kambi ya upinzani kuanza kupanda.

Wanaeleza zaidi kwamba, baada ya vuguvugu la wananchi kuwa kubwa kufuatia kusimamishwa kwa Zitto, serikali ilibuni mbinu kadhaa za kulinyamazisha, zikiwemo ziara za mawaziri mikoani kupambana na hoja za kambi ya upinzani.

Hata hatua ya Rais Kikwete kumtetea Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ambaye aliliambia Bunge kuwa mikataba yote ya madini imeshapitiwa, nayo inadaiwa kuwa moja ya mbinu za kupambana na hoja ya Zitto aliyoiibua bungeni.

Kushindwa kufanikiwa kwa mbinu hizi, ndiko kulikomfanya Rais Kikwete kubuni mbinu ya kuunda Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini, mbinu ambayo imeanza kuonyesha mafanikio.

Kwa kutumia mbinu hii, vijana wa kundi la ‘wanamtandao maslahi’ walio katika fani ya uandishi wa habari, walimhoji Zitto baada ya kutangazwa kuwa ni mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo na kumnukuu akieleza kuwa Rais Kikwete ni rais makini anayepaswa kuliongoza taifa hili kwa sasa.

Kauli hii ya Zitto, inamuonyesha kuwa kiongozi kigeugeu ambaye hivi karibuni alikuwa mstari wa mbele, pamoja na viongozi wengine wa kambi ya upinzani kumlaumu Rais Kikwete kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya ahadi zake kwa Watanzania, pamoja na kumtaja katika orodha ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Hata hivyo, baadhi ya watu walio karibu na mwanasiasa huyo, walilieleza gazeti hili kuwa, ingawa kweli Zitto alihojiwa na waandishi na habari, baadhi ya maneno yaliyoandikwa hakuyatamka, bali yameandikwa kwa lengo la kumshushia heshima yake kwa jamii.

Hatua nyingine inayodhihirisha kufanikiwa kwa mbinu hiyo, ni mgongano wa kauli za viongozi wa CHADEMA. Wakati Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe akipinga waziwazi kuteuliwa kwa Zitto katika kamati hiyo na akimtaka kujitoa mara moja, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbroad Slaa, yeye ameeleza kuwa chama kinaunga mkono kuteuliwa kwa Zitto.

Habari za hivi karibuni zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili zinaeleza kuwa, baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku wa kuamkia jana walifanya kikao kizito cha dharura cha kujadili uteuzi huo wa Zitto.

Wakati hali ya mambo ikiwa hivyo ndani ya CHADEMA, wananchi mbalimbali waliotoa maoni yao kuhusu uteuzi huo, wameonyesha shaka ya wazi kuwa huo ni mwanzo wa kumshughulikia Zitto na kauli yake kukubali uteuzi huo na kummwagia sifa Rais Kikwete ikichukuliwa kama shukrani kwa rais kumkumbuka kuwemo katika kamati hiyo.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu, ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela na Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM).

Wajumbe wengine ni Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers, Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.


Chanzo cha Habari zote mbili ni Tanzania Daima
 
sasa hii nini dada asha ??

basi mwanakijiji aje na timu yake ya ufundi hapa walau watupe mawili matatu then tusafishe koo .............!
 
sasa hii nini dada asha ??

basi mwanakijiji aje na timu yake ya ufundi hapa walau watupe mawili matatu then tusafishe koo .............!

usishtuke maneno hayo hayana pa kushika ni mabuje tu hayo.

hilo ni Tanzania Daima dada ASha katuletea ili........
 
sasa hii nini dada asha ??

basi mwanakijiji aje na timu yake ya ufundi hapa walau watupe mawili matatu then tusafishe koo .............!


Mbona umekaa kiudaku udaku saaana, hata hivyo hutajibiwa kiudaku udaku.

Chadema ni chama chenye Demokrasia ndio maana unaona kila mtu anapewa uhuru wa kutoa maoni yake.Si kama hao wa CCM waliokalishwa bungeni chini ya Lowasa eti wanapangiwa ni nini waseme na nini waache! Ndio maana kutokuwepo kwa uhuru huo nadani ya CCM kumeligharimu sana taifa letu,mfano tungeweza kupata ukweli na kunusurika na suala la Richmond,IPTL,Rada nk. kama kungekua na Demokrasia ya kweli ndani ya CCM.

Hivyo basi CHADEMA kama chama mbadala ambacho kiko makini na kinachojua jinsi udhaifu wa CCM ulivyoturudisha nyuma,kinajaribu kuwa tofauti kwa kupanua wigo wa kidemokrasia.Usishanage kuona Mhe.Mbowe akatofautiana kimaoni na Dr.Slaa but istituonally wakatoa tamko la Chama.Hii ndio Demokrasia ambayo CCM wamejima na wametunyima kwa muda mrefu

Umenipata hapo?
 
KadaMpinzani sniffs the air *mhm*
smells a CHADEMA fanatic ^^ there !

(nilipoona tu sentensi yako ya kwanza frankly i didnt dare read what you wrote)!!

kwa hiyo kusafisha koo unachukulia udaku, si ndio ? what you think it meant in that context ? nilikuwa na maana asawazishe njia kwa kujibu niliyosema then tumove on, lakini wewe sijui mtu wa wapi hata huelewi !
(Ningekushauri usome quotations then useme kama ni UDAKU au LA, kama ni udaku basi elewa huo udaku ni kati ya slaa, na wenzake niliowaquote !
lakini unaposema udaku just kwa kuwa nimeweka neno la kiswahili "koo" unanijaji by that, just shows how mdaku you are !
 
Ulianza wewe mkuu,eti slaa na Mbowe wanakandamiza wanachama hakuna mwanachama aneruhusiwa kuongea,mkuu unatakiwa kupewa darasa kidogo kubali upewwe shule uache kelele!

Suala la mtu kuwa na uhuru wa kutoa mawzao it doesnt mean that,he can call a press comference na kutoa tamko la kichama.Lazima kuwe na channel maalum otherwise itakua ni vurugu.

Otherwise uniambie what do you mean unaposema wanakandamiza wanachama.

Halafu mkuu jiangalie vizuri uelewa wako badala ya kusema wengine hawaelewi,Ulishaambiwa mara ngapi kuwa Tanzania Daima si ya Chadema.Unatakiwa kupigwa revision mara ngapi mkuu au ndio hivyo tena unazi utatufanya hata kumbukumbu zetu zichil
 
i still smell a chadema fanatic in the air !

acha nipige uluzi nitoke hadi harufu itakapopungua !
 
Uhuru wa kujieleza kwa sisiem ni mwiko. Collective responsibility ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Nchi inauzwa bei ya kutupwa " NBC", Tz Breweries, Kiwanda cha Sigara n.k. Watu wanafanya biashara Ikulu, Wageni wanaaajiriwa kwa kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya, Wageni wanafanya biashara za kimachinga bila kizuizi. Haya yote watu wanaojifanya makini, wabunge, Maprof, MaDoc walioko ndani ya sisiem wanayajua lakini wanaogopa kunyoosheana vidole. Kwa mtaji huu ni Bora uhuru uliopo Chadema kuliko unafiki ndani ya sisiem
 
Watanzania Mtakuwa wataalamu wa Bla bla sasa, hata hili nalo mnataka kusema ni rocket science, tume imeundwa kuangalia mambo kwa mapana, hii tume haina uhusiano wa karibu sana na Karamagi, Msabaha, Yona, Kikwete,Majogo, na Mawaziri wengine wote waliopitia pale wizara ya madini!

Tume hii tuangalia kwa mapana masilahi ya taifa;

Chonde Chonde wanaCHADEMA na wanaCCM, msione kama nchi hii ni ya kwenu wenyewe, ni yetu pia sisi tusiokuwa na pa kusemea!!!

We make us tired of these politics!!!

next tym b sure of usemayo...una uhakika hiyo kamati iliyoundwa members wake hawana uhusiano na watuhumiwa???ndo yale yale kesi ya ngedere anapewa nyani
 
next tym b sure of usemayo...una uhakika hiyo kamati iliyoundwa members wake hawana uhusiano na watuhumiwa???ndo yale yale kesi ya ngedere anapewa nyani

Mkuu kama maneno yako ni kweli basi wanakamati hiyo wanahitajika kutoka nchi nyingine, hivi ni nani Tanzania asiyemjua mwingine? Eti ni jaji wa mahakama gani bongo hamjui kiongozi yoyote wa CCM au upinzani? Sasa kesi zao tukazifanyie wapi?
 
Mugo"The Great";100811 said:
Uhuru wa kujieleza kwa sisiem ni mwiko. Collective responsibility ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Nchi inauzwa bei ya kutupwa " NBC", Tz Breweries, Kiwanda cha Sigara n.k. Watu wanafanya biashara Ikulu, Wageni wanaaajiriwa kwa kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya, Wageni wanafanya biashara za kimachinga bila kizuizi. Haya yote watu wanaojifanya makini, wabunge, Maprof, MaDoc walioko ndani ya sisiem wanayajua lakini wanaogopa kunyoosheana vidole. Kwa mtaji huu ni Bora uhuru uliopo Chadema kuliko unafiki ndani ya sisiem

yaani vizuri maana umekuwa open katika kutetea chadema na wapinzani wake wanavyo-opress members wake ! haya tukutane katika kujegna hoja za kusaidia taifa na sio vyama vya siasa !
 
Mkuu heshima mbele, nani ameleta hii heading "CHADEMA flip flopping at its best !! Jisomee mwenyewe uone !!" Nani kaanza kujadili vyama?
"haya tukutane katika kujegna hoja za kusaidia taifa na sio vyama vya siasa !"
Nani anatengeza sera za kujenga au kubomoa Taifa kama si vyama vya siasa? Ni kweli, kama tupo serious tujadili hoja za kujenga taifa na siyo hii ya "CHADEMA flip flopping at its best"

"yaani vizuri maana umekuwa open katika kutetea chadema na wapinzani wake wanavyo-opress members wake !"
Najaribu kulinganisha sisiem na Chadema juu ya Uhuru wa kujieleza.
 
Back
Top Bottom