Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,489
- 13,608
Miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015 katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Mama Asha Migiro walitembea nchi nzima kwa lengo maalum. Walikwenda kuiombea msamaha CCM mbele ya wananchi, walijaribu kadri walivyoweza kuirudisha CCM kwenye fikra za wananchi wa kawaida. Mzee Kinana hakusita kuwaita mizigo baadhi ya mawaziri waliyoonekana kutokuwa na msaada kwa serikali ya awamu ya nne. Wasomi wakagawanyika kimawazo kuhusiana na ziara zile za viongozi wa juu wa CCM nchi nzima.
Wapo walioamini kwamba Kinana anaongea lugha ya upinzani ambayo itachangia kukibomoa kabisa chama cha mapinduzi, lakini alichofanya kilikuwa ni sawa na mtu aliyegombana na mchumba/mke halafu akaanza kumtimia zawadi nyingi tu ili kuuteka tena moyo wa mpenzi wake.
Wakati wa kampeni kazi iliyofanywa na Kinana pamoja na migiro ikawa imeshapunguza makali ya chuki waliyokuwa nayo wananchi kwa CCM. JPM akatumia ujanja wa kujitambulisha yeye badala ya CCM huku akifanya kampeni akiwa amevaa mavazi ya CCM. Kinana na Migiro walitumia ukongwe wao kwenye siasa katika angalau kujaribu kurudisha hali kwenye ubora uliokuwepo miaka mingi nyuma kabla mafisadi hawajakichafua chama cha mapinduzi.
CHADEMA wamepata katibu mkuu mpya, wanao muda wa kutosha kuelekea 2020, huu sasa ni wakati muafaka wa kutengeneza mikakati ya ushindi sio kuendelea kutegemea kura za huruma (mahaba). CCM kwa sasa wanafanya kila njia ili waweze kuwa karibu na wananchi wa kawaida, wamelibomoa daraja lililokuwa linawatenganisha wao na wananchi wa kawaida. Waziri mkuu akiona bango njiani anasimamisha msafara na kuwasikiliza wananchi, akibipiwa anapiga muda ule ule. Hakuna tena muda wa kuunda tume za ajabuajabu kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi mambo yanayoweza kutatuliwa ndani ya siku moja ya kazi.
CHADEMA wautambue mkakati mpya wa CCM na wajipange kisayansi katika kuukabili, ili wasipotee machoni na mioyoni mwa watu ambao walikuwa sehemu ya wahudhuriaji wa mikutano yao ya kampeni. Awamu ya tano imekuja kivingine, JPM sio JK ambaye aliruhusu uzembe ambao ulitumika vizuri katika kuifanya heshima ya CCM ikapotea. JPM na wasaidizi wake wanapaswa kuwafumbua macho CHADEMA ili waje kivingine yaani kisasa zaidi kwa faida ya mtanzania wa kawaida. Ni mawazo yangu tu.