CHADEMA fanyeni hima na kuzidisha nguvu zenu kanda ya kusini (Lindi na Mtwara) CCM iko hoi

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Salaam,,

Mwisho wa wiki hii iliyoishia jana nilibahatika kutembelea kanda ya kusini nikimaanisha Lindi na Mtwara,,nilienda kikazi tokea wiki iliyopita na kunilazimu kutumia muda wangu wa weekend kuzunguka baadhi ya maeneo ya mkoa na wilaya za Mtwara. CHADEMA mmejitahid sana kujenga chama na uelewa kwa wananchi walio wengi wazee, vijana hadi wanawake.

Nimefika Newala jimbo la waziri Mkuchika , hali ni mbaya sana hana matumaini ya kuweza kutetea kiti kile na wananchi wameichoka nakupoteza tumaini moja kwa moja na chama cha mapinduzi, nguvu ya CUF nayo imefifia ukifananisha na wilaya jirani ya Tandahimba.CHADEMA mna plani gani na jimbo lile la Newala??

Mimi nadhani fursa hii siyo ya kuilazia damu, changeni karata zenu vyema jimbo la Newala linahitaji ukombozi pia.
 
Hapo umenena mkuu , ccm imechokwa hii mikoa , chadema wawekeze maeneo haya ya kusini kwani ni rahisi sana kuwaangusha maccm kwa sasa
 
Kuna ile kanda ya Zitto ya wanamtwara wanaiuliza serikali "mnatuachaje" ipelekwe Mtwara na Lindi. Ni nzuri sana ile speech
 
Back
Top Bottom