CHADEMA, familia ya Lissu na TLS rudini mezani upya

_____________________________________

Tangu juzi baada ya hotuba ya Mh Mbowe, mimi nilijawa na furaha, furaha yangu ilikuwa katika mambo mengi, lakini kubwa zaidi ilikuwa nikusikia kuwa Lissu wetu amepata ahueni na sasa anakula, anaongea anakaa na anapunga mkono.

Hii ni furaha yangu kuu, furaha ilizidi zaidi jana majira ya alasiri ambapo picha ya kwanza ya mpendwa wetu iliwekwa hadharani, pude si punde sauti yake halisi ikasikika ulimwenguni kote ikinena kwa shukrani toka vilindi na vilima vya moyo wake mkuu kuja kwetu wana wa dunia.

Naaam, katikakati ya furaha hii nilizama katika tafakuri kubwa, hasa nikiwaona Watanzania walivyojawa na furaha isiyo kifani. Tafakuri yangu ilijikita kuichambua hotuba ya Mh Mbowe neno kwa neno na huku nikiangazia hali ya usalama wa Lissu sasa na huko mbele mpaka hitaji la Mungu litimie.

Katika Hotuba yake Mh Mbowe alisema, Chadema sasa inaiachia familia ya Mh Lissu iongoze shughuli katika kipindi hiki cha matibabu awamu ya pili (rehabilitations), akasisitiza kuwa Chadema haitakuwa mbali itaendelea kuwa bega kwa bega na familia katika kipindi chote.

Katika mizani ya kiutu ya ugonjwa wa kawaida ni jambo jema sana ambapo familia inachukua nafasi yao kwa kiongozi wa umma aliyeugua kawaida, na kwa picha na sauti ile ya mgonjwa Mh Lissu, unaweza kukadiria kwamba sasa amepona kwa asilimia 51% hivi kutoka katika hali ya umahututi, kutoka mtu asiyejitambua amefikaje Nairobi mpaka mtu anayeweza kulihutubia taifa kwa shukrani.

Lakini katika mizani ya kiusalama, kwa tukio lile la mauaji ya risasi zaidi ya 30 yaliyofeli mchana kweupe, Lissu anawekwa hatarini zaidi kuliko alipokuwa mikononi mwa Chadema pale ICU. CHADEMA pekee ndio taasisi pekee yenye chombo cha intelijensia na ulinzi imara dhidi ya maisha ya Lissu kwa sasa na hata milele. Nje ya hapo mtakuja kukumbuka maneno haya niwaambiayo.

Kwanza niweke wazi, SIKUBALIANI KABISA na kauli ya Mh Mbowe kwamba chadema inaiachia familia iongoze mchakato huu wa matibabu awamu ya pili, Sikubaliani nalo kwa kuliangalia kiusalama zaidi. Na hili nikosa kubwa sana ambalo walioamua watakuja kujuta kesho.

Ninafikiri Familia ya Lissu, Chadema, Mh Alute Mgwai Lissu kaka wa Mh Lissu, Mama Alice Lissu mke wa Mh Lissu, Mh Mbowe, Mh Msigwa, Mh Lema, Mh Lowassa na TLS wakae watafakari upya, Uhai wa Lissu ni zaidi ya mapenzi yetu ya kisiasa, Uhai wa Lissu ni zaidi ya undugu wetu wa damu.

Jambo muhimu ambalo pande zote zinazomuuguza Lissu na watanzania kwa ujumla tunatakiwa kulielewa nikwamba, nadharia ya kiusalama inasema hivi, chuma kilichoingia kwa kugongwa na nyundo, kitatolewa kwa kugongwa na nyundo.

Hivyo kwa nadharia hiyo ya kiusalama nikuwa Lissu ameumia katika siasa, ni lazima apone katika siasa. Nje ya hapo mnammaliza kwa mikono yenu. Yeyote anayesema suala la Lissu lisiwe la kisiasa anaweza kuwa anamtakia mema Lissu, lakini asamehewe kwakuwa hajui atendalo.

Familia ya Lissu haina mifumo ya kiintelijensia kuzinusa na kuzikabili hatari zozote juu ya Lissu, bali ina moyo wa upendo na utu tu kwa ndugu yao, Lakini Lissu sio mali ya Ndugu zake, wala sio mali ya Chadema, wala sio mali ya TLS, Lissu ni mali ya Watanzania. Kwa picha na sauti zile, watanzania 90% wanaamini Lissu ameshapona, hivyo leo wakija kusikia kinyume kwa lolote hawataelewa la mwadhini wala la msoma sala.

Waliotaka kumua Lissu sio wajinga hata kidogo, ni professional, na kwa nadharia tu ya tukio na mwenendo wake, sio mtu mmoja au wawili waliopanga na kutenda haya, hivyo ili kuyakabili mambo haya yanahitajika taaluma ya hali ya juu na zaidi inahitajika busara na uvumilivu wa hali ya juu.

Nadharia inasema wazi, kadiri mlengwa wa mauaji anavyozidi kupona baada ya jaribio la mauaji kufeli, ndivyo anavyozidi kuwa hatari zaidi kwa wahalifu, waati huo ndio anazidi kuwa kwenye hali ya hatari zaidi. Njia salama kwa waauaji ni kumzima Lissu.

Bahati mbaya zaidi Lissu aliwaona kwa macho yake ya nyama, hivyo njia ni mbili tu katika kesi hii, ama Lissu afe, ama waliotumwa kumuua wauawe wao. Hakunaga njia ya mkato katika haya.

Rejea mauaji ya mtaalamu wa nyukilia wa Syria Jenerali Mohammed Suleiman yaliyotekelezwa na Kikosi cha Kidon cha Israel, ilikuwa ni baada ya majaribio kadhaa yaliyopelekea kutibiwa mahututi na kupona mithiri hii ya Lissu, kosa dogo tu lilitosha kupenyeza muuaji. Mifano hii itupe funzo katika kuulinda uhai wa Lissu, na sio vinginevyo.

Mimi kutoka moyoni mwangu, kwa jicho la kiusalama, sasahivi si wakati wa familia ya Lissu kuachiwa iongoze mchakato huu, Chadema pekee ndio yenye vitendea kazi na mbinu bora za kukabili hatari yoyote dhidi ya Lissu, tayari Chadema inaongoza mchakato huu, sio busara kubadili mfumo katikatika ya mwendo. Sijaona sababu za msingi kuzidi nyendo za kiusalama wa Lissu sasa mpaka kufikia Chadema iseme sasa famili ya Lissu ishike hatamu.

Watanzani wenye Lissu wao, wanaiangalia Chadema, Chadema ndio itakayojibu mbele ya umma kwa lolote, Haina sababu kukwepa au kupokezana katika jambo hili ambalo kwa hakika hali ya usalama ni muhimu kuliko jambo lolote,

Hakuna wa kumuamini nje ya nyinyi mliokuwa mnamtibu Lissi tangu awali, yeyote anayeingia sasa kwenye aweza kuwa hatari kuliko mfikiriavyo, si ndugu, si rafiki, si mpendwa. Kiusalama ni kwamba walioingia ndio watakaomaliza kumtibu. Hakuna Sababu, sioni sababu, zakupokezana majukumu katika nadharia ya tukio kama hili la Lissu, Je Chadema imechoka kumtibu mpaka mwisho? Je familia inahamu ya kumtibu kimila zaidi nje ya hospital? Jibu ni HAPANA KUBWA.

CHADEMA, Familia na TLS msiruhusu mwanya huu ambao muovu atautumia kummaliza Lissu hukohuko Rehabilitation, Acheni kabisa jaribio hilo, nawaambieni, jicho la kiusalama limeiona hatari iliyopo...tena kubwa... Chadema tulieni mmalize kazi ya Lissu, na kuanzia leo mpaka milele alindwe kwa nguvu zote kama alindwavyo Mh Lowassa, Mh Sumaye, na ikiwezekana alindwe sawa na alindwavyo rais wa nchi.

Naiona hatari iliyombele ya Lissu aliyepona kwa 50%, ninaona giza nene... Fungeni na kuomba zaidi Lissu wetu apone haraka....

Na Yericko Nyerere
Yericko uiswe na wasiwasi, hata Lissu hakuwahi kuwa na wasiwasi sio kwa akili yake wala kwa Mungu wake.Lissu aliwahi sema HAYA MAJAMAA YAKITAKA KUKUUA YANA KILA MBINU NA UWEZO WA KUKUA ,ILA NI KUMWACHIA TUU MUNGU.NA MUNGU AKASIMAMA KTK HILI. Chadema wana Intelligentia nzuri ,ila sio mara zote ni rahisi kuzuia majaribio.Na majaribio mengine yanaweza kuwa na level ya juu ya success km haya ya Lissu au Saanane. Ila ukweli unabaki kuwa,kila jaribio lifanywalo na waovu.Kuna njia ya kuwapanish kwa kuwapa options ngumu. na chadema huwa hawaachi options rahisi km adui anavyodhani. nadhani unakumbuka poll out ya Mbowe ktk ukuta.Ni km kiama cha viongozi wa dini wanaotumika kurudi tena majukwaani kujenga nadharia ya kuumiza watz na upinza. Sasa hivi kiongozi akirudi ataulizwa upo wapi mrejesho wa ukuta kwanza? Si mlisema mna mmudu na ni msikivu?Tuliacha ukuta,sasa majibu yap wapi?
 
Asante kwa kuweka msisitizo juu ya hili. Naamini Chadema na uongozi kwa ujumla wapo makini na walishawaza kabla kuhusu ni namna gani wataendelea ku handle na ku monitor usalama juu ya mpendwa wetu mpaka hatua ya mwisho ya utengamafu wa comrade Lissu.

Tuzidi kumuombea kaka yetu, tunamhitaji sana katika mapambano kuliko wakati wowote.
 
Ha ha ha, naona unaanza kupanick. Mgonjwa anaendeleaje leo na hao malaika weupe?
Unajichekesha km wale wamama wa kiswahili,wakiona wanaume ndio wanatoka kufua nje na kanga moja. Kwao mipasho ni zaidi ya maisha. Naona sasa umeahmia kujibaraguza tuu. Umeshindwa jibu umeona wapi huo weupe wa Yerricko umeamua kugeuza kuwa mipasho bila kuogopa hata kuwa unachoongea km una conpromise .
 
lissu awekewe ulinzi. kwangu toka mwanzo naamini chadema walifanya uzembe...
Wa nini?Unaweza kuwa na ulinzi dhidi ya dola uliyopo ktk nchi yako?Ulinzi wa Lissue unatakiw akuwa passive.Otherwise wale wasiojulikana na mamluki yao. Bila kuwa makini unaweza shambuliwa ,na hawa jamaa ,huku mchana walikuambia, wewe ndie ulikuwa mlinzi kwa hiyo wewe ndie utakuwa umehusika.
 
Unajichekesha km wale wamama wa kiswahili,wakiona wanaume ndio wanatoka kufua nje na kanga moja. Kwao mipasho ni zaidi ya maisha. Naona sasa umeahmia kujibaraguza tuu. Umeshindwa jibu umeona wapi huo weupe wa Yerricko umeamua kugeuza kuwa mipasho bila kuogopa hata kuwa unachoongea km una conpromise .
Mzeee wa malaika weupe, duh.
 
Yeriko, Mbowe alisema watakuwa nyuma ya familia ya Lissu. Hakusema watamwacha. Haya yote unayoyasema wameyatafakari na ndiyo maana hata sasa hujui ataenda nchi gani na lini?
 
Tulia usome tema kwa umakini, tahadhari yangu ipo sehemu gani?
 
Ndugu wameamua kumchukua mgonjwa wao baada ya kuona chadema wanafanya Tundu kama Trophy,wanamtumia kisiasa huku akizidi kuteketea michango wanatafuna,kazi kwenda kupiga picha tu na kurusha mitandaoni.
Kwa sasa matibabu yatafadhiliwa na serikali,kwa aibu chadema wakasema wanajiweka pembeni kwa sababu waliongea mbovu sana siku za kwanza za maafa.
Hapo ndipo penye shida. Hawa jamaa hawana utu hata kidogo , wamemtumia Lissu kujipatia manufaa ya kiuchumi lakini leo wanaamua kumtelekeza.
 
Kamanda nimekuelewa zaid ya sana!! Kama kuna mtu hajakuelewa arudie kusoma atapata kitu. Akiwa anafanya hivyo akumbuje movies kadhaa zenye kufanana na hili!

Lakn kuna sehem huenda tumetofautiana kumwelewa mbowe. Binafs nilimsikia akisema tuko katika hatua ya pili ya kumpeleka sehem nyingine na hiyo sehem hatuitaji kwa usalama zaid. Hii kauli imebeba hoja kwamba bado wao ndio watawajibika kwa usalama wake. Kingine ni kitendo cha kuomba tuendelee kumchangia huku akisema hatuko tuyari kukaa meza moja na watesi wetu ili tu watupe hela za kumtibu ndugu yetu bila kuhakikishiwa usarama wetu. So naona bado chadema kama taasisi bado wako na Lissu mpaka mwisho.

Umenipata yeriko!!

Nimefikiria hivyo pia walicjokicha lea familia ni kumsemea Lissu n.a. kwa vile Lissu anauwezo wa kuongea ataweza kuongea hata mwenyewe ndiyo sababu hajataja wapi ataelekea lea phase 2.Familia yake siyo wajinga pia wasijue havina ya ndugu yao hasa mkewe.
 
Tatizo sio chadema, Tatizo lipo kwenye familia ya lisu, Familia wanataka kushirikiana na serikali kugharamia matibabu ya lisu, Chadema ILIKATAA kuandika barua kuomba pesa za matibabu,kumbuka mlipa zumari ndiye huchagua wimbo!! Serikali ikigharamia matibabu maana Yake watu WOTE wa serikali wataweza kumuona lisu kadri watakavyo. Sasa miongoni mwao Waziri na wabaya wa lisu watakuwemo ambao wanaweza hata kumpulizia Sumu ya kufa pole pole na CDM hawatakuwa na nguvu ya kuwasachi au kuamua Nani aingie kumuona mgonjwa na Nani asiingie,!! Ndiyo maana chadema imejitoa kuongoza ili iwaachie familia Yake washirikiane na serikali kama wanavyotaka wao ili kesho na kesho kutwa familia ndo watatupa majibu. Familia inasema ndugu YAO anatumika kisiasa, !
 
_____________________________________

Tangu juzi baada ya hotuba ya Mh Mbowe, mimi nilijawa na furaha, furaha yangu ilikuwa katika mambo mengi, lakini kubwa zaidi ilikuwa nikusikia kuwa Lissu wetu amepata ahueni na sasa anakula, anaongea anakaa na anapunga mkono.

Hii ni furaha yangu kuu, furaha ilizidi zaidi jana majira ya alasiri ambapo picha ya kwanza ya mpendwa wetu iliwekwa hadharani, pude si punde sauti yake halisi ikasikika ulimwenguni kote ikinena kwa shukrani toka vilindi na vilima vya moyo wake mkuu kuja kwetu wana wa dunia.

Naaam, katikakati ya furaha hii nilizama katika tafakuri kubwa, hasa nikiwaona Watanzania walivyojawa na furaha isiyo kifani. Tafakuri yangu ilijikita kuichambua hotuba ya Mh Mbowe neno kwa neno na huku nikiangazia hali ya usalama wa Lissu sasa na huko mbele mpaka hitaji la Mungu litimie.

Katika Hotuba yake Mh Mbowe alisema, Chadema sasa inaiachia familia ya Mh Lissu iongoze shughuli katika kipindi hiki cha matibabu awamu ya pili (rehabilitations), akasisitiza kuwa Chadema haitakuwa mbali itaendelea kuwa bega kwa bega na familia katika kipindi chote.

Katika mizani ya kiutu ya ugonjwa wa kawaida ni jambo jema sana ambapo familia inachukua nafasi yao kwa kiongozi wa umma aliyeugua kawaida, na kwa picha na sauti ile ya mgonjwa Mh Lissu, unaweza kukadiria kwamba sasa amepona kwa asilimia 51% hivi kutoka katika hali ya umahututi, kutoka mtu asiyejitambua amefikaje Nairobi mpaka mtu anayeweza kulihutubia taifa kwa shukrani.

Lakini katika mizani ya kiusalama, kwa tukio lile la mauaji ya risasi zaidi ya 30 yaliyofeli mchana kweupe, Lissu anawekwa hatarini zaidi kuliko alipokuwa mikononi mwa Chadema pale ICU. CHADEMA pekee ndio taasisi pekee yenye chombo cha intelijensia na ulinzi imara dhidi ya maisha ya Lissu kwa sasa na hata milele. Nje ya hapo mtakuja kukumbuka maneno haya niwaambiayo.

Kwanza niweke wazi, SIKUBALIANI KABISA na kauli ya Mh Mbowe kwamba chadema inaiachia familia iongoze mchakato huu wa matibabu awamu ya pili, Sikubaliani nalo kwa kuliangalia kiusalama zaidi. Na hili nikosa kubwa sana ambalo walioamua watakuja kujuta kesho.

Ninafikiri Familia ya Lissu, Chadema, Mh Alute Mgwai Lissu kaka wa Mh Lissu, Mama Alice Lissu mke wa Mh Lissu, Mh Mbowe, Mh Msigwa, Mh Lema, Mh Lowassa na TLS wakae watafakari upya, Uhai wa Lissu ni zaidi ya mapenzi yetu ya kisiasa, Uhai wa Lissu ni zaidi ya undugu wetu wa damu.

Jambo muhimu ambalo pande zote zinazomuuguza Lissu na watanzania kwa ujumla tunatakiwa kulielewa nikwamba, nadharia ya kiusalama inasema hivi, chuma kilichoingia kwa kugongwa na nyundo, kitatolewa kwa kugongwa na nyundo.

Hivyo kwa nadharia hiyo ya kiusalama nikuwa Lissu ameumia katika siasa, ni lazima apone katika siasa. Nje ya hapo mnammaliza kwa mikono yenu. Yeyote anayesema suala la Lissu lisiwe la kisiasa anaweza kuwa anamtakia mema Lissu, lakini asamehewe kwakuwa hajui atendalo.

Familia ya Lissu haina mifumo ya kiintelijensia kuzinusa na kuzikabili hatari zozote juu ya Lissu, bali ina moyo wa upendo na utu tu kwa ndugu yao, Lakini Lissu sio mali ya Ndugu zake, wala sio mali ya Chadema, wala sio mali ya TLS, Lissu ni mali ya Watanzania. Kwa picha na sauti zile, watanzania 90% wanaamini Lissu ameshapona, hivyo leo wakija kusikia kinyume kwa lolote hawataelewa la mwadhini wala la msoma sala.

Waliotaka kumua Lissu sio wajinga hata kidogo, ni professional, na kwa nadharia tu ya tukio na mwenendo wake, sio mtu mmoja au wawili waliopanga na kutenda haya, hivyo ili kuyakabili mambo haya yanahitajika taaluma ya hali ya juu na zaidi inahitajika busara na uvumilivu wa hali ya juu.

Nadharia inasema wazi, kadiri mlengwa wa mauaji anavyozidi kupona baada ya jaribio la mauaji kufeli, ndivyo anavyozidi kuwa hatari zaidi kwa wahalifu, waati huo ndio anazidi kuwa kwenye hali ya hatari zaidi. Njia salama kwa waauaji ni kumzima Lissu.

Bahati mbaya zaidi Lissu aliwaona kwa macho yake ya nyama, hivyo njia ni mbili tu katika kesi hii, ama Lissu afe, ama waliotumwa kumuua wauawe wao. Hakunaga njia ya mkato katika haya.

Rejea mauaji ya mtaalamu wa nyukilia wa Syria Jenerali Mohammed Suleiman yaliyotekelezwa na Kikosi cha Kidon cha Israel, ilikuwa ni baada ya majaribio kadhaa yaliyopelekea kutibiwa mahututi na kupona mithiri hii ya Lissu, kosa dogo tu lilitosha kupenyeza muuaji. Mifano hii itupe funzo katika kuulinda uhai wa Lissu, na sio vinginevyo.

Mimi kutoka moyoni mwangu, kwa jicho la kiusalama, sasahivi si wakati wa familia ya Lissu kuachiwa iongoze mchakato huu, Chadema pekee ndio yenye vitendea kazi na mbinu bora za kukabili hatari yoyote dhidi ya Lissu, tayari Chadema inaongoza mchakato huu, sio busara kubadili mfumo katikatika ya mwendo. Sijaona sababu za msingi kuzidi nyendo za kiusalama wa Lissu sasa mpaka kufikia Chadema iseme sasa famili ya Lissu ishike hatamu.

Watanzani wenye Lissu wao, wanaiangalia Chadema, Chadema ndio itakayojibu mbele ya umma kwa lolote, Haina sababu kukwepa au kupokezana katika jambo hili ambalo kwa hakika hali ya usalama ni muhimu kuliko jambo lolote,

Hakuna wa kumuamini nje ya nyinyi mliokuwa mnamtibu Lissi tangu awali, yeyote anayeingia sasa kwenye aweza kuwa hatari kuliko mfikiriavyo, si ndugu, si rafiki, si mpendwa. Kiusalama ni kwamba walioingia ndio watakaomaliza kumtibu. Hakuna Sababu, sioni sababu, zakupokezana majukumu katika nadharia ya tukio kama hili la Lissu, Je Chadema imechoka kumtibu mpaka mwisho? Je familia inahamu ya kumtibu kimila zaidi nje ya hospital? Jibu ni HAPANA KUBWA.

CHADEMA, Familia na TLS msiruhusu mwanya huu ambao muovu atautumia kummaliza Lissu hukohuko Rehabilitation, Acheni kabisa jaribio hilo, nawaambieni, jicho la kiusalama limeiona hatari iliyopo...tena kubwa... Chadema tulieni mmalize kazi ya Lissu, na kuanzia leo mpaka milele alindwe kwa nguvu zote kama alindwavyo Mh Lowassa, Mh Sumaye, na ikiwezekana alindwe sawa na alindwavyo rais wa nchi.

Naiona hatari iliyombele ya Lissu aliyepona kwa 50%, ninaona giza nene... Fungeni na kuomba zaidi Lissu wetu apone haraka....

Na Yericko Nyerere
Three parts as you mentioned in your thread, should come together in the discussion about the so called LISSU'S SECURITY ....

Among those three parts is CHADEMA and you mentioned some of CHADEMA leaders such as Hon. A. Mbowe, Hon. P. Msigwa, Hon. G. Lema and Hon. E. Lowassa ......

Wote ulowataja ni VIONGOZI ndani ya chama, HAPANA SHAKA KATIKA HILO ..... na wanaweza shiriki katika vikao vya MAJADILIANO juu mstakabali wa USALAMA WA MH. T. LISSU kama ulivyoshauri .....

SWALI:

Je viongozi WATATU WA MWISHO katika mtiririko hapo juu wanayo NGUVU SANA YA USHAWISHI PIA MAMLAKA NDANI YA CHAMA zaidi ya Mh. Mashinji (katibu mkuu) na Manaibu wake wawili Mh. Mnyika (bara) na Mh. Mwalimu (visiwani) bila kumsahau Mh. Baregu (makamu m/kiti na mshauri wa chama)? .....

Je huoni kuwa licha ya NIA NJEMA ulonayo juu ya Mh. T. Lissu kuhusu USALAMA wake waweza sababisha TAFAKURI pia MASWALI FIKIRISHI juu ya SUGGESTION YAKO YA HAYO MAJINA?

WHY ONLY THOSE FELLAS?

NI MTAZAMO WANGU TU .... I ALSO STAND TO BE CORRECTED .....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom