CHADEMA endeleeni kuelimisha kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya

Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,273
2,000
Kwanza hongera kwa kuleta wazo hilo lakuomba uwepo wa uhamasishaji na elimu kwa wananchi kuchangia kupata katiba mpya ikiwa serikali itasingizia uviko umeshusha uchumi.

Ni wazo zuri na la kizalendo kwa kinga ya vizazi vijavyo. Ushauri wangu muondokane na agenda yakujinga kwa uchaguzi 2025.

Agenda kuu iwe kujenga chama nakutoa elimu ya umuhimu wa katiba mpya. Katiba mpya itakuwa pia jibu la tume huru.

Achaneni pia na UVIKO 19. Hukumu yao ipo huku uraiani. Fanyeni kila mbinu MIDAHALO IANZE ya elimu kwa taifa, nguvu yakutunisha misuli kwenye kampeni za uchaguzi itumike kutoa elimu ya katiba.

Wananchi tunachangia tunu Mwenge.

Vivyo hivyo tunu katiba tutachagia.

Hamasisheni kidigitali TUTAFIKA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom