CHADEMA eleweni, Tume huru ya uchaguzi sio kigezo cha kupata kiongozi

Mbaga Jr

JF-Expert Member
May 28, 2018
18,993
41,361
Chadema walikuwa vinara kuiponda tume ya uchaguzi ya Tanzania huku wakiisifia ya Kenya, ni kweli tume ya kenya imetupita mbali sana lakini tume huru sio kigezo cha kupata kiongozi.

Tume hiyo hiyo huru ya Kenya mliyokuwa mnaisifia wao kwa wao ndio waliopishana kuhusu mshindi wakati huo huo matokeo yanajulikana na kila Mkenya kuwa mshindi ni Ruto na sio Odinga.

Haiwezekani tume huru wao kwa wao wawe na makundi ndani yao wenyewe, kuna waliokuwa wanamuunga mkono Ruto aliyeshinda kwa haki na wengine walitaka Odinga atangazwe wakati wanajua kabisa hakushinda.

Haiwezekani makamu mwenyekiti apinge matokeo wakati huo huo mwenyekiti anataka kutoa matokeo ya uchaguzi.

Unaweza ukawa na tume huru lakini sio ya watu sahihi.
 
Nachelea kutoa neno linaweza kuwa tusi, lakini kiujumla wewe ni Zuzu.
 
Huoni uhuru wa tume ya uchaguzi ya Kenya ndio ulioleta haki kwa mshindi halali kutangazwa?
Wale wafia chama au mgombea fulani walitia mpira kwapani na kulala mbele kuukwepa ukweli hata hivyo Chebukati hajawaangunisha wananchi.

Tanzania hatuna shida na CCM kushindwa ila wizi na uporaji wa chaguzi ndio maana wanademokrasia wanataka uwazi na uhuru wa tume husika ili kuondoa mambo kama ya akina Jecha na wenzake.
 
Tume huru ni hatua kaka. Sio suala la CDM tu kama unavyotaka kutuaminisha na kutubinafsishia hapa. Ni suala la Kikatiba. Na katika hili Kenya wameshatupita kwa mbali sana. Walianza na Katiba, Tume huru ikafuatia na hatimae ni Katiba hiyo hiyo inaweza "kuiadhibu" tume huru kupitia Mahakama.

Chukua hatua.
 
Chadema walikuwa vinara kuiponda tume ya uchaguzi ya Tanzania huku wakiisifia ya Kenya, ni kweli tume ya kenya imetupita mbali sana lakini tume huru sio kigezo cha kupata kiongozi.

Tume hiyo hiyo huru ya Kenya mliyokuwa mnaisifia wao kwa wao ndio waliopishana kuhusu mshindi wakati huo huo matokeo yanajulikana na kila Mkenya kuwa mshindi ni Ruto na sio Odinga.

Haiwezekani tume huru wao kwa wao wawe na makundi ndani yao wenyewe, kuna waliokuwa wanamuunga mkono Ruto aliyeshinda kwa haki na wengine walitaka Odinga atangazwe wakati wanajua kabisa hakushinda.

Haiwezekani makamu mwenyekiti apinge matokeo wakati huo huo mwenyekiti anataka kutoa matokeo ya uchaguzi.

Unaweza ukawa na tume huru lakini sio ya watu sahihi.

..mtoa mada unakubali kwamba tume ya kenya imetupita mbali sana ukiilinganisha na tume ya tanzania.

..katika mazingira hayo kwanini unaona chadema wamekosea kupongeza?

..pia kama unakiri tume ya kenya ni nzuri kwanini unapinga tusiige mazuri yake?

..tuige mambo mazuri ya tume ya kenya, yale mabaya tuachane nayo.
 
Hakuna kiongozi wa upinzani Tanzania mwenye akili kama Kenya. Hakuna nani Heche, Mnyka who. Wote ni wizi wa ruzuku na uzinzi. Hakuna kujenga Taifa mle. Povu ruxa.
 
Kwahiyo bora tume isiwe huru ili impitishe anayetakiwa na wajumbe wa tume?
Kilichonifurahisha Kenya ni kuwa na Tume iliyo huru na Uhuru ule kuonekana wazi. Yaani Mawakala walishuhudia Kura zikihesabiwa, Wagombea, Waangalizi wa Kimataifa na bila kuwasahau Waandishi wa Habari (walio huru na Sio kama kina Mayalla).
 
Chadema walikuwa vinara kuiponda tume ya uchaguzi ya Tanzania huku wakiisifia ya Kenya, ni kweli tume ya kenya imetupita mbali sana lakini tume huru sio kigezo cha kupata kiongozi.

Tume hiyo hiyo huru ya Kenya mliyokuwa mnaisifia wao kwa wao ndio waliopishana kuhusu mshindi wakati huo huo matokeo yanajulikana na kila Mkenya kuwa mshindi ni Ruto na sio Odinga.

Haiwezekani tume huru wao kwa wao wawe na makundi ndani yao wenyewe, kuna waliokuwa wanamuunga mkono Ruto aliyeshinda kwa haki na wengine walitaka Odinga atangazwe wakati wanajua kabisa hakushinda.

Haiwezekani makamu mwenyekiti apinge matokeo wakati huo huo mwenyekiti anataka kutoa matokeo ya uchaguzi.

Unaweza ukawa na tume huru lakini sio ya watu sahihi.
CCM mmeanza kulia kulia sasa na hiyo ndio maana ya demokrasia, ingekuwa tanzania tayari wapinzani wangeshakamatwa
 
Hujui kitu kilichosumbua Kenya. Kilichosumbua Ni ukabila tu
Chadema walikuwa vinara kuiponda tume ya uchaguzi ya Tanzania huku wakiisifia ya Kenya, ni kweli tume ya kenya imetupita mbali sana lakini tume huru sio kigezo cha kupata kiongozi.

Tume hiyo hiyo huru ya Kenya mliyokuwa mnaisifia wao kwa wao ndio waliopishana kuhusu mshindi wakati huo huo matokeo yanajulikana na kila Mkenya kuwa mshindi ni Ruto na sio Odinga.

Haiwezekani tume huru wao kwa wao wawe na makundi ndani yao wenyewe, kuna waliokuwa wanamuunga mkono Ruto aliyeshinda kwa haki na wengine walitaka Odinga atangazwe wakati wanajua kabisa hakushinda.

Haiwezekani makamu mwenyekiti apinge matokeo wakati huo huo mwenyekiti anataka kutoa matokeo ya uchaguzi.

Unaweza ukawa na tume huru lakini sio ya watu sahihi.
 
Kwahiyo bora tume isiwe huru ili impitishe anayetakiwa na wajumbe wa tume?
Unajua kwanini Tundu Lissu akiongelea elimu ya uraia huwa anaongea kwa ukali? Kwasababu anajiuliza inakuwaje common sense haiko common kwa baadhi ya watu!
 
Huoni uhuru wa tume ya uchaguzi ya Kenya ndio ulioleta haki kwa mshindi halali kutangazwa?
Wale wafia chama au mgombea fulani walitia mpira kwapani na kulala mbele kuukwepa ukweli hata hivyo Chebukati hajawaangunisha wananchi.

Tanzania hatuna shida na CCM kushindwa ila wizi na uporaji wa chaguzi ndio maana wanademokrasia wanataka uwazi na uhuru wa tume husika ili kuondoa mambo kama ya akina Jecha na wenzake.

Ruto hakuwa mshindi halali
 
Unaweza ukawa na tume huru lakini sio ya watu sahihi.

Ni kweli, lakini ujue pia kwamba hakuna uwezekano wa kuwa na watu sahihi ndani ya tume isiyokuwa huru. Tume isiyokuwa huru inakuwa na watu wenye agenda moja tu: kulinda maslahi ya walio madarakani.

Wewe umewahi kusikia NEC yetu imegawanyika hata mara moja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom