Chadema ebu jitafakarini hapa halafu ndo muendelee na harakati zenu za M4C | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema ebu jitafakarini hapa halafu ndo muendelee na harakati zenu za M4C

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zema21, Aug 29, 2012.

 1. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Binafsi huwa nashangazwa saana vitendo vinavyofanywa na serikali ya CCM kwa kutumia jeshi la polisi. Huwa mara nyingi wamekuwa wakizuia maandamano ya vyama vya upinzani kwa madai ya kuwa wamepata taarifa za kiitelijensia kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani.

  Awali nilifikiria kuwa ni kweli kwamba vana dhamira safi ya kuwalinda wananchi wake lakini kumbe laa! Hao hao endapo chama kitakaidi huwa wanaenda eneo la tukio na kuanzisha vurugu kubwa ambayo inaleta uvunjifu wa amani na matukio ya mauaji.. sote tumeshudia matukio kadhaa likiwemo la arusha, ambapo polisi waliosema kuwa wanawakataza chadema ili kuzuia uvunjifu wa amani walienda wakaleta vurugu kubwaa, kujeruhi wananchi pamoja na mauaji ya wasiokuwa na hatia…

  Tukio la juzi morogoro la polisi kuleta vurugu, kujeruhi na kuua ni kitu cha kushangaza sana! Badala yake baada ya polisi kuzidiwa nguvu, chadema waliandamana kwa amani, wakafika uwanjani, wakafanya mkutano na kumaliza kwa amani bila vurugu!!!

  Kuna wakati polisi huzuia mikutano kwa kisingizio kuwa hawana polisi wakutosha kuwalinda chadema katika mkutano wao lakini ikitokea chadema wakasema wanaandama basi polisi na vifaa vingi utadhani wako vitani hutembea mitaani kwa ajili ya kuwadhibiti chadema, ebu jiulize hawa polisi huwa wanapatikana wapi? Iweje chadema wanambiwa kuwa hakuna askari wa kutosha kuwalinda katika maandamano yao hivyo wasiandamane lakini wakikaidi na kuandamana huwa askari lukuki hujazwa mitaani ili kuja kuwadhibiti? Huwa wanatoka wapi hawa?

  Kwanini zile risasi za moto huwa hazielekezwi kwa akina dr slaa, au lisu au myika au mbowe bali ni kwa raia wa chini wasiokuwa hata na magwanda?

  Tujiulize
   
 2. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  Mkuu wangu police huwa wanatii amri toka juu sasa tuwaulize hao akina mwema ndio watujibu
   
 3. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wawa pige makamanda wakuu tena unadhani nchi itatawalika tena? Wanajua wakifanya ivo ndio mwisho wao na badala yake huua raia ili raia wengine waogope kushiriki Siku nyingine bila kujua kufanya ivo ndio kuwaongezea hari na chuki juu Yao. Ulishaona wapi nwizi katoka jela na kuacha wizi kwa kuhofia jela??? Wanadhani wanatutishia kumbe hawajui ndio wanatukomaza iko Siku watakimbia kivuli chao wenyewe sema ni sisi wenyewe ndio tumezoea kumalizia hasira kwenye keyboard badala ya action
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Matumizi ya silaha za moto dhidi ya raia ni kitu bado ninakifikiria na kukifanyia itafiti, kama kuna mtu anafahamu neno moja "vocabrary" inayobeba maana nzima ya kitendo hiki anisaidie.
   
 5. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Taarifa kamili za matukio ya mauaji kama haya zinapaswa kutunzwa ili wakati ukifika makamanda na wanasiasa wanaotoa hizo amri wawajibike kisheria, ikiwezekana mpka ICC - The Hague. Chadema mmeisha fikiria hii option ya kuyafanya haya mauaji kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu na ualifu dhidi ya ubinadamu? Wanaharakati mko wapi? Mbona hamsikiki mnapohitajika?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ninavyoona jeshi la polisi wameichoka ccm. Kwa kwua polisi wanajua kuwa hawana uwezo wa kusema wazi wazi, wameamua kuihujumu ccmna serikali yake ili ishindwe
   
 7. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  CCM wako dhoofu li hali, ni taasisi yao moja tu ya Polisi ndio inayojaribu kupambana na umma, wananchi wamekwisha ikataa Tanganyika nzima. Hawajui wafanye nini wamebaki wamechanganyikiwa. JK alipanda mbegu mbaya ya udini, ushkaji, kutowajibika, wizi anavuna. Nakubaliana na wazo la kutunza hizo kumbukumbu ili wafuatao tuwapeleke ICC kuanzia 2016. nao ni Jakaya Kikwete, Saidi Mwema, Nape Nnauye, Wilson Mukama, nk mikono yao imejaa damu za Watanganyika na jhawataponyoka mkono wa sheria, wajiandae tu
   
 8. K

  Kiwera Mikaeli Senior Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yamkini u sahihi.....:eek2:
   
 9. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  polisi + usalama wa taifa = c.c.m
   
Loading...