CHADEMA Dodoma mjini watoa salamu za pole kufuatia vifo vya wanafunzi, walimu na dereva

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,182
1,490
Create Date: 5/7/2017 21:06

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA)WILAYA YA DODOMA MJINI



Tumepokea kwa mshituko na masikitiko Makubwa sana taarifa za msiba uliotokana kwa Ajali iliyosababisha vifo vya watoto wetu, wadogo zetu(wanafunzi zaidi ya 30), Dereva na walimu,iliyotokea Karatu mkoani Arusha tarehe 06/May.2017.

Dodoma Mjini na Dodoma kwa ujumla tunaungana kwa pamoja na Familia za Wahanga wa Ajali hiyo na Watanzania wote kwa ujumla kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awarehemu na azilaze roho za marehemu Mahali pema peponi, Amen

Rambirambi zetu kwa Familia za Wahanga, Viongozi wa Chama Mkoa wa Arusha viongozi wa serikali Mkoa wa Arusha, viongozi wa Dini Mkoa wa Arusha,ndugu, jamaa, Marafiki na Watanzania wote,Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hichi Kigumu cha Majonzi.tumhimidi yeye na kumtukuza kwakuwa yeye ni Alpha na Omega.


Bwana Ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.

Imetolewa na
Mathias Raymond Nyakapala
Katibu Wa Wilaya Dodoma Mjini
 
Back
Top Bottom