CHADEMA, CUF wahoji usafi wa Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, CUF wahoji usafi wa Rais Kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Limbani, Apr 26, 2011.

 1. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  • Wamtaka atangaze mali zake, wadai naye ni fisadi

  na Irene Mark na Bakari Kimwanga


  [​IMG] KAULI mbiu ya ‘kujivua gamba’ ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kuwa mwiba mchungu kwa chama hicho baada ya wananchi kuhoji nguvu ya kimaadili ya Rais Jakaya Kikwete ambaye anadai kutaka kuondoa mafisadi ndani ya chama huku naye akihusishwa na ufisadi mwingine.
  Baadhi ya viongozi na makada wa CCM na vyama vya upinzani wamedai jitihada za Rais Kikwete kushambulia na kuadhiri wanasiasa wenzake kwa kumtumia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, ni za kinafiki, kwani naye (Kikwete) yu miongoni mwa mafisadi.
  Jana ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, na Diwani mstaafu wa Tarime (CHADEMA) John Heche, ambao kwa nyakati tofauti walisema CCM haisafishiki.
  Walisema ili kuisafisha CCM na serikali yake, ingepaswa kuwaondoa wote waliotajwa kwenye ufisadi akiwemo Rais Kikwete.
  Profesa Lipumba aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CUF.
  Mbali na ufisadi wa Kikwete uliotajwa na Dk. Willibrod Slaa Septemba 2007, jana Profesa Lipumba aliongeza mali za Kikwete.
  Alisema Rais Kikwete aligoma kutangaza mali zake alipoingia madarakani na hata sasa hataki kufanya hivyo kwa sababu kuna harufu ya ufisadi katika mali hizo.
  Profesa Lipumba alidai kuwa Rais Kikwete, kama angekuwa mtu safi angetangaza mali zake kabla hajaingia Ikulu kama alivyofanya mtangulizi wake, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ili wananchi wapime uadilifu wake.
  “Kama kweli Rais Kikwete ana nia ya kupambana na ufisadi atangaze mali zake na wale wote wanaotuhumiwa wafunguliwe mashtaka na wafikishwe mahakamani.
  “Najua katika hili, Rais Kikwete hawezi, kwani anahofia wale waliopewa siku 90 watatoa siri kubwa pamoja na kuwataja vigogo walionufaika na ufisadi wao. Hiki ni kipimo kuwa CCM haina uwezo wa kupambana na ufisadi ila inachofanya ni usanii dhidi ya ufisadi,” alisema Profesa Lipumba.
  Hata hivyo alisema kamwe CCM haiwezi kuwachukulia hatua watuhumiwa hao wa ufisadi kwa kile alichodai kuwa tuhuma hizo zinawagusa vigogo wengi wa CCM ambao kama walivyoshindwa kuchukua hatua dhidi ya kampuni ya Kagoda na mafisadi wa EPA, haiwezi kuwagusa hata hawa.
  Kuhusu ununuzi wa rada, alisema kama kweli serikali ina nia ya kupambana na ufisadi, itumie ushahidi ulioletwa na Ofisi ya Upelelezi wa Makosa Makubwa ya Uingereza (SFO) kuwafikisha mahakamani vigogo wote waliohusika na sakata la ununuzi wa rada kwani hadi sasa hakuna ofisa yeyote aliyekamatwa.
  Kuhusu mchakato wa kubinafsishwa kwa mashirika ya umma hasa kampuni ya sigara na kampuni ya simu, Lipumba alisema makampuni hayo yaliuzwa kwa bei ndogo kuliko thamani yake.
  Kutoka Mwanza, Heche aliweka wazi kwamba kauli zinazotolewa na Nape ni tambo na hadaa kwa wananchi kwa vile amekubali kuwa vuvuzela la mafisadi.
  Heche alisema hayo katika mkutano wake na vyombo vya habari, huku akitangaza nia yake ya kuwania uenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA).
  Alisema Nape anatoa kauli za kitoto za kudai kuwa Dk. Willbrod Slaa anatumiwa na mafisadi ili amshambulie Rais Kikwete na familia yake, kwa kuwa Dk. Slaa ndiye aliyewataja hao mafisadi, Kikwete akiwamo; na kwamba vita ya ufisadi ni ya CHADEMA si ya CCM.
  “Nape anadiriki kusema hayo kwa sababu badala ya kueneza itikadi za CCM anajigeuza vuvuzela la mafisadi. Ameamua kuwa mweneza propaganda badala ya itikadi. Hatuwezi kumsikiliza hata kidogo.
  “Ingawa kwa juujuu anajifanya kupambana na ufisadi, Nape hana uwezo wala uadilifu wa kukemea mafisadi kwa sababu hata Rais Kikwete anayemtetea ametajwa kwenye orodha ya mafisadi kule Mwembeyanga.
  “…Ningependa kumuuliza Nape katika orodha ya mafisadi 16 waliotajwa na Dk. Slaa, yeye anamtetea fisadi yupi? Anajua kwamba hata Rais Kikwete alitajwa? Ni lini Nape amepewa ajira ya kutetea udhaifu binafsi wa Rais na familia yake?” alihoji Heche kupitia taarifa hiyo.
  “Tumeushtukia mpango wa CCM kuidhoofisha hoja ya CHADEMA inayolenga kupambana na mafisadi wanaotafuna fedha za Watanzania na hatuko tayari kuukubali,” alieleza Heche.
  Alisema wote wanaotaka kuondoa ufisadi nchini lazima wautazame kwa marefu na mapana, wajue na wakubali kusema wazi kwamba Rais Kikwete mwenyewe ni zao la ufisadi. Pesa za EPA zilizoibwa Benki Kuu zilitumika kununua urais wake.
  “Tunaamini kwamba Watanzania walishagundua ukweli huu, ndiyo maana mwaka 2010 hawakumpa Rais Kikwete kura za kutosha kama mwaka 2005 wakati anaingia. Hivyo, wote wanaomtetea akiwemo Nape, wanatetea ufisadi. Wanahujumu Watanzania.
  “Enzi za CCM kuendelea kuongoza Watanzania zimekwisha. Hii ni zamu ya Watanzania wanaotafuta matumaini mapya kupitia CHADEMA,” alisisitiza Heche.
  Akizungumzia azima yake ya kusaka uongozi wa BAVICHA, Heche alisema: “Kwa kuwa mimi ni mwanachama makini wa CHADEMA na kwa kuwa nimewahi kuwa kiongozi sasa nawania uongozi tena, naona ni vema nitumie fursa hii kuzungumzia masuala kadhaa ninayoshuhudia yakisemwa au yakifanywa na chama tawala kinachokaribia kumaliza muda wake.”
  Aidha, aliwaomba vijana wote kuwa makini zaidi katika kuitengeneza Tanzania mpya kwa mustakabali wa vizazi vijavyo na kubainisha kwamba kazi ya BAVICHA ijayo chini ya uongozi wowote utakaochaguliwa ni kuwainua vijana katika kuwamulika mafisadi wote hata kama wapo madarakani.
  CHADEMA kinatarajiwa kufanya uchaguzi wa BAVICHA uliofutwa miaka miwili iliyopita baada ya uongozi wa chama kuridhika kwamba taratibu za uchaguzi zilikosewa.
  Heche anakuwa mwanachama wa kwanza kutangaza nia hiyo. Alitaja sababu tisa za kugombea uongozi BAVICHA. Alisema:
  “Kwanza mimi ni mwana CHADEMA kijana. Nafasi inayogombewa ni ya vijana. Hii ni fursa kwangu kuitumia vema haki yangu ya kugombea uongozi wa vijana ndani ya chama.
  “Dhamira yangu ni kuifanya BAVICHA kuwa taasisi imara, ambayo itakuwa tanuru la viongozi makini katika ngazi mbalimbali, kichama na kitaifa. BAVICHA ni chombo kipya. Uchaguzi huu ni sehemu ya mchakato wa kukianzisha, kukijenga na kukiimarisha, ili kiwe kimbilio la vijana wengi wa taifa hili wanaotaka mabadiliko.
  “Katika kuisuka BAVICHA kutoka ngazi ya kata hadi taifa, tutakuwa tumeunganisha nguvu za vijana wa Tanzania katika kudai uhuru wa kweli, usawa na haki.
  “Nataka kuendeleza jitihada za viongozi na makada wetu za kupigania ushiriki wa vijana katika siasa za Tanzania na uongozi.
  “Nataka kuijenga BAVICHA iwe daraja la kuwafikia, kuwainua na kuwajenga vijana wasomi walio vyuoni na waliohitimu waweze kushiriki siasa za ukombozi wa taifa lao.
  “Ningependa, kupitia BAVICHA, kusimika mapambano ya ukombozi ya aina yake Tanzania Visiwani, kwa kuanzisha kanda maalumu ya BAVICHA visiwani, kama moja ya mikakati ya chama ya kukikuza CHADEMA miongoni mwa vijana na jamii ya Zanzibar.
  “Nataka kuifanya BAVICHA kuwa chachu ya mafunzo kwa vijana juu ya falsafa na itikadi za chama katika ngazi za majimbo, wilaya na mikoa.
  “Nataka kuongoza taasisi itakayosaidiana na taasisi nyingine rasmi na zisizo rasmi katika kusimamia, kuwajibisha na kuihoji serikali kuhusu masuala muhimu yanayohusu maisha ya Watanzania.
  “Nataka kuongoza vijana, kupitia BAVICHA, kuendelea kudai serikali ianzishe Baraza la Vijana la Taifa.”  Source: Tanzania Daima
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kujua ukwasi wake usiounganika vema katika historia, nenda ukatafute kujua salio kwenye misururu ya mi-akaunti za Rz1.
   
 3. F

  Fareed JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA na CUF wanatumiwa na Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge kuibua tuhuma za kupikwa za ufisadi dhidi ya Kikwete na viongozi wengine wa CCM ili mapacha hawa watatu wapate kuzuia kufukuzwa kwao kwenye CCM. Ni aibu sana kuona hata vyama vya upinzani navyo vimeingiliwa na mafisadi hawa mapacha watatu ambao ni hatari sana kwa taifa letu hili.

  Kama kawaida yake, Tanzania Daima, chini ya mhariri mkuu Absalom Kibanda, ambaye ameajiriwa na Lowassa kwenye jarida lake la Umoja, linaendelea kutumika kama jukwa lakuwasafisha mafisadi hawa.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  kheeee
   
 5. F

  Fareed JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa faida ya wengi, naweka post hii yangu ya zamani watu waelewe mchezo wa kifisadi unaochezwa na Lowassa, Rostam na Chenge kwa kutumia viongozi wa upinzani na waandishi wala rushwa:

  CHADEMA yatumika kuwaokoa Rostam, Lowassa wasifukuzwe CCM!

  CHADEMA sasa imeanza kutumika kuwasafisha Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge wasifukuzwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya CCM.

  Kutumika kwa CHADEMA ni sehemu ya mkakati wa Rostam, Lowassa na wenzake kuzuia wasifukuzwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) na nafasi zao nyingine za uongozi.

  Mkakati huo unahusu kuitumia CHADEMA na viongozi wa vyama vingine vya upinzani, kama CUF, NCCR Mageuzi, UDP, TLP na DP ya Christopher Mtikila, kutoa tuhuma za kupikwa kwa viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili ionekane kuwa viongozi wote wa CCM wana tuhuma za ufisadi na si Lowassa, Rostam na Chenge tu.

  Tuhuma hizo za kutengenezwa sasa zimeanza kusambazwa na kina Rostam dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Jakaya Kikwete, na viongozi wengine waandamizi wa chama ambao wanaheshimika katika jamii, akiwemo John Magufuli, Samuel Malecela, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Bernard Membe na wengine.

  Rostam na Lowassa wanaitumia CHADEMA ili kuzuia kufukuzwa kwenye CCM kupitia LIST OF SHAME mpya ya chama hicho cha upinzani ambayo imewataja kina Magufuli na Malecela. Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa, ameingizwa mkenge
  na viongozi wenzake ndani ya chama hicho kuitoa LIST OF SHAME mpya bila kujua kuwa mpango huo umepikwa na kina Rostam.
  Rostam na Lowassa kwa kutumia viongozi wa CHADEMA ambao wako nao karibu wamemuingiza mkenge Dk. Slaa aitoe List of Shame mpya ili kuleta mvurugano ndani ya CCM.

  Siyo "coincidence" hata kidogo kuwa CHADEMA waliibuka na LIST OF SHAME yenye majina mapya siku chache tu baada ya CCM kuwataka kina Rostam, Lowassa na Chenge wajiuzulu.

  Inaeleweka wazi kuwa Rostam na Lowassa wako karibu sana na baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA (siyo Dk. SLAA) na wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nao.

  "Wanachotaka kufanya kina Rostam, Lowassa na Chenge ni kuibua tuhuma mpya za uongo dhidi ya Kikwete, Magufuli, Malecela, Sitta, Mwakyembe, Sumaye na viongozi wengine wa CCM ili wapate kujitetea kwenye vikao vya NEC vijavyo kuwa mbona kuna viongozi wengi za CCM wenye tuhuma lakini wanatakiwa wajiuzulu wao tu," alisema mpambe mmoja wa Lowassa.

  Pia, Rostam na Lowassa wamekuwa wakitumia baadhi ya magazeti, likiwemo Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, katika mkakati huo wa kuibua tuhuma za kupikwa za ufisadi dhidi ya viongozi wengi zaidi ndani ya CCM ili wajinurusu kufukuzwa.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wiki hii CHADEMA ililazimika kukanusha habari za Tanzania Daima, gazeti la mwenyekiti wa chama hicho, zilizodai kuwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ametajwa kwenye List of Shame mpya ya CHADEMA.

  Lowassa amemuajiri mhariri mkuu wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, kwenye jarida lake la UMOJA na amekuwa akimtumia Kibanda mara kwa mara kutoa habari na makala za kumsafisha Lowassa, Rostam na Chenge kwenye Tanzania Daima.

  Inafahamika wazi kuwa Kibanda ana urafiki wa karibu sana na Lowassa na Rostam na amekuwa akitumiwa mara kadhaa kuwachafua maadui zao, ikiwemo Samuel Sitta, Bernard Membe, Harisson Mwakyembe, na wengine.

  Mafisadi wamekuwa wakipenda kulitumia sana Tanzania Daima mara nyingi kujaribu kujisafisha kwa kuwa linaheshimika kwenye jamii kwa kuonekana kuwa gazeti "huru" kuliko magazeti ya RAI na Mtanzania yanayomilikwa na Rostam.

  Kwa kufuata maelekezo ya Lowassa, Tanzania Daima juzi iliandika habari ya uongo kwa makusudi kuwa CHADEMA imemtaja Sumaye kwenye List of Shame mpya.

  Bado ni kitendawili kikubwa kwa nini Mbowe anamruhusu mhariri wake mkuu, Kibanda, kuwa mwajiriwa wa Lowassa na hivyo kuwa na mgongano wa kimaslahi na kimaadili (conflict of interest/ethical dilemma) katika kazi zake Tanzania Daima.
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo mwaka huu, kwa hiyo Chenge, Lowassa na Rostam wote ni people's power!!?? Mwisho tutasikia Mama Salma nae ni Chadema...
   
 7. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kazi ipo mwaka huu, kwa hiyo Chenge, Lowassa na Rostam wote ni people's power!!?? Mwisho tutasikia Mama Salma nae ni Chadema...
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Umeona eeh!!!
   
 9. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sina cha kusema maana akili za watu wengine huwa zinafikiria kinyume nyume
   
 10. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Thinking aloud, no truth it is just CCM propaganda.
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kikwete yupo safi bwana acheni propaganda za kupika. Kama wanajua uchafu wake siwauweke wazi? kwanini wanaogopa? mbona wale mafisadi wengine walianikwa uchafu wao.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ninavyo jua mimi Kikwete ni mshirika na Endrew Chenge kwenye viwanda vya kuchambua pamba kuli shinyanga na Lowasa ni swaiba wake mkuu hivyo kama watu hawa ni wachafu huwezi kumuweka pembeni Kikwete
   
 13. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,541
  Likes Received: 1,589
  Trophy Points: 280
  kumbe chenge alitakiwa kujihudhuru kitambo.

  hii nchi mafisadi wanalindana sana.
   
 14. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2015
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama kikwete angekuwa safi wala usingesikia huu uchafu unaoendela...mambo zaidi yatajulikana akiisha achia ngazi...ref kwa nyerere, nyerere alikuwa apendi haya mambo ya ki... ndiyo maana kama ikitokea ufisadi wa kimbwa kama huu watu walikuwa wakishughurikiwa... hakuwahi kusema"rudisheni pesa mlizo iba niwasamehe..." huu ni upuuzi wa hali ya juu una ugonjwa wa akili
   
 15. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2015
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mikataba kibao iliyo sainiwa kifisadi inamgusa mkwere kwa njia moja wa nyingine... hivyo kumtetea ni kujitoa ufahamu
   
 16. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2015
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,070
  Trophy Points: 280
  Kumekucha, kumekuchwa!

  ...ni miaka takribani mitano sasa, hebu tetea uhalali wa bandiko lako la tarehe 26 April 2011.
  wajuzi wa mambo wanasema 'time will tell', je hii miaka mitano inatwambia (inatu - tell) nini!?
   
 17. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,541
  Likes Received: 1,589
  Trophy Points: 280
  mkwere... naye fisadi !!

  hii hata mimi naikubali sn.
  wanaharibu alafu yeye anacheka cheka tu.
   
 18. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2015
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Utawala wa ccm mwisho wao ni mwaka huu
   
 19. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2015
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Fisadi mkubwa sana hujaona kwenye escrow alivyokuwa anawatetea wezi mwenzake ccm
   
Loading...