CHADEMA, CUF kuungana kuikabili CCM - NI TUKIO KUBWA LA KIHISTORIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, CUF kuungana kuikabili CCM - NI TUKIO KUBWA LA KIHISTORIA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  • NI TUKIO KUBWA LA KIHISTORIA

  na Abdallah Khamis


  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kile cha CUF viko mbioni kuungana na kuendesha maandamano makubwa ya pamoja kuishinikiza serikali kuwajibika kwa kushindwa kuongoza nchi.

  Wakati CUF kupitia kwa Mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba, kikiwa kimeweka wazi utayari wake wa kushirikiana na vyama vingine kufanya maandamano ya nchi nzima kutaka viongozi waliotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma wawajibishwe, CHADEMA jana kilisema nacho kipo tayari kuungana na chama hicho kufanikisha jambo hilo.

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema wapo tayari kuungana si na CUF tu, bali chama chochote chenye dhamira ya kurudisha mamlaka ya nchi kwa Watanzania.


  Mnyika alisema tayari Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alishatangaza wiki iliyopita akiwa bungeni kuwa watarudi kwa wananchi kuunganisha nguvu za pamoja na kufanya maandamano makubwa kupinga vitendo vya kifisadi baada ya kuona viongozi wa juu wa serikali wakishindwa kuchukua maamuzi magumu.


  Aliongeza kuwa hivi sasa umma unapaswa kuungana kuiwajibisha serikali na kumtaka Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, asirudi nyuma katika dhamira ya kuwatetea wananchi.


  "Si kuunganisha upinzani tu bali CHADEMA iko tayari kuendelea kuunganisha Watanzania wote wenye kutaka uwajibikaji wa serikali ya Kikwete kwa kuwa madaraka na mamlaka yote ni ya umma, serikali inafanya kazi kwa niaba ya wananchi," alisema Mnyika.


  Alibainisha serikali iliyopewa ridhaa na wananchi ya kuwaongoza inaposhindwa kusimamia masilahi ya wananchi na kuwalinda mafisadi inapaswa iwajibishwe na wananchi na kubainisha hatua hiyo itakuwa ni muendelezo wa harakati za ukombozi wa kweli wa Watanzania.


  Hata hivyo, Mnyika alisema maamuzi kamili ya namna ya kuunganisha nguvu hizo na kufanya maandamano makubwa yatakayotikisa nchi, yatatolewa Jumapili wiki hii baada ya kikao cha Baraza Kuu la CHADEMA kukutana.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa vizuri sana kama CUF ingevunja na ile ndoa yake na CCM.
  Otherwise Siwaamini CUF hata kidogo.
   
 3. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Siungi mkono hata kidogo chadema tuna jitosheleza sana
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  JK kishamaliza kazi... Mkakati utabadilika?
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mnajitosheleza kwa viti 48 bungeni........?!!!!!!!!!
   
 6. MWIBA WA KATANI

  MWIBA WA KATANI Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi habari zimepikwa na watu wa chadema kwa kutumia gazeti lao la propaganda la tanzania daima.nilisikiza kwa makini hotuba ya prof.lipumba hakuna mahali aliposema cuf itaungana na chadema kuunda maandamano ya pamoja.huu ni uzushi.alichosema ni kwamba cuf itatakutana kujadili kuandaa maandamano ya kushinikiza kujiuzuru kwa mawaziri na uwajibikaji mwingine.tanzania daima muwe wakweli.cuf inajitosheleza kufanya kile inachotaka kufanya bila boost kama wengine.
   
 7. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tuwe makini na mambo tunayofikiria kuyafanya
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hivyo viti 48 vilisababisha bibi kiroboto kudondosha wigi mjengoni, hata jk hahudhurii misiba kwa raha kama desturi yake, CHEZEA CDM WEWE!!!!!
   
 9. Moseley

  Moseley Senior Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  WEWE NDO ULIPIKA??

  NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK

  Check hii link ..

  http://www.mwananchi.co.tz/news/49-uchaguzi-mkuu/22328-lipumba-jk-amemziba-pinda-mdomo.html

  Dotto Kahindi na Geofrey Nyang'oro

  MWENYEKITI cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka jamii kutomhukumu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kushindwa kushughulikia madai ya wabunge kutaka mawaziri wajiuzulu akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete amemziba mdomo.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema hata kama Pinda angekuwa na utashi wa kuzungumzia suala hilo, asingeweza kusema chochote kwa kuwa Rais Kikwete alimziba mdomo... "na suala hilo pia liko juu yake."

  Profesa Lipumba alimtuhumu Rais Kikwete kuwa chanzo cha kuwapo kwa mawaziri wabadhirifu kwa kile alichoeleza kuwa mara zote amekuwa akiwakingia kifua.

  "Tatizo la ubadhirifu haliwezi kuisha katika Serikali ya Awamu ya Nne maana tatizo siyo watendaji wala mawaziri, ni Rais Kikwete mwenyewe… amekuwa ni mtu asiyekuwa na uamuzi," alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

  "Haishangazi kuona mawaziri katika wizara moja hawaelewani. Kuna mawaziri wana nia njema na wanasimamia haki, lakini hata wakitoa mapendekezo yao yanapuuzwa na wapo ambao wanatumia nafasi zao vibaya huku Rais akiendelea kuwachekea."

  Alisema CUF kinaangalia namna kitakavyounganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani kikiwemo Chadema kuongoza maandamano nchi nzima ili kushinikiza mawaziri wanaotuhumiwa kwa madai mbalimbali wajiuzulu.

  Alisema kwa namna yoyote ile Waziri Mkuu asingeweza kuamua jambo bila kupewa ruhusa na Rais na kushindwa kuwawajibisha watu hao ni dhahiri kuwa Rais hakumtaka kufanya hivyo.

  Alidai kuwa Baraza la Mawaziri limegawanyika katika makundi na baadhi wamejenga chuki baina yao kutokana na Rais kuendelea kuwalea watendaji wabovu huku akipuuza ushauri anaopewa.

  Alipongeza na kuunga mkono hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.


  Alisema jukumu kubwa la wabunge sasa ni kushinikiza Waziri Mkuu kujiuzulu kutokana na kushindwa kutumia nafasi yake kuwawajibisha mawaziri wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za umma.
  Profesa Lipumba alisema katika kumshinikiza Rais Kikwete kuchukua hatua dhidi ya watendaji wabadhirifu serikalini wakiwemo mawaziri, watawashirikisha wananchi kwa kuandaa maandamano nchi nzima.

  Alimpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kwa kutoa ripoti aliyoeleza kuwa imeibua madudu bila upendeleo.

  Alisema jamii inahitaji kujua matumizi ya Serikali katika shilingi inayotokana na kodi za wananchi na namna zinavyosimamiwa huku akisema ubadhilifu uliojionyesha katika ripoti ya CAG, ni aibu kubwa kwa Serikali ya Kikwete.

  Kauli hiyo ya Profesa Lipumba imekuja wakati tayari Chadema kimetangaza kuitisha maandamano ya wananchi ili kuiwajibisha Serikali, iwapo Rais Kikwete hatawafukuza mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma hizo.


  Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika imeeleza kuwa chama hicho kitatumia Ibara ya 8 (1) (a) ya Katiba kuunganisha nguvu za wananchi katika kutimiza azma hiyo.

  "Iwapo Rais Kikwete hatavunja Baraza la Mawaziri au kuwafukuza mawaziri hao… pamoja na hatua zinazoendelea sasa za kuwasilishwa hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu; Kurugenzi ya Habari na Uenezi itawasilisha taarifa kwenye vikao vya chama ili Ibara ya 8 (1) (a) Katiba ya nchi itumike kuunganisha nguvu za wananchi kuiwajibisha Serikali," alisema Mnyika katika taarifa hiyo.

  Ibara hiyo inaeleza kuwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia na kwamba wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake kutoka kwa wananchi.

  Mnyika alisema Rais Kikwete anapaswa kutekeleza haraka wito wa kuvunja Baraza la Mawaziri au kuwafukuza baadhi, kwani sehemu kubwa ya masuala yaliyokuwa yakijadiliwa bungeni yakiwemo ya ufisadi na matumizi mabaya yanatokana na udhaifu wa uongozi wao.

  Alimtaka Rais Kikwete kutumia mamlaka anayopewa na Katiba katika Ibara ya 57 (1) (c) inayomruhusu kufuta uteuzi na kuwaondoa madarakani mawaziri pindi anapoona inafaa kufanya hivyo.

   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ndoa hiyo iko visiwani siyo bara!
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Ndoa ina status nyingi labda iko kwenye 'separation'!
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Duh, hiyo ndoa babu kubwa, halali visiwani lakini haramu bara...! Yaani mapenzi motomoto visiwani lakini bara ni kununiana mtindo moja...! Kwa maana nyingine ndoa zinazofungwa visiwani, hazitambuliki bara ... hii mbona hatari!
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  kwa kuwa suala la kuiwajibisha serikali ni la kila mwananchi, sioni sababu ya kutowaamini. Hata wanaccm waliokerwa na ubovu wa Serikali wanakaribishwa kwenye maandamano.
   
Loading...