CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!.

kwani walionda mahakamani ni chadema au upinzani.
hahahhh ccm bhana hya nikuulize kuendana na makubaliano yale je 1/3 inatakiwa wa wabunge wote 9 au kundi la upinzani??? na je kwenye kundi la upinzani inatakiwa iwe 1/3 au ni chadema 1/3 na pia cuf iwe 1/3 ukinijibu hili ndio utakuwa umenisaidia sana
 
Mkuu Pascal Kusema ukweli kabisa, Mimi Ni mshabiki wako Mkubwa, ila Kuna kipindi unapungukiwa hekima, Na kipindi hiki nadhani Ni zaidi.
Huwezi wapangia watu wenye mrengo Wao namna ya kuendesha mambo Yao kwa kadiri wanavyoona Wao, provided hawa athiri haki za watu wengine.
Na ukiangalia kwa Makini, Chadema wana set trend ya kutaka Kila jamboo lenye utata litafsiriwe kisheria.... Itatisaidia Sana huko tuoendako.

Ni mwehu Tu anaeweza kukwambia Jirani yake mbona unakula ugali samaki wakati Kuna maziwa Na Nyama kwenye friji....
Utainekana wa hovyo Sana,.... Unakaribia hapo.
Mkuu njaa inapotaka kushiba inapiga hesabu kali sana.
 
Wanabodi
Declaration of interest. Paskali sio mwanachama, mfuasi, mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania Mzalendo wa nchi yake anayetanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kutoa mawazo, maoni na mapendekezo yake freely kwa ukweli daima bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au utamuumiza nani, kwa sababu ukweli ni ukweli tuu na utasisima mpaka mwisho.

Nayaandika haya kwa nía njema ile ile ya kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tulaani na kwenye madhaifu tukosea kwa nia ya kujenga, "constructive criticism", kama tunavyoikosoa serikali yetu kwa lengo la kuisaidia, sisi ambao sio watu wa partisan politics pia tutavikosoa vyama kwa lengo la kuvisaidia.

Kati ya udhaifu mkubwa kabisa wa Chadema na ndio ambao unaifanya Watanzania kushindwa kuiaminia na kuikabidhi ikulu yetu ni kupoteza muda mwingi kwa kukumbatia siasa za matukio badala ya siasa za mikakati, kitu kinachoifanya kuendelea kupiga mark time na ikulu kuisikia tuu.

Kwa jinsi watu walivyoichoka CCM, Chadema zamani ingeishakuwa Ikulu siku nyingi kama ingejikita katika siasa za kimipango mikakati na sio sia za matukio na hizi za maji taka.

Bunge la bajeti linakwenda kuanza ndio most serious na longest session ambapo wapinzani makini wenye utayari wa kutawala nchi wanatakiwa kuichallenge serikali kwa bajeti mbadala kwenye kila sekta kuonyesha kuwa Watanzania walifanya makosa sana kuichagua CCM iwapo wangekuwa wao wangefanya hili na lile na nchi yetu ingekuwa mbali ili 2020 Watanzania wawaaminie wawakabidhi nchi, lakini suburini tutaambiana, kama mwanzo wenyewe ndio huu!.

Niliishasema siku nyingi kuwa CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!
Lakini kwa hii CCM ya Magufuli inavyojipanga, sijui tutarajie nini kwa opposition come 2020.

Naomba kukiri kupandisha bandiko hili kutokana na bandiko hili

Kiukweli kama hili litafanyika, Chadema kitakuwa ni chama cha ajabu sana! . Kinapeleka mahakamani issue ndogo ambayo sio issue kabisa ya kisheria bali ni kikanuni tuu!, lakini kumetokea very serious issues za kukanyagwa kwa katiba ambako ndiko haswa kungehitaji legal interpretation Chadema inakupiga kwa kuunda UKUTA na kuhamashisha mandam ano na mikutano nchi mzima!.

Spika is right, kati ya wabunge 9, watatu ni wanawake. CCM ina nafasi 6 imepeleka wanawake 6 na wanaume 6. Opposition wana nafasi 3, walipaswa kupeleka wagombea angalau 6 ambapo 3 wanaume, 3 wanawake.

Hata kama kati ya nafasi 9 za Tanzania wanawake ni watatu na tayari CCM inao wanawake watatu, wanaochagua wabunge wa EALA ni Bunge la JMT na sio CCM, hivyo hiyo haki ya female represention lazima ionekana kwa vyama vyote ili wabunge wa Bunge la JMT wawe na choice to choose from all parties na sio kulazimishwa kuwakumbatia wagombea wa CCM.

Nadhani Chadema wanamtegemea sana Lisu kwenye legal interpretation, yes Lisu ni mwanasheria mzuri, nguli na mbobezi ila sio mzuri saana kivile kwenye kanuni, udhaifu wa Lisu ulionekana wakati wa muswada wa katiba aliwaingiza chaka opposition wote kama nilivyo eleza hapa
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Hivyo kama ndiye aliyewashauri Chadema waende mahakamani kupinga uchaguzi wa EALA wakati uchaguzi ni leo, the anawaingiza tena chaka.

The best thing to do kwa Chadema ni kufuata tuu sheria, taratibu na kanuni, kwa Chadema kurekebisha makosa katika muda waliopewa.

Japo ni kweli Mahakama ndio chombo rasmi cha kutoa legal interpretation nchini Tanzania hivyo Chadema kinaitumia haki hiyo, kwanza wakamilishe taratibu na kanuni za kibunge kwa kufuata maelekezo ya Spika wakati wakijaribu kusimamisha uchaguzi huo mahakamani, kwa sababu uwepo wa wagombea kutoka Chadema sio prerequisite ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Mahakama haitausimamisha uchaguzi huo kwa respect ya the principles of separation of powers kutoingilia Mhimili wa Bunge, na hata wakiusimamisha , bado uchaguzi utafanyi kwa Mhimili wa Bunge hautakubali kuingiliwa na Mahakama, hivyo Chadema wata loose big time.

Hawajifunzi kwa CUF ambao ni loosers, CUF walipotangaza kususia uchaguzi wa marudio Zanzibar walidhani uchaguzi ungeshindikana, amini usiamini saa hizi Maalim anajuta, anautamani hata ule umakamo! .

Kiukweli Chadema ni chama cha ajabu sana, kinakimbilia mahakani kutafuta legal redress kwenye trivia issue ndogo tuu za kanuni, halafu very serious issues kama kuvunjwa kwa katiba na rais wa JMT, wao ndio wana deal nayo kwa kuunda UKUTA na kupanga maandamano na mikutano nchi nzima?!.

Katiba imetoa uhuru kwa vyama vya siasa kukutana na kufanya mikutano ya kisiasa. Ametokea mtu aliyeapa kuilinda katiba lakini akaikanyaga. This is very serious allegations ambazo ndizo zingehitaji haswa a legal redress, kutoka kwa mabingwa na wabobezi wa sheria.

Nilijitahidi kutafuta Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!

Chadema walipounda UKUTA kupinga udikiteta, niliwauliza hivi katiba ikikiukwa solution yake ni kufanya maandamano na mikutano? .Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!

Mwaka 2014 wakati tukisubiria uchaguzi wa 2015, niliwahi kutoa ushauri wa bure kwa Chadema kuhusu udikiteta CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
Halafu watu kama hawa ndio watujie ile 2020 kuwaomba Watanzania wawakabidhi nchi?!.

Pia nilishauri
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Uchaguzi wa Mwaka 2015 Chadema ilikuwa ina stand better chances kuchukua nchi only if Chadema wangezitia hili
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Hivyo wote wenye matumaini ya mageuzi Tanzania, wana very high expectations na Chadema, as a leeder on opposition atakaye kwenda kuipumzisha CCM, lakini unfortunately and very sad kwa nchi yetu Tanzania, Chadema ina wa let down kwa issues kama hizi za kijinga kijinga zinazoipotezea muda Chadema kushinda mahakamani kufunga na kufungua, 2020 hiyo hapo.

CCM iliishachokwa siku nyingi, kuna watu kibao wangependa kuipiga chini CCM hata kesho, wakiwemo CCM wenyewe, tatizo ni waikabidhi nchi kwa nani? .

Tanzania bado hatuna kabisa a serious opposition ya kuiangusha CCM 2020, hivyo kwa Watanzania wengi hata 2020 wataingia kwenye uchaguzi wakiwa faced na two choices, in between the two devils, you choose the lesser! .

Niliwahi kusema mahali kuwa CCM ni li zimwi na Watanzania wengi wanajua wakiwemo wana CCM wenyewe, lakini unapokuwa faced na mazimwi mawili, unachagua zimwi likujualo, better a devil you know than you don't know, sasa kama mambo ya Chadema ndio kama haya kwenye mambo madogo madogo, tutegemee nini 2020? .

Naelewa matokeo ya ukosoaji wowote wa Chadema humu jf, naomba kuwahakikishia Wanachadema kuwa mimi ni miongoni mwa watoaji wa fedha zangu kwenye ruzuku yao hivyo nina haki yote ya kuzungumza lolote kuhusu hatma ya matumizi ya kodi yangu ndio maana nilishauri Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Nawatakia Bunge jema.
Jumanne njema.
Paskali
Well said P
 
Mkuu Pascal Kusema ukweli kabisa, Mimi Ni mshabiki wako Mkubwa, ila Kuna kipindi unapungukiwa hekima, Na kipindi hiki nadhani Ni zaidi.
Huwezi wapangia watu wenye mrengo Wao namna ya kuendesha mambo Yao kwa kadiri wanavyoona Wao, provided hawa athiri haki za watu wengine.
Na ukiangalia kwa Makini, Chadema wana set trend ya kutaka Kila jamboo lenye utata litafsiriwe kisheria.... Itatisaidia Sana huko tuoendako.

Ni mwehu Tu anaeweza kukwambia Jirani yake mbona unakula ugali samaki wakati Kuna maziwa Na Nyama kwenye friji....
Utainekana wa hovyo Sana,.... Unakaribia hapo.
 
Mzee wa kungata na kupuliza!
Mayalla siyo mtu wa kumwekea dhamana...

Ova
Nashangaa anauliza na kuleta mada ya vitu anavyovijua na vingine aliuliza yy mwenyewe kwenye mkutano wa wahariri na aliambiwa hakuna mpango wa vitu hivyo,. Hivi anajua moja ya kipaumbele cha ukuta ni kupelekea mjadala mpana wa kuwaamsha wananchi waidai katiba yao inayovunjwa pamoja na rasimu iliyotumia mabilioni yetu ya kodi kwa ajili ya kukusanya maoni yetu,,? Hv Pascal hujui wanavyoenda kuomba tafsiri mahakamani ni kuijenga haki ya kimahakama huko mbeleni hata kama jambo hilo leo halina nguvu kihivyo, kwani unafikiri chadema hawajui hata hao wawili waliowapeleka sio rahisi kushinda sababu ya uwingi wao,? Unapozungumzia tume huru unataka waidai vp kwa katiba na ubabe huu bila kurekebisha na kupata nguvu kimahakama,? Hv hukumbuki ulivyojibiwa kwa dhalili siku ile pale pamoja na kuuliza haki ya matumizi ya uchukuaji wa hela na kuzipeleka kwingine ukitaka kujua ni kwa nguvu ipi ya kisheria alizozitumia kufanya vle na ukabaki ukitingisha kichwa pamoja na kutupiliwa mbali suala lako la katiba,? MI NACHOTAKA KUKUULIZA PASCAL UMEPEWA NINI AU UMEKULA NINI HADI SIKU HIZI UWE KTK UKINYONGA HUO,?
 
Mie nawashangaa nikwann wanalazimishia chaguo la masha na wenje tu?!
kwani ukipeleka majina ya wanachadema wa5 (wakiwemo wanawake) alafu miongoni mwao wakapatikana wa2 kuna tatizo gani?!
hao wanaolazimishiwa kama wangekuwa majembe wangelishinda huko jimboni.....masha mwenyewe wakuja tu kakuta wafia chama ambao leo wanaonekana si chochote ndani ya chama!

Kwani kanuni zinasemaje ? CHADEMA wamekiuka kanuni yoyote labda ? Nadhani tukijikita kujadili hapo na kupata jibu, ndo tunaweza kukubaliana na Paskali ama la

Na kwa upande wako wewe Paskali na wengine wenye mtazamo kama wako, ni kwamba CHADEMA hawatapoteza nafasi yao ya uwakilishi ktk bunge la EALA.

Ni kwa sbb, hii ni birth right yao. Na nadhani tatizo hapa ni wapinzani na watani wao kutokuwataka watu ambao chama kimewateua i. e Wenje na Masha !!

Kwa lugha rahisi kabisa, hawa wanachezeana michezo yao ya kisiasa tu sawasawa na ilivyokuwa ktk uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambapo mwisho wa siku intimidation za CCM/serikali zilibuma na TL kuibuka mshindi....

Mwisho, Paskali Hebu tuambie kuna kanuni yoyote iliyokiukwa na CHADEMA ?

Hayo mengine sijui ya CHADEMA na ikulu unajua kabisa yalivyo na mfano halisi ni CUF na kule Zanzibar ktk uchaguzi wa mwaka 2015.....
 
Paskal, katika nafasi za ubunge EAL, ukiongea ccm 12, zungumzia na cdm 2, zungumzia na cuf 1 na siyo upinzani 3, kwa sababu hata huko mahakamani hawajaenda upinzani bali cdm, NIAMBIE ONE THIRD YA MBILI UNAIPATAJE ? ukiwa kama mtaalam wa hesabu .
One third ya mbili inapatikana kimahesabu,lkn labda bwana Pascal na spika watuambie one third ya watu wawili wanapatikanaje,??
 
uchambuzi mzuri. unajua kwa nini prof shifji alikwepa kuzungumza na wewe kuhusu udikteta tanzania. kwa sababu haupo ila ni dhana inayopandikizwa na upinzani.
Sio kweli alikataa jwa sababu aliogopa kuitwa msaliti au kusumbuliwa mahakamani kama Lisu,kwa hiyo labda akaona umri na mahusiano yake aliache,kwa maana ishara ya kukaa kimya unamaanisha kukubali ulichoulizwa
 
Nashangaa anauliza na kuleta mada ya vitu anavyovijua na vingine aliuliza yy mwenyewe kwenye mkutano wa wahariri na aliambiwa hakuna mpango wa vitu hivyo,. Hivi anajua moja ya kipaumbele cha ukuta ni kupelekea mjadala mpana wa kuwaamsha wananchi waidai katiba yao inayovunjwa pamoja na rasimu iliyotumia mabilioni yetu ya kodi kwa ajili ya kukusanya maoni yetu,,? Hv Pascal hujui wanavyoenda kuomba tafsiri mahakamani ni kuijenga haki ya kimahakama huko mbeleni hata kama jambo hilo leo halina nguvu kihivyo, kwani unafikiri chadema hawajui hata hao wawili waliowapeleka sio rahisi kushinda sababu ya uwingi wao,? Unapozungumzia tume huru unataka waidai vp kwa katiba na ubabe huu bila kurekebisha na kupata nguvu kimahakama,? Hv hukumbuki ulivyojibiwa kwa dhalili siku ile pale pamoja na kuuliza haki ya matumizi ya uchukuaji wa hela na kuzipeleka kwingine ukitaka kujua ni kwa nguvu ipi ya kisheria alizozitumia kufanya vle na ukabaki ukitingisha kichwa pamoja na kutupiliwa mbali suala lako la katiba,? MI NACHOTAKA KUKUULIZA PASCAL UMEPEWA NINI AU UMEKULA NINI HADI SIKU HIZI UWE KTK UKINYONGA HUO,?
Paskali kapenyezewa bahasha itakuwa

Ova
 
kasoro gani ssa?? kwani unafkiri wakati wanateua chama kizima chenye wanasheria kma kina safari na mallya hawakujua kanuni??? embu acheni basi chama kifanye kazi yake ili tafsiri ya mahakama itumike kma rejea kwa issue kma hii huko mbele!!!!
Nadhani Umeona kilicho wakuta kulikuwa na shida gani kupeleka wagombea watatu maana hapo kusinge kuwa na kura za ndio au hapana
 
Nadhani Umeona kilicho wakuta kulikuwa na shida gani kupeleka wagombea watatu maana hapo kusinge kuwa na kura za ndio au hapana
Hakuna shida kwa upinzani kupeleka wawili shida inakuja ccm kuweka mbele uchama ssa wamefanya ivo kuikomoa chadema sijui watagain nni??? Anyway kwa ushabiki huu nliouona jana wa kivyama sitegemei lolote jipya EALA na mtavuna mlichopanda CCM
 
Mkuu Pascal Mayalla

Heshima kwako.

Maoni yako kwamba Watanzania prefers the devil they knowc (CCM) to the angel they do not know (Opposition) ni maono sawia.

Nafikiri wakati umefika kwa waandishi nguli ukiwamo Mwandishi Mwanasheria Msomi Ndg Pasco Mayalla kuandika kitabu/vitabu vinavyoelekeza namna vyama vya upinzani vinaweza kufanya ili kuiondoa CCM madarakani.

Angalizo langu kwa utafiti mdogo niliofanya, Watanzania wengi walau 60% wanaikubali sana CCM. Tena wanaichukulia kama chama cha kufa na kuzikana. Maana hiki ndio kiwango ambacho CCM imejikita mioyoni mwa Watanzania wengi.

Maswali ni je, Wapinzani waendelee kutegemea makosa ya CCM ili wakubalike kwa Wananchi? Ama Wapinzani waendelee kutegemea minyukano ndani ya CCM ili wapo wapenye na kushinda uchaguzi mkuu? Ama Wapinzani wakomae na mikakati yao, huku wakipima mafanikio kwa kila kipindi kifupi?


 
Back
Top Bottom