Chadema, CCM ni vita mpya Arusha Kuhusu uchaguzi wa Madiwani

JOB SEEKER

Senior Member
Aug 1, 2011
145
33
Sunday, 1/1/ 2012


Peter Saramba, Arusha
HOMA ya uchaguzi mdogo kujaza nafasi tano za viti vya udiwani Manispaa ya Arusha imezidi kupanda kati ya CCM na Chadema huku kila upande ukijinasibu kuvinyakua.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, viongozi wa vyama hivyo viwili vyenye upinzani mkubwa wilayani Arusha, walidai kuwa sasa wameanza maandalizi ya ushindi wa nafasi hizo.

Nafasi hizo zilizobaki wazi baada ya baadhi madiwani kuvuliwa uanachama na mmoja kufariki dunia.

Chadema iliwavua unachama madiwani wake watano, wakiwamo wanne waliokuwa wakishikilia kata za Kimandolu, Themi, Elerai na Kaloleni pamoja mmoja wa Viti Maalumu waliodaiwa kukaidi maagizo na maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu muafaka wa nafasi ya umeya wa Arusha.

Waliovuliwa uanachama na kugonga mwamba mahakamani walikofungua kesi na kata zao kwenye mabano ni pamoja na Estomih Mallalh (Kimandolu), Rueben Ngowi (Themi), John Bayo (Elerai), Charles Mpanda ‘Rasta’ (Kaloleni) na Rehema Mohamed wa Viti Maalum.

CCM nao juzi walipoteza diwani mmoja baada ya Bashir Msangi wa Kata ya Daraja II kufariki dunia ghafla usiku wa kuamkia Desemba 26, mwaka huu, hivyo kufanya idadi ya kata zilizo wazi kuwa tano.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo licha ya kuelezea masikitiko ya chama chake kutokana na kifo hicho, alisema wanaimani watanyakua viti hivyo.

“Pamoja na kata ya Daraja II, pia tumejipanga kunyakua viti vingine vya Kaloleni, Elerai, Kimandolu na Themi vilivyobaki wazi baada ya madiwani waliokuwa wakivishikilia kufukuzwa uanachama na chama chao,” alitamba Kiondo

Kiongozi huyo wa CCM alisema tayari chama hicho kimerekebisha kasoro nyingi zilizosababisha kipoteze viti hivyo pamoja na kile cha ubunge Jimbo la Arusha mjini walivyovyokuwa wakivishikilia kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, naye alitamba chama chake kutetea viti vinne walivyoshinda kwenye uchaguzi uliopita pamoja na kuibwaga CCM kata Daraja II .

Nanyaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mkoa wa Arusha, alisema maandalizi kwa ajili ya kurejesha kata zao umekamilika na hivi sasa wameanza mkakati wa kunyakua kata ya Daraja II ili uchaguzi utakapotishwa, wabaki na kazi ndogo ya kupita kuwasalimia wananchi na kumtambulisha mgombea wao.

“Kama tuliweza kuwashinda CCM kipindi kile walipokuwa wamoja, basi hivi sasa tuna sababu nyingi za kushinda baada ya chama hicho kutafunwa na migogoro ya makundi na falsafa ya kujivua gamba,” alitamba Nanyaro.

Licha ya tambo hizo, vyama vyote viwili vinakabiliwa na changamoto nyingi zinazoelekea kufanana, mojawapo ikiwa ni kuibuka kwa makundi kutokana na sababu mbalimbali zinazotafautina.

Ingawa mpasuko huo unaweza kuonekana mdogo kwa viongozi na wana Chadema, bado unaweza kuleta madhara iwapo madiwani waliofukuzwa watakuwa na ushawishi kwenye kata zao.

Hata hivyo CCM kimeonekana kupoteza ushawishi katika makundi mbalimbali mjini hapa hali inayosabisha kuwepo hofu ya kupoteza kwenye uchaguzi huo.

SOURCE:Mwananchi ,Jumapili 1/1/2012
 
Haya sasa. Ngoma inogile,wana Arusha musituangushe nasisi huku Mwanza mikakati ya kutetea tena kiti cha kata ya Kirumba kilichoachwa na marehemu kamanda Nova imeshakamilika,tunasubiri kipyenga cha refarii mechi ianze.Peoooooooples Poweeeeer
 
Haya sasa. Ngoma inogile,wana Arusha musituangushe nasisi huku Mwanza mikakati ya kutetea tena kiti cha kata ya Kirumba kilichoachwa na marehemu kamanda Nova imeshakamilika,tunasubiri kipyenga cha refarii mechi ianze.Peoooooooples Poweeeeer
Na sisi shinyanga tumeshamaliza kazi ya kuchukua kata ya mwawaza ambayo ilikuwa mikononi mwa magamba
 
Filimbi inapulizwa lini wacha tuone mtihani huu kama NEC mpya ya JK kama itashinda. tusubiri ... machaliii A-town msituangushe kulinda kura
 
Back
Top Bottom