Chadema candidate falls ill on the campaign trail

Status
Not open for further replies.

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Chadema candidate falls ill on the campaign trail

By Polycarp Machira

By Polycarp Machira
THE CITIZEN

Chadema's candidate for the Kiteto by-election, Mr Victor Kimesera, was yesterday airlifted to Dar es Salaam after falling ill while campaigning in the constituency.

Mr Kimesera is among those vying for the seat following the death last year of CCM's Benedict Losurutia.

A chartered plane carrying Mr Kimesera arrived at Dar es Salaam's Julius Nyerere International Airport shortly before 2pm.

A Knight Support ambulance was on hand to rush the aspirant to Aga Khan Hospital. Efforts to get Mr Kimesera to comment on his illness failed.

However, Chadema official Ben Kapwani, who accompanied Mr Kimesera from Manyara Region, said they were forced to fly the aspirant to Dar es Salaam after his condition deteriorated rapidly.

He was seriously sick and could not walk. We had to carry him on stretcher and into an ambulance. He was complaining of acute stomach pains, said Dr Kapwani, who is also the Chadema Iringa regional chairman.

Mr Kimesera was well until Saturday evening when they had supper together before retiring for the night.

Dr Kapwani said he was woken up yesterday morning by their driver who informed him that Mr Kimesera was very ill.

Being a medical doctor, Dr Kapwani administered First Aid on Mr Kimesera after which the patient vomited. It was then that it was decided that the candidate be flown to Dar es Salaam for further treatment.

Chadema chairman Freeman Mbowe told reporters yesterday that it was too early to speculate on the cause of Mr Kimesera�s illness, saying doctors were still trying to find out what he was suffering from.

It's still too early to jump to conclusions, but nothing can be ruled out at this moment. We have many political enemies who will stop at nothing to derail our campaign for the seat, he said.

Mr Mbowe added that prior to the campaign, the there was a petition by CCM members seeking to bar Mr Kimesera from vying for the seat. It was, however, thrown out on the grounds of lacking legal basis.

He said Chadema stood a good chance of winning the seat after other opposition parties rallied behind its candidate, adding that Mr Kimesera's illness had not halted Chadema's campaign.

People should not be discouraged by what has happened. We still have three teams campaigning in the region and hope to win the seat and save the people of Kiteto from endless problems, Mr Mbowe added.
 
My God!
Mgombea alishwa sumu

na Irene Mark
Tanzania Daima

MGOMBEA Ubunge wa Kiteto kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Victor Kimesera (68), anahofiwa kula chakula chenye sumu, juzi usiku.
Kimesera, mgombea anayeungwa mkono na vyama vitano vya upinzani, ambavyo viko kwenye ushirikiano, anadhaniwa kula chakula hicho, saa tano usiku kwenye hoteli ndogo baada ya kuhitimisha siku ya nne ya kampeni hizo.

Hali ya mgombea huyo anayepewa nafasi kubwa ya kunyakua jimbo hilo kutokana na kuwa na rekodi ya aina yake tangu alipoanza kugombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 1995, ilianza kubadilika jana alfajiri baada ya kuanza kuhisi maumivu makali ya tumbo.

Kutokana na kubadilika kwa hali ya afya ya mwanasiasa huyo, ambaye ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, familia na viongozi wa chama hicho cha upinzani walilazimika kufanya mipango ya dharura ya kutuma ndege maalum ya kubeba wagonjwa iliyokwenda kumchukua Kiteto na kumsafirisha hadi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Awali kabla ya kumsafirisha hadi jijini Dar es Salaam, Kimesera alipata matibabu ya awali katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto iliyopo Kabaya ambako alipewa dawa maalum iliyomwezesha kutapika na kumpa nafuu kiasi.

Ndege hiyo ya kukodi yenye namba za usajili N30MS iliyokuwa na maandishi yanayosomeka ‘Fly Medical Service' (ndege mahususi ya kubeba wagonjwa) iliyombeba Kimesera, ilitua katika uwanja wa zamani wa ndege wa Mwalimu Nyerere (Terminal One) majira ya saa 8.00 mchana.

Katika ndege hiyo, Kimesera aliyekuwa akilalamika kwa maumivu makali alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Iringa, Ben Kapwani ambaye kitaaluma ni daktari, aliyekuwa sambamba na mgombea huyo katika kampeni za ubunge zilizoanza katikati ya wiki iliyopita.

Waandishi wa Tanzania Daima waliokuwa uwanjani hapo wakati ndege hiyo ikitua, waliweza kuwaona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika wakiwa uwanjani hapo kumpokea mwanasiasa huyo.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Kimesera aliyekuwa katika kitanda maaluma cha wagonjwa na aliyekuwa amevaa fulana yenye kola yenye michirizi ya rangi ya bluu na nyeupe, huku akiwa na suruali ya kaki, aliingizwa katika gari maalum la wagonjwa la Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support, lenye namba T 360 AAU.

Kabla ya kuingizwa katika gari hilo la wagonjwa, daktari wa Knight Support alilazimika kumchoma Kimesera sindano ya Tramadol ili kumpunguzia maumivu aliyokuwa akipata kutokana na kulalamika.

Alipoingizwa ndani ya gari hilo la wagonjwa, mgombea huyo, ambaye alitulia kiasi baada ya kudungwa sindano hiyo ya maumivu, alifunikwa shuka jeupe na kwa mwendo wa pole gari hilo likaanza safari ya kumpeleka hospitali.

Msafara huo uliokuwa na magari matatu, la wagonjwa, la Mbowe na la Tanzania Daima ulipita kwa mwendo wa taratibu ukiongozwa na king'ora katika barabara za Nyerere, Bibi Titi hadi katika Hospitali ya Aga Khan iliyo eneo la ufukwe wa Upanga jijini Dar es Salaam.

Ulipowasili katika hospitali hiyo majira ya saa 8:32, Kimesera alitolewa ndani ya gari la wagonjwa na kwa haraka haraka akaingizwa katika chumba maalum alikoanza kupatiwa matibabu.

Mmoja wa viongozi wa kampeni za uchaguzi huo katika kambi ya upinzani, Dk. Kapwani, alisema afya ya mgombea huyo ilikuwa nzuri hadi juzi usiku baada ya kupata chakula kwenye hoteli hiyo.

Dk. Kapwani, alisema kabla ya kwenda kulala walipata chakula kwenye hoteli hiyo wakiwa na baadhi ya viongozi na wanachama waliokuwapo katika kampeni za siku hiyo.

"Mpaka jana usiku (Jumamosi) muda ya saa tano usiku hivi tulikuwa kwenye hoteli hiyo ndogo pamoja na wajumbe wengine na mgombea wetu… tuliagiza na kuletewa chakula kila mmoja kwenye sahani yake.

"Wote tulikula, nikahakikisha amekwenda kulala nyumbani kwake. Muda wote huo alikuwa mzima wa afya. Leo (Jumapili) saa moja asubuhi, dereva alinifuata akaniambia kuwa mzee anaumwa sana, lakini hakula kitu chochote hadi alfajiri alipoanza kuumwa tumbo.

"Nilifika hadi alipolala kwa bahati nikaambiwa amepelekwa hospitali ya wilaya, nilipokwenda huko nikamkuta hali yake mbaya… alikuwa na maumivu makali ya tumbo kiasi cha kushindwa hata kuvaa nguo.

"Ilifika mahali alishindwa kuzungumza kabisa kutokana na maumivu. Madaktari, walipompima kila kitu kilikuwa normal, lakini alizidi kulalamika kwa maumivu. Alikuwa na maumivu makali sana.

"Kuona hivyo, madaktari wa hospitali hiyo walimpa dawa ambapo baada ya muda mfupi alianza kutapika vitu vya ajabu. Alitapika vitu vyenye rangi tofauti ikiwamo nyekundu… yaani havieleweki.

"Hapo tukajua atakuwa amekula chakula chenye sumu. Walimchoma sindano ya kupunguza maumivu tukaweza kupanda naye kwenye ndege ingawa aliendelea kuhisi kutapika," alisema Dk. Kapwani baada ya Kimesera kufikishwa na kuingizwa kwenye chumba cha madaktari wa Aga Khan.

Alisema, wakati wote huo, walikuwa wanawasiliana na makao makuu ya chama hicho, kabla ya ndege iliyowabeba kwenda Dar es Salaam kuwasili kwenye uwanja mdogo wa Kayaba, mjini Kiteto.

Akizungumza na Tanzania Daima nje ya Hospitali ya Aga Khan, daktari wa Knight Support, Rosemary Temba aliyekuwa ameongozana na Kimesera tangu uwanja wa ndege wa JK Nyerere alisema alilazimika kumchoma sindano hiyo ya Tramadol, baada ya kumuona akilalamika kwa sauti ya juu.

Dereva wa gari la wagonjwa la kampuni hiyo alipoulizwa na Tanzania Daima sababu za kuendesha gari kwa taratibu sana na hivyo kumchukua dakika zipatazo 30 hadi kufika Aga Khan, alisema alikuwa akifanya hivyo baada ya kubaini kuwa kila alipokuwa akipita katika mabonde barabarani mgonjwa alikuwa akilalamikia maumivu makali.

"Nilikuwa natembea taratibu kutokana kumsikia mgonjwa akilalamika nyuma kwa maumivu makali. Unajua mimi naendesha kwa maelekezo ya daktari aliyekuwa na mgonjwa huyo, kwa sababu kila gari lilipopita kwenye mashimo alikuwa akilalamika kwa maumivu," alisema dereva wa gari hilo, Saidi Mussa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo na hatua watakazochukua, alisema ni mapema kufanya lolote kwa sasa kwani wangali wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa madaktari.

Mbowe aliwatoa hofu wananchi wa Kiteto na wanachama wa vyama vitano vya UDP, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na CUF kuwa watulivu na kuwahakikishia kampeni za nguvu na hatimaye ushindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge unaotarajia kufanyika Februari 24, mwaka huu.

"Ni mapema mno kuzungumzia hatua tutakazochukua kama chama… kwanza tunasubiri taarifa za madaktari ili kujua ukubwa wa tatizo hili, kama unavyoona ndiyo kwanza amefika hapa na uchunguzi umeanza.

"Katika siasa zipo mbinu mbalimbali zinazoweza kufanyika ili mgombea anayeonekana kuwa na nguvu ashindwe. Hatuwezi kamwe kutolihusisha hili na hujuma za kisiasa," alisema Mbowe na kuongeza kwamba rekodi ya mgombea huyo ni nzuri tangu mwaka 1995.

Alisema: "Rekodi ya Kimesera katika chaguzi za ubunge kuanzia mwaka 1995 ni nzuri… amekuwa akishinda kila wakati kwa zaidi ya asilimi 40, na hivi sasa vyama kama UDP, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na vingine vinatuunga mkono. Kwa sababu hiyo hatuwezi kurule out kuwa hizi ni hujuma za kisiasa."

"Hapo utaona ni kiasi gani tumeelekeza nguvu zetu katika jimbo hilo… hujuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa na kufanya tuikose Kiteto. Nawaomba Wanakiteto watulie, zipo timu zetu tatu za kampeni ambazo zitaendelea kufanya kampeni kama kawaida," alisisitiza Mbowe akiwa nje ya chumba alimokuwa akifanyiwa uchunguzi mgombea huyo.

Kuhusu gharama za kumhudumia mgombea huyo, Mbowe alisema CHADEMA hakijatoa fedha yoyote, badala yake amesafirishwa hadi Dar es Salaam kutokana na bima yake ambako ndege hiyo ya kukodi iligharimu sh 1,874,000 kutoka Kibaya hadi Dar es Salaam.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Benedict Losurutia kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana kutokana na maradhi ya figo.




 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom