CHADEMA Bado Elimu sio kigezo kikubwa kwa Ubunge?

majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
427
250

1) Godbless Jonathan Lema -- Diploma
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level,
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education,
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary,
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

Summary: Primary school...............2 credit 0.0625 x 2 =0.125
O level..........................5 credit 0.125 x2 =0.625
A level...........................1 credit 0.25 x1 =0.250
Diploma.........................2 credit 0.5 x2 =1.000
A Diploma.......................2 credit 0.8 x2 =1.600
Bachelor's degree............. 6 credit 1 x6 =6.000
Masters Degree................2 credit 2 x2 =4.000
PHD................................1 credit 3 x1 =3.000
Total Credit ..................................................= 16.6

Wastani wa credit = 16.6/24 =0.692,

Msitari mwekundu kwa Uongozi wa juu nchini kama Ubunge unatakiwa uwe juu ya Advance diploma, Hili la Ubunge kwa chadema ni kama vile Mheshimiwa slaa alivyotangaza Kirahisi kuhalalisha gongo kwa lengo la kuvuna kura za wanywa gongo eti atakuza uchumi kupitia watengeneza gongo na wanywaji! Kasahau kwamba gongo hata kama sio sumu ila inaweza kutengeneza genge la wavivu kufanya kazi, Hawajali taaluma na wanazidi kujitetea na kutangaza kwamba elimu sio kigezo cha lazima kwenye uongozi kwani wasomi wa ccm wamechemsha tangu Uhuru!.

Ukweli ni kwamba ukiondoa wabunge wasomi wachache wa chadema wengine ni wapiga kelele tu Bungeni wanafanya kuonekana tu kwamba wanaongea lakini ni wabunge wasio na mtazamo wambali wanaona mwisho wa pua zao tu.

Taifa zima linapaswa kuamua sasa Kukataa kuongozwa na waigizaji wa Darasa la saba, na lazima tusitumie maneno rahisi kujenga jamii isiyothamini elimu Kama tunavyoaminishwa na wanasiasa rahisi hawa ambao kwasasa wanaonekana kivutio kwa wasiosoma kama akina afande sere, JB, Ray, Mzeemajuto ambao lengo lao kusaka ubunge nikuongeza umaarufu wao ila hawana vission yeyote kwa Watanzania.

Bungeni sio sehemu ya kuenda kufanya sanaa, Bungeni sio kwenda Kuchekesha Bali nikuenda kuwawakilisha watu milioni karibia hamsini sasa ambao asilimia 80 wanaishi katika umasikini wakutupwa, acha mwanamziki afanye kazi ya mziki, muigizaji aigize, mchekeshaji achekeshe nasio kukimbilia mambo mazito ya kitaifa kwa umaarufu rahisi walionao.

Tujiulize swali Tunajenga Taifa gani kwa kuongoza na Darasa la 7 au wasanii?
Hivi mzee majuto anataka aende Bungeni Kufanya nini kama sio dharau kwa Bunge letu?
Mtu kama Lema au Sugu Ufahamu wake unaweza kulitoa taifa letu toka katika umasikini? au ndio tunazidi kuongeza migogoro katika jamii?

Tusitumie Kigezo rahisi Eti wasomi wameshindwa basi kilamtu awe kiongozi katika jamii, angalia ukweli Hivi mtu kama zitto au J Mnyika anaposimama bungeni unaweza kufananisha na sugu au Lema.

Taifa lolote lililoanza kupoteza Muelekeo linaanza kukumbatia wasio soma na wahuni kama akina lema na sugu na hii ni dalili mbaya Lazima Tujitambue na Tutambue athari za mfumo huu unaojongea Taratibu, Tusipokuwa makini Tutafanya kosakubwa sana kwa kuongozwa na Dicteta ambae kichwa chake ni sifuri kabisa.

Chadema Kama chama Mbadala talajali wa CCM, jitahidini kutujengea viongozi Bora, shawishini wasomi wagombee nafasi kubwa kama ubunge na msiangalie umaarufu wa mtu kwasababu baadaye mkipewa nchi mawaziri watabaki kunywa gongo, kuvuta bangi, kufanya maigizo, na kuimba bongo flever tu badala yakuwa serious kujenga Uchumi.

Wabunge ambao ni darasa la saba je wanajiendeleza kielimu au ndio wamebweteka wakijua chadema Hakuhitaji wasomi? au nadharia yenu ya kuogopa umaarufu wao ndio bado itawapa nafasi ya kugombea ubunge tena 2015?, Tuleteeni akina Mnyika, akina mdee, akina zitto wengi2015 nasio kutujazia watu waliokimbia umande eti wanaweza kwakuwa wapiga kelele wasiojua hata uelekeo.

Uchaguzi wa 2015 lazima Uwe uchaguzi utakaotuletea wasomi vijana wengi bungeni, Sugu, Lema, Majimarefu, Murugo, wote jiandaeni kugombea labda udiwani na hata baadhi yenu udiwani pia hauwafai gombeeni serikali za mtaa mwakani.
 
Sita Sita

JF-Expert Member
Aug 25, 2008
1,338
1,500
kuna soeech moja ya mwalimu nyerere alisema hatuwezi kuwa na wasomi katika TANU kwa kuwa TANU ingekuwa ni tabaka la wasomi ambao wangewaburuza wananchi. hivyo TANU ikabaki ni chama cha watu wasio na elimu ya juu na wale wenye elimu ya juu wakabaki serikali na kwenye kampuni binafsi kama waajiriwa.

mwalimu Nyerere alisema viongozi wa siasa wanatakiwa wafanane na wananchi wanaowaongoza. je unajua ni asilimia ngapi ya watanzania wana MSc, MA, MLB, MPhil na PhD? chama cha siasa hakiitaji wasomi bali viongozi bora na kuwa kiongozi bora huitaji PhD.
 
jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
1,195
Mleta hoja hujatenda haki kabisa , ungeweka vyama vyote , kuanzia hapo ndo tufanye ulinganifu, lakini pia napenda ukumbuke ya kuwa South Africa ina nguvu kubwa ya kiuchumi dunia kuliko hata mataifa ya Ulaya, Rais wake ni Jacob Zuma asiyeenda shule kabisa
 
Mwihadisa

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
608
195
Tuwekee hapa pia viwango vya elimu vya hawa hapa..1. Philip Augustino Mulugo 2. John Komba, 3. Deo Sanga "Jah People", 4. Aeshi Hillary, 5. Maji Marefu 6. Asnan Murji 7. Lameck Airo 8.Idd Azan 9. Wabunge wote wa CCM Zanzibar na 10.William Vangimembe Lukuvi 11. Emmanuel Nchimbi 12. Mary Michael Nagu 13. Modestus Kilufi n.k Na kabla ya hapo tuwekee CV yako hapa
 
majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
427
250
kuna soeech moja ya mwalimu nyerere alisema hatuwezi kuwa na wasomi katika TANU kwa kuwa TANU ingekuwa ni tabaka la wasomi ambao wangewaburuza wananchi. hivyo TANU ikabaki ni chama cha watu wasio na elimu ya juu na wale wenye elimu ya juu wakabaki serikali na kwenye kampuni binafsi kama waajiriwa.

mwalimu Nyerere alisema viongozi wa siasa wanatakiwa wafanane na wananchi wanaowaongoza. je unajua ni asilimia ngapi ya watanzania wana MSc, MA, MLB, MPhil na PhD? chama cha siasa hakiitaji wasomi bali viongozi bora na kuwa kiongozi bora huitaji PhD.

Kipindi unachoongelea wewe kilishapitwa na wakati sana brother, Hii ni karne ya 21, Tunahitaji wasomi vijana waelewa wa mambo, na wenye upeo mkubwa.
yerere aliweka wasio soma kwasababu dunia ya wakatihuo haikuwa kama sasa, sasahivi ukiweka watu wasiosoma tutaendelea kulizwa na baadae kujipooza eti wasiosoma wanafaa wakeup bro.

Ulishawahi kujiuliza ni kwanini nyerere hakuruhusu uvunaji wa ,aliasili kama madini wakati huo? sababu ni kwamba alikuwa akisubiri kipindi kama hiki ambapo uelewa wa watanzania utakuwa umepanda kitaaluma, tofauti nakipindi chake ambapo wote waliomzunguka walikuwa hawajasoma, ukiondoa wachache walio soma.

Hivi unaweza kupeleka waziri wa Darasa la saba kuamua mambo ya A mashariki pamoja na waziri mwenye degree wa Kenya? , practically unacceptable! shule lazima kwa wanasiasa.
 
gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
0
ordinary mind discuss people!poor you

kuna wakati wanaCDM wenzangu wanaudhi mpaka unataka kujitoa utu ili utukane......mtoa mada ana hoja ya msingi sana.
tena ameonsha ana machungu na CDM hivyo anatamani iwe na wabunge bora wengi zaidi kuliko maccm.
tatizo wafuasi waanza kutukana kisa mbowe na lema hawana sifa nzuri kwa mujibu wa thread, lakini mtoa hoja ametoa ushauri wa-update elimu zao ili kwenda na wakati.
hata mfano wake uko wazi kabisa, linganisha hoja za zito/mnyika/lisu vs mbowe/lema/sugu!

tusipotaka kukosolewa ili hatimaye tujitathmini, mabadiliko 2015 itakuwa ni doto.

NB: Hatuungi mkono ubaguzi wa kielimu, ila fursa zitolewe kulingana na sifa kwa kuwa hata asiye na sifa leo anaweza kuwa na sifa hizo kesho iikiwa ATATAKA kufanya hivyo!
 
Una hoja lakini pia nimegundua kuwa wewe sio mwanasiasa rjea kauli ya Nyerere kipindi hicho wasomi walikuwa wanahitajika sana lakini akawambia waachane na mambo ya TANU waende wakafanye kazi za kujenga taifa, maana yake si kweli kuwa siasa haitaji wasomi na pia si kweli kuwa ukiwa na wasomi wote ndo chama kitakuwa imara, kuwa mwanasiasa makini haitegemei tu elimu bali pia mbinu na ushawishi na mvuto wa kisiasa.

Wenzenu waliliona hilo ndo maana kwenye katiba ijayo impendekezwa kigezo cha elimu ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari na pia Mawaziri wasitokane na wabunge . Mbunge aweza kuwa mtu yoyote yule aliyekubalika na wananchi, kwa nini ujiulizi ilikuwaje hao waliochaguliwa iwe ccm, cdm, nncr au cuf , walipita na hali elimu zao ni ndogo ?

Kigezo kimependekezwa kwenye katiba mpya ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari, usishangae akitokea prof. akashindana na mwenye elimu ya sekondari kwenye siasa prof. anaweza asichaguliwe huyo mwenye elimu ya sekondari akachaguliwa
 
majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
427
250
Tuwekee hapa pia viwango vya elimu vya hawa hapa..1. Philip Augustino Mulugo 2. John Komba, 3. Deo Sanga "Jah People", 4. Aeshi Hillary, 5. Maji Marefu 6. Asnan Murji 7. Lameck Airo 8.Idd Azan 9. Wabunge wote wa CCM Zanzibar na 10.William Vangimembe Lukuvi 11. Emmanuel Nchimbi 12. Mary Michael Nagu 13. Modestus Kilufi n.k Na kabla ya hapo tuwekee CV yako hapa

Mkuu mimi sina lengo la kugombea cheo chochote chadema ila napenda chadema Kiwe mfano wa kweli na kionyeshe dalili zote za mabadiliko ya kweli ambayo tunayahubiri,

CCM wameisha shindwa muda mrefu katika hili, na dio maana wananchi wanataka mabadiliko, pamoja na kwamba ratio ya waliosoma na wasiosoma kama nilivyochambua kidogo hapo juu CCM wako juu kidogo, ila wasomi wa CCM wengi wametawaliwa na tamaa na ubinafsi.
 
majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
427
250
Una hoja lakini pia nimegundua kuwa wewe sio mwanasiasa rjea kauli ya Nyerere kipindi hicho wasomi walikuwa wanahitajika sana lakini akawambia waachane na mambo ya TANU waende wakafanye kazi za kujenga taifa, maana yake si kweli kuwa siasa haitaji wasomi na pia si kweli kuwa ukiwa na wasomi wote ndo chama kitakuwa imara, kuwa mwanasiasa makini haitegemei tu elimu bali pia mbinu na ushawishi na mvuto wa kisiasa.

Wenzenu waliliona hilo ndo maana kwenye katiba ijayo impendekezwa kigezo cha elimu ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari na pia Mawaziri wasitokane na wabunge . Mbunge aweza kuwa mtu yoyote yule aliyekubalika na wananchi, kwa nini ujiulizi ilikuwaje hao waliochaguliwa iwe ccm, cdm, nncr au cuf , walipita na hali elimu zao ni ndogo ?

Kigezo kimependekezwa kwenye katiba mpya ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari, usishangae akitokea prof. akashindana na mwenye elimu ya sekondari kwenye siasa prof. anaweza asichaguliwe huyo mwenye elimu ya sekondari akachaguliwa

hili linatokea katika level za wananchi wa chini na kwakuwa wameisha onyeshwa mfano na vyama, lakini elimu inaongeza upeo wa kuona mambo na kwa karne hii elimu kwa vijana wanasiasa itaongeza ufanisi wa taifa letu.

hivi hamuoni umakini wa vijana wasomi kama jj mnyika? ni nani kati ya hao darasa la anaeweza kufanana na kijana huyu makini?.
 
gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
0
kimsingi nakubaliana naww.
lakini pia nadhani sio sahihi kulinganisha umuhimu wa wasomi kipindi cha nyerere kwa kigezo cha kuwaambia watu waachane na TANU na kwamba waende wakafanye kazi kujenga taifa - hili inawezekana kabisa lilikuwa nisuala la kuangalia kipaumbele tu hasa kwa sabb idadi ya watu wakati huo haikuwa changamoto kubwa hivyo wasomi wachach waliokuwepo wangeweza kujipanga kuendesha nchi.
narudia, elimu ni muhimu - sanasana iende sambamba na hekima na busara ili kuepuka wasomi aina ya kapuya!
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000

1) Godbless Jonathan Lema -- Diploma
2) Antony Gervase Mbassa - - Adv diploma - KCMC
3) Prof Kulikoyela Kanalwanda Kahigi --- Phd
4) Freeman Aikaeli Mbowe – Form six
5) Highness Samsoni Kiwia ---- Secondary education – O level
6) Simon Peter Msigwa - -- O level,
7) Yohana Israel Natse --- Diploma in Education,
8) Halima James Mdee --- Degree, UDSM
9) Zitto Zuberi Kabwe --- Degree (economic) UDSM, Masters degree (MLB)
10) Silvester Mhoja Kasulumbay – Primary,
11) John Magale Shibuda --- O LEVEL
12) Joseph Osmund Mbilinyi --- Form IV
13) David Ernest Silinde --- Degree(BCOM), UDSM
14) Mustapha Boay Akunaay – Degree in law, Open University
15) Meshack Jeremiah Opulukwa --- Not updated
16) Philemon Ndesamburo --- Advanced diploma in Shipping
17) Said Amour Afri --- Primary school
18) Vicent Kiboko Nyerere -- O level
19) Ezekia Dibogo Wenje --- Degree, St Augustine
20) Joseph Roman Selasini --- Degree, UDSM
21) Tundu Antiphas Mughwai Lissu ___ LLM – Masters degree
22) John John Mnyika --- CV not updated
23) Salvatory Naluyaga Machemuli ___ Degree – DIT
24) Joshua Samwel Nassari – Not updated

Summary: Primary school...............2 credit 0.0625 x 2 =0.125
O level..........................5 credit 0.125 x2 =0.625
A level...........................1 credit 0.25 x1 =0.250
Diploma.........................2 credit 0.5 x2 =1.000
A Diploma.......................2 credit 0.8 x2 =1.600
Bachelor's degree............. 6 credit 1 x6 =6.000
Masters Degree................2 credit 2 x2 =4.000
PHD................................1 credit 3 x1 =3.000
Total Credit ..................................................= 16.6

Wastani wa credit = 16.6/24 =0.692,

Msitari mwekundu kwa Uongozi wa juu nchini kama Ubunge unatakiwa uwe juu ya Advance diploma, Hili la Ubunge kwa chadema ni kama vile Mheshimiwa slaa alivyotangaza Kirahisi kuhalalisha gongo kwa lengo la kuvuna kura za wanywa gongo eti atakuza uchumi kupitia watengeneza gongo na wanywaji! Kasahau kwamba gongo hata kama sio sumu ila inaweza kutengeneza genge la wavivu kufanya kazi, Hawajali taaluma na wanazidi kujitetea na kutangaza kwamba elimu sio kigezo cha lazima kwenye uongozi kwani wasomi wa ccm wamechemsha tangu Uhuru!.

Ukweli ni kwamba ukiondoa wabunge wasomi wachache wa chadema wengine ni wapiga kelele tu Bungeni wanafanya kuonekana tu kwamba wanaongea lakini ni wabunge wasio na mtazamo wambali wanaona mwisho wa pua zao tu.

Taifa zima linapaswa kuamua sasa Kukataa kuongozwa na waigizaji wa Darasa la saba, na lazima tusitumie maneno rahisi kujenga jamii isiyothamini elimu Kama tunavyoaminishwa na wanasiasa rahisi hawa ambao kwasasa wanaonekana kivutio kwa wasiosoma kama akina afande sere, JB, Ray, Mzeemajuto ambao lengo lao kusaka ubunge nikuongeza umaarufu wao ila hawana vission yeyote kwa Watanzania.

Bungeni sio sehemu ya kuenda kufanya sanaa, Bungeni sio kwenda Kuchekesha Bali nikuenda kuwawakilisha watu milioni karibia hamsini sasa ambao asilimia 80 wanaishi katika umasikini wakutupwa, acha mwanamziki afanye kazi ya mziki, muigizaji aigize, mchekeshaji achekeshe nasio kukimbilia mambo mazito ya kitaifa kwa umaarufu rahisi walionao.

Tujiulize swali Tunajenga Taifa gani kwa kuongoza na Darasa la 7 au wasanii?
Hivi mzee majuto anataka aende Bungeni Kufanya nini kama sio dharau kwa Bunge letu?
Mtu kama Lema au Sugu Ufahamu wake unaweza kulitoa taifa letu toka katika umasikini? au ndio tunazidi kuongeza migogoro katika jamii?

Tusitumie Kigezo rahisi Eti wasomi wameshindwa basi kilamtu awe kiongozi katika jamii, angalia ukweli Hivi mtu kama zitto au J Mnyika anaposimama bungeni unaweza kufananisha na sugu au Lema.

Taifa lolote lililoanza kupoteza Muelekeo linaanza kukumbatia wasio soma na wahuni kama akina lema na sugu na hii ni dalili mbaya Lazima Tujitambue na Tutambue athari za mfumo huu unaojongea Taratibu, Tusipokuwa makini Tutafanya kosakubwa sana kwa kuongozwa na Dicteta ambae kichwa chake ni sifuri kabisa.

Chadema Kama chama Mbadala talajali wa CCM, jitahidini kutujengea viongozi Bora, shawishini wasomi wagombee nafasi kubwa kama ubunge na msiangalie umaarufu wa mtu kwasababu baadaye mkipewa nchi mawaziri watabaki kunywa gongo, kuvuta bangi, kufanya maigizo, na kuimba bongo flever tu badala yakuwa serious kujenga Uchumi.

Wabunge ambao ni darasa la saba je wanajiendeleza kielimu au ndio wamebweteka wakijua chadema Hakuhitaji wasomi? au nadharia yenu ya kuogopa umaarufu wao ndio bado itawapa nafasi ya kugombea ubunge tena 2015?, Tuleteeni akina Mnyika, akina mdee, akina zitto wengi2015 nasio kutujazia watu waliokimbia umande eti wanaweza kwakuwa wapiga kelele wasiojua hata uelekeo.

Uchaguzi wa 2015 lazima Uwe uchaguzi utakaotuletea wasomi vijana wengi bungeni, Sugu, Lema, Majimarefu, Murugo, wote jiandaeni kugombea labda udiwani na hata baadhi yenu udiwani pia hauwafai gombeeni serikali za mtaa mwakani.

TUwekee ya kwako halafu nikuombe ujiunge na chadema lakini si kwa kigezo za phd za kubaka na kulawiti watoto yatima kama akina prof. Kapuya, Nchemba, Simbachawene
 
gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
0
Una hoja lakini pia nimegundua kuwa wewe sio mwanasiasa rjea kauli ya Nyerere kipindi hicho wasomi walikuwa wanahitajika sana lakini akawambia waachane na mambo ya TANU waende wakafanye kazi za kujenga taifa, maana yake si kweli kuwa siasa haitaji wasomi na pia si kweli kuwa ukiwa na wasomi wote ndo chama kitakuwa imara, kuwa mwanasiasa makini haitegemei tu elimu bali pia mbinu na ushawishi na mvuto wa kisiasa.

Wenzenu waliliona hilo ndo maana kwenye katiba ijayo impendekezwa kigezo cha elimu ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari na pia Mawaziri wasitokane na wabunge . Mbunge aweza kuwa mtu yoyote yule aliyekubalika na wananchi, kwa nini ujiulizi ilikuwaje hao waliochaguliwa iwe ccm, cdm, nncr au cuf , walipita na hali elimu zao ni ndogo ?

Kigezo kimependekezwa kwenye katiba mpya ili mtu awe mbunge angalau awe na elimu ya sekondari, usishangae akitokea prof. akashindana na mwenye elimu ya sekondari kwenye siasa prof. anaweza asichaguliwe huyo mwenye elimu ya sekondari akachaguliwa

kimsingi nakubaliana naww mkuu.
lakini pia nadhani sio sahihi kulinganisha umuhimu wa wasomi kipindi cha nyerere kwa kigezo cha kuwaambia watu waachane na TANU na kwamba waende wakafanye kazi kujenga taifa - hili inawezekana kabisa lilikuwa nisuala la kuangalia kipaumbele tu hasa kwa sabb idadi ya watu wakati huo haikuwa changamoto kubwa hivyo wasomi wachach waliokuwepo wangeweza kujipanga kuendesha nchi.
narudia, elimu ni muhimu - sanasana iende sambamba na hekima na busara ili kuepuka wasomi aina ya kapuya!
 
gastone

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
329
0
TUwekee ya kwako halafu nikuombe ujiunge na chadema lakini si kwa kigezo za phd za kubaka na kulawiti watoto yatima kama akina prof. Kapuya, Nchemba, Simbachawene

kamanda najua umeguswa hasa kwa sabb lema 'ameguswa' - lakini hoja hii ni ya msingi sana hivyo tujifunze kuvumiliana.
hatuzungumzii maccm hapa - tunazungumzia chadema!
 
majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
427
250
TUwekee ya kwako halafu nikuombe ujiunge na chadema lakini si kwa kigezo za phd za kubaka na kulawiti watoto yatima kama akina prof. Kapuya, Nchemba, Simbachawene

kigezo sio kwa hao wasomi wasiojitambua kama hao ulivyowataja. ila wapo vijana wasomi wachache ambao wamekuwa mfano thabiti wakutofautishia waliosoma na ambao hawajasoma katika kuleta maendeleo yakweli na kujenga hoja.

hivi ukiondo mnyika, tundulisu, zitto, mdee, utabakia na nani smart bungeni? hawa wengine wapiga kelele tu bungeni, Huo ndio ukweli wachache sana ambao angalau pamoja na elimu zao ndogo wanajitahidi mfano mbowe pekee.
 
Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,892
2,000
Unadhani ndio maana wanan'gan'gania serikali tatu badala ya kuangalia matatizo yanayowakabili wananchi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom