Chadema badilisheni mtazamo; kuvua gamba si lazima uiache CCM au chama chako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema badilisheni mtazamo; kuvua gamba si lazima uiache CCM au chama chako

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Sep 5, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,323
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Ningependa sana kuwasihi Chadema kuufanyia mabadiliko mtazamo wa vua gamba; isiwe lazima watu waache vyama vyao. Chadema tafuteni kukubalika ndani ya vyama vingine, CCM, CUF, NCCR, TLP nk, ili watu wawaunge mkono wakiwa ndani ya vyama vyao na kwamba si lazima wajiunge na Chadema ili kuiunga mkono Chadema. Onyesheni kwamba hamuichukii CCM kama taasisi, bali utendaji wa CCM kama chama tawala kinachoongozwa na watu wenye ubinafsi wa kupindukia. Waonyesheni wana CCM kwamba kuiunga mkono Chadema ni namna mojawapo ya wao kuonyesha wanataka mabadiliko yafanyike ndani ya Chama chao CCM.

  Na pia Chadema mjue kwamba si watu wote wanaowaunga mkono wanataka kuwa wanachama wa Chadema. Kumbukeni haitaleta maana kwamba kila mmoja nchini Tanzania awe mwanachama wa Chadema.
   
 2. m

  mikumoso Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Nakuunga mkono mkuu!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Unategemea mt afanye nini pale ambapo GAMBA KATIKA CCM haupo tu katika sura za watu ndani chama hicho bali ni GAMBA AMBALO NI SARATANI YA KIMFUMO mzima usioweza kuondolewa??????????
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20 ibara ya 21
  21.-(1) Afisa polisi au mtu mwingine hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kutumia nguvu zaidi au kuvunja utu wa mtu huyo zaidi ya ilivyo lazima kufanikisha ukamataji au kumzuia utorokaji wa mtu baada ya kukamatwa.
  (2) Bila kupunguza matumizi ya kifungu kidogo cha (1), afisa polisi hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kufanya kitendo kinachoweza kusababisha kifo kwa mtu huyo, isipokuwa kama afisa polisi anaamini kwa sababu za msingi kwamba kufanya kitendo hicho ni muhimu katika kulinda maisha au kuzuia madhara makubwa kwa mtu mwingine.


  Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 4 ibara ya 18B.-
  (1) Katika kutumia haki ya kujilinda mwenyewe au kumtetea mtu mwingine au kutetea mali, mtu atatakiwa tu kutumia nguvu za kiasi zinazostahili ulinzi husika.

  (2) Mtu atawajibika kuwa ametenda kosa la jinai kwa kosa lolote litakalotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda au anapomlinda mtu mwingine au anapolinda mali.
  (3) Mtu yeyote atakayesababisha kifo cha mtu mwingine kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda, anakuwa ametenda kosa la kuua bila kukusudia.
   
 5. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  100% nimepitisha
   
 6. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tanzania haina sheria. Viongozi ndio wa kwanza kuidhulumu sheria kwa kuchakachua, kuuwa, kuonea, na mengine. Polisi ambao ni law enforcement ni wa kwanza kuvunja sheria kwa kuuwa, kuonea, kusingizia, kurent silaha kwa majambazi, kubambikizia watu makesi ili wapate rushwa, nk.
  Je kama haya yanafanyika ni nani anafikiria sheria? Na kama kuna sheria ni kwa mnyonge pekee yule ambaye hana hongo ya kutosheleza tumbo la mapolisi. Sasa hizo sheria zina maana gani? Si afadhali zifutwe?
  Kiongozi anapaswa aongoze sii kwa maneno tu bali kwa matendo. Viongozi wetu wanafanya nini? Kweli ndugu tumebaki kuwa taifa la aibu. Hiyo iko wazi, na sheria ziliondoka na Nyerere ile siku alipozikwa. Viongozi waliobakia wanatembea uchi mbele za watu bila hata aiabu yeyote ile. Sasa tuwaze sheria kama hata utu umetutoka?
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,323
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa umenichanganya kidogo kuhusana na mada inayajadiliwa
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kwani ni lazima ujiunge na chadema?????
  Ushauri wako hauna mashiko.
   
 10. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,323
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mie naangalia maslahi ya Watanzania kwa ujumla. Ushindi wa Chadema hauko katika kuisambaratisha CCM isiwepo tena. Hilo litakuwa pigo kwa demokrasia yetu nchini. Uongozi wa CCM wa sasa haufai kabisa, ndio maana watu wengi nchini wanataka mabadiliko, kwamba taasisi yenye watu wenye uzalendo na uchungu na maendeleo ya nchi yetu ishike hatamu za uongozi wa nchi. Na wengi wanaona kwamba Chadema inazidi kuudhihirishia umma kwamba wako tayari kushika hatamu za uongozi wa Tanzania.

  Hata hivyo, kama ambavyo tu wakati fulani hili CCM ilikuwa nzuri tu, na baadaye ikabadilika kuwa dudu la ajabu, hatuna uhakika kwamba Chadema ya leo ndio itakuwa Chadema ya kesho. Nini kitatokea wakati kina Slaa, Lissu nk hawapo tena katika uongozi wa Chadema? Bila shaka hata leo hii ndani ya Chadema wapo watu ambao nia zao zinatiliwa shaka; wanaonekana wanataka maslahi yao binafsi badala ya maslahi ya wananchi . Vipi hawa watu wakija kuwa wakuu wa Chadema baadaye?

  Kwa hiyo ndio maana tunataka CCM ibaki kama taasisi, kwa sababu inawezekana kabisa Chadema wakajisahau hapo baadaye na kulewa madaraka, kosa ambalo CCM wamelifanya. Hapo tena, itakuwa wakati muafaka wa wananchi kusema Chadema kaa kando ukajipange upya, na CCM au (taasisi nyingine mbadala) irudi tena, kama imerekebisha makosa yake. Kwa sasa CCM inabidi ikae kando kwa kuwa haikidhi tena mahitaji ya wananchi wala ya wanachama wake walio wengi. Wakae kando wakajipange upya, na wakiwa katika kujipanga upya taasisi mbadala iliyopo ni Chadema.
   
 11. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,323
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Baharini kuna samaki wa aina nyingi, wengine hawafai kuliwa japo hawana madhara, na wengine hawafai kabisa kuliwa kwa kuwa wana sumu.
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Huwezi kumlazimisha mtu awe na mawazo kama yako vinginevyo apende yeye na ndo chadema wanachofanya, hawawalazimishi cuf, nccr au tlp kuwa na mawazo yao
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60  Mkuu nimekupata vizuri. Ila nionavyo mie ni bora kwa sasa tukahakikisha tunapata mabadiliko ya uongozi wa kisiasa Tanzania. hii ndo itakuwa njia pekee ya kuvifanya vyama vya siasa viwaheshimu watanzania. ccm haiwaheshimu tena wananchi, imeshajibadilisha na kuwa zimwi la ajabu sana. mimi naamini, watanzania wakiitoa ccm madarakani, hata CHADEMA watajua kuwa wamepewa madaraka ili watimize mahitaji ya wananchi kwa mujibu wa sheria. KIKUBWA KWA SASA, TUJITAHIDI TUIONDOE ccm MADARAKANI, ILI WANASIASA WAJIFUNZE KUWATUMIKIA WANANCHI, NA SIO KUWAKANDAMIZA WANANCHI KAMA INAVYOFANYWA NA HAWA WAUAJI ccm KWA SASA.


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waling'oe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wazo lisilokamilika kama hili lako kamwe haliwezi kwa peke yake bila mtoa wazo kujikuta analazimika tena sana kwenda hatua ndefu kutafuta walau mafiga matatu au manne hivi kujaribu kuimarishia hisia binasi ili hisia hizo walau zipate kusimama japo hata kwa sekunde 30 tu kuonekana ni mantiki kitu vile.

  Hata hivyo, Mwana-JF mwenzangu nachagua kukutetea hadi tone la mwisho katika hii dhania yako watu tukuruhusu haki yako ya kuitandarua hapa ukutani ila mwisho wa yote ni kwamba CCM must go!!!!!!!!!!
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Very powerful and relevant speech by Mbowe. Thanks for the reference which should refute current and future similar propaganda as the thread goes.
   
Loading...