CHADEMA baada ya miaka 28 hatimaye leo imekufa rasmi

FAHAD KING

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
301
373
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "

Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA

Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.

Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana

Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama

Alamsiki
 
Hivi huwa mnashabikia nini kwenye siasa mbona Mimi huo mzuka sinaga yani kama vile mpira
Unashindwa kula kisa upumbavu wa mtu mwingine?? Hii ishu ikoje??
Yaan ufanye ujinga wako mimi niumie??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Siasa haihitaji kushabikiwa. Una mawazo potofu kabisa. Siasa inahitaji kusimamiwa ili haki itendeke. Kila raia anawajibu huo. Kumbuka: Sio kushabikia bali kusimamiwa.
 
Hivi huwa mnashabikia nini kwenye siasa mbona Mimi huo mzuka sinaga yani kama vile mpira
Unashindwa kula kisa upumbavu wa mtu mwingine?? Hii ishu ikoje??
Yaan ufanye ujinga wako mimi niumie?
Mkuu uko kama miye. Na mijitu mingine mpaka inauliwa ikiwa mbele kwenye maandamano. Ukiiuliza unapigania nini hasa hata haijui. Halafu kesho na kesho kutwa hao hao unaowapigania mpaka kuhatarisha maisha yako unawakuta wako pamoja wanafakamia keki ya taifa. Utopolo mtupu na kamwe sitakaa nishabikie mwanasiasa !
 
Back
Top Bottom