FAHAD KING
JF-Expert Member
- Sep 14, 2017
- 301
- 373
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "
Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA
Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.
Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana
Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama
Alamsiki