CHADEMA ARUSHA WAIGOMEA POLISI - Mkuu wa wilaya na mpango wa Kufunga uwanja wa NMC leo jioni

Kwa nini ufungaji wa maeneo ya wazi yaendane na utoaji humuku kwenye kesi ya Mhe Lema jijini Arusha??????????

Ni kitu gani hiki kama si uchokozi wa wazi kwa umma wa Tanzania??.?????? Nadhani sasa kila mtu anaona jinsi gani serikali ya CCM inavyojibidisha kutengeneza mazingira mapya ya kupata sababu ya KUUA TENA RAIA WA NCHI HII?

kamanda wa mkoa(RPC) akiuwa anapandishwa cheo kwenda makao makuu,eg RPC Kamuhanda anaandaliwa nafasi pale makao makuu,source majira newspaper
 
Nashauri kesho iwe siku ya kwanza kwa polisi nao kupoteza wenzao kikatili hapa arusha maana hawatajifunza thamani ya damu ya raia mpaka waonyeshwe jjazba iliovuka mipaka ya raia wa tz maana ni bora kufa kuliko kuwa chini ya uatwala Ccm na polisi mbona babu zetu mpaka mkoloni mweupe akaondoka itakuwa hawa wakoloni weusi ka mi..ndu ya nyani bwanaaa potelea mbali mimi nipo NMC tangu asubuhi ya kesho siogoopii bunduki risasi maji washa wala kufa poteleambali
 
Unaweza kuufunga uwanja wa NMC lakini uwezi kuzifunga fikra za watu juu ya CDM,hii nisawa na kumpigia mbuzi gitaa na sijui nani anayebuni mbinu DHAIFU a.k.a GO-I-GO-I a.k.a.a.a.a LEGELEGE
 
Jamani ccm! Anakuja hatia kuna hatia gani watu kukutana? Mkizuia mikutano leo hamtaizuia milele. Freedom is comming today
 
Hivi tulitokaga wapi na jeikei jamaniiiiiiiiiiiiiiiiii???? Mbona ni matatizo makubwa!!!
 
Wewe Meya wa kuchonga, Lyimo, damu ikimwagika Arusha safari hii na wewe ujiandae kabisa kuhama huo mji.

Ni maamuzi gani hayo ya kufunga eneo la wazi ambako hata baba yako mzazi alipata kuchezea akiwa kijana mdogo hapo Arusha????????????????
 
Hivi tulitokaga wapi na jeikei jamaniiiiiiiiiiiiiiiiii???? Mbona ni matatizo makubwa!!!

Raisi dhaifu tangu tupte uhuru wa bendera, na atakayesahaulika haraka na wananchi na hakutakuwa na mtu wa kumkumbuka kwa lolote aliloifanyia nchi hii.

Raisi gani kiguu na njia kila siku kwenda ulaya na marekani hata hajui majukumu aliyokabidhiwa kwa wananchi wake.
 
Magamba bwana wamechooooooooka. Hawana wabunge wa kufanya mikutano ya hadhara na wao? Mbona kazi ni kuweka kiwingu tu kwa wenzao?
 
Jamani nauliza tena..hizi tetesi zimethibitishwa??!
Na tetesi zenyewe zinasema ywanja utafungwa usiku...wabongo bana....haya endeleeni kujadili na kutukana na kupandisha jazba...
 
Nafurai ccm inavyohangaishwa, hii inamaanisha mwisho wake umekaribia.!
 
Kabla ya Kifo cha David Mwangosi kule Iringa kuna Thread nilianzisha ya tahadhari. Sijawahi kuiona. Mauaji yalifanyika. Leo nakaa kimya.
 
mbona ghafla namna hiyo au kwa sababu wamesikia ujio wa CUF ARUSHA?
Ujio wa CUF ndo una nini? Hata CUF wakiwa wanaenda kufanya mkutano Arusha sidhani kama huo mkutano wao utakuwa na effects zozote kwa Chadema sababu Chadema anahangaika na CCM(ambaye ni mume ktk ile ndoa ya Zenji) na co CUF(mke wa CCM).
 
Arusha wiki hii kuna tukio moja kubwa na lenye kuvuta sana hisia za wakaazi hapo; Hukumu ya Rufaa ya Kesi ya Mh; Lema.

Maoni yangu ni kuwa kufanya mkutano saa 24 kabla ya hukumu (kesho kutwa alhamisi) hilo naona halijakaa vizuri. Kufanya rally siku moja kabla ya hukumu inaweza ikaonekana ni kama kutaka kujenga mazingira fulani (siege mentality). Nawaomba makamnda wetu wakuu Mh; Mbowe, Dr. Slaa, Mh: Mnyika na wengine waangalie kwa busara. Nikijaribu kutumia common sense yangu ndogo, naona ni vema kuahirisha mkutano wa jumatano pengine hadi wiki ijayo. Kwa kufanya hivyo naamini hilo litaepusha kuwapa Magamba na polisi wao sababu zozote za kufanya uovu wao, maana upo ila wanasubiri condusive environment tu.

Kwa upande wa pili, kama hakuna hukumu ya rufaa ya Mh. Lema wiki hii basi si busara wala haki hata kidogo kwa Polisi kuizuia CHADEMA kufanya shughuli zake halali na za kikatiba za kisiasa. Kwa hiyo OCD, Meya, RC na mamlaka yoyote hapo Arusha isijaribu kutengeneza maafa kwa kuzuia mkutano huo kwa sababu zozote zile.

Hoja ya Polisi ya suala la mtihani wa darasa la saba ni hoja dhaifu kuliko zote nilizopata sikia. Kwani wananfunzi na wasimamizi wao si watakuwa kwenye vyumba vya mitihani? Kadhalika kama niliuona ule uwanja vizuri nadhani shule zilizopo karibu ni 2 na zote mbili ni za sekondari.
Hata mimi nakuunga mkono mkuu, magamba wanaweza kutumia mwanya huu kuathiri maamuzi ya kesi ya tarehe 20.
 
Inasemekana baada ya njia
zote za kudhibiti mkutano wa CHADEMA hapo kesho kushindikana, mkuu wa
wilaya ya Arusha mjini na meya wa CCM Gaudence Lyimo wamekutana na
kuweka mkakati wa kuufunga uwanja wa NMC leo usiku ili kuthibiti dhamira
ya CHADEMA ya kufanya mkutano huo.

Katika mpango huo, OCD ametakiwa kuwaandikia CHADEMA barua nyingine
yenye sababu nyingine kuwa uwanja umefungwa ili wamachinga waweze
kuhamia baada ya sababu ya awali kukataliwa na CHADEMA kuwa hawaruhusiwi
kufanya mkutano kwa sababu darasa la saba wanafanya mtihani.

Jambo hili limenung'unikiwa na madiwani wote wakiwemo wa CCM kuwa
maamuzi haya hayakuwa yamefikiwa hitimisho la kuufunga uwanja wa NMC
(open space) na kuwa masihara haya na kukiwinda CHADEMA kisifanye
mikutano ndicho chanzo cha mabalaa mengi hapa mjini.

Ndo msing'ang'anie kwenda huko kubishana na dola halafu yakitokea maafa muwalaumu polisi wakati bado mna muda mzuri kuamua kutokwenda huko.
 
Back
Top Bottom