CHADEMA Arusha ‘’kwafuka moshi’’; Godbless Lema aambiwa hajitambui na hajui majukumu yake

Bajeti ya halmashauri imepitishwa wabunge hawahudhurii. Muda mwingi hawaonekani kwenye vikao wala kukaa ofisini, watajuaje matatizo ya wananchi? Lipo tatizo la kutatua bila kuangaliana usoni. Mnyika ana kazi kubwa sana, nina wasiwasi kama atavumilia huu ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama Mnyika ataweza kuleta suluhu kwenye mtifuano unaoendelea Arusha na Moshi!

Chama kinapaswa kupata watu ambao hawako kwenye makundi ndani ya chama ili kutatua mtifuano huu.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ana kundi lake ambalo mmojawapo ni Lema!

Tatizo haliwezi kutatuliwa na walioleta tatizo!
 
Mkuu nadhani ni bora kusikiliza hoja ya huyu Diwani na kuifanyia kazi. Watu wanaona ingawa viongozi wanaweka earphone zenye Muziki mnene wakati Miwani yao ni ya Mbao
Alisema anaunga juhudi mkono,siku anaondoka,huko alipokwenda anajua kwamba,unahitajika mkopo wa kujenga matundo ya choo,na kwamba sisi sio donor country kama ilivyokuwa inasemwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diwani kaongea point Sana badala ya CHADEMA kujikita na mambo ya CCM ni vizuri wakijikita zaidi na mambo yao ya chama maana jahazi aliendi vizuri kabisa.Uzi Kama Huu uwezi ukakuta wanachama au wapenzi wengi wa CHADEMA wakijadili tatizo siasa zetu zinaongozwa na mahaba kuliko ukweli.
Kutojadili Uzi haiwezi kubadilisha ukweli au hali halisi ya mtifuano unaoendelea ndani ya chama chao!

Zamani walikuwa wanajificha kwenye dhana ya ''WANANUNULIWA'' lakini kwa sasa ukweli umeanza kuchomoza!

Ukweli umeanza kubainisha kuwa Arusha na Moshi kunafukuta moshi wa mapambano ndani ya CHADEMA!
 
Huyo diwani kama kweli anayaona matatizo ndio awe wa kwanza kufanya juhudi za kuyatatua, anasema lazima wakae kama chama sasa mbona sio kakimbilia kurekodiwa kwa video analalamika, hayo angetakiwa ayasemew kwenye vikao, huyu diwani nae ni dhaifu tu km waliokimbia CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani humfahamu vizuri Diwani Isaya Doita!
 
Sorry i mean mwanama boss,wananchi naona wanasema watamsusia bidhaa zake.

dodge
Naomba nikupe muendelezo.

Leo Mheshimiwa dalali wa TISS CCM nje ya TISS mfumo amekaa na huyo diwani na akina Bananga na wengine nane ili watangaze kuunga juhudi.
Sisi wapiga kura tuna habari sahihi ya kila dakika kwa wakati.
Wajue badala ya kumbomoa Lema wamemjenga mara dufu. Na sisi wananchi tumeelewa vizuri kuwa kodi zetu halmashauri zinaendelea kutumika ndivyo sivyo na maccm.
 
Aisee ai mchezo,Bananga siku hizi simuelewi elewi. Hivi na yeye yuko ktk wanaotaka kuunga mkono juhudi?
Naomba nikupe muendelezo.

Leo Mheshimiwa dalali wa TISS CCM nje ya TISS mfumo amekaa na huyo diwani na akina Bananga na wengine nane ili watangaze kuunga juhudi.
Sisi wapiga kura tuna habari sahihi ya kila dakika kwa wakati.
Wajue badala ya kumbomoa Lema wamemjenga mara dufu. Na sisi wananchi tumeelewa vizuri kuwa kodi zetu halmashauri zinaendelea kutumika ndivyo sivyo na maccm.

dodge
 
Diwani wa Kata ya Ngarenaro kwa tiketi ya CHADEMA, Isaya Doita amemtuhumu Godbless Lema kuwa hajui kazi na majukumu yake kama kiongozi wa juu wa CHADEMA na pia kama Mbunge.

Isaya Doita ametoa tuhuma hizi baada ya CHADEMA kupoteza Madiwani 3 pamoja na Katibu wa CHADEMA katika Jiji la Arusha. Mpaka sasa CHADEMA katika Jiji la Arusha imepoteza Madiwani 12 ambao wamejiunga CCM.

‘’Kuna tatizo nadhani viongozi wetu wa chama wilaya,mkoa, Kanda na hata taifa wanapaswa kukaa chini na kujiuliza ni nini kinaendelea Arusha’’, Isaya Doita alisema.

Ameendelea kusema, ‘’Badala ya viongozi kutoa matusi na kuwakashifu kwenye mitandao wanaohama, ni wakati sasa tujitathmini ili kujua tatizo liko wapi na njia gani zitumike ili kuzuia hali hii. Tatizo linalotusumbua CHADEMA ni kutoambiana ukweli na kama tutaendelea hivi na kutojitambua basi kuna uwezekano nafasi za madiwani na Mbunge tulizoshinda zikafutika katika Jiji la Arusha kwenye Uchaguzi ujao’’.

‘’Shida ninayoiona kwa sasa hapa Arusha tumekuwa kama familia ambayo imekosa mtu wa kutuunganisha pamoja. CHADEMA hatuna kiunganishi kizuri kati ya Mkoa na Kanda. Mwenyekiti wa Kanda, Godbless Lema lazima arudi hapa Arusha na akae na wanaCHADEMA na athamini uwepo wa wanaCHADEMA/viongozi wengine’’ Isaya Doita Alisema.

Alimalizia kwa kusema, ‘’Sitaki kuwa muongo na mnafiki, Wabunge wetu katika Jimbo la Arusha Mjini hawana impact, hawajawahi kugusa maisha ya Wananchi wa Arusha. Kuna tatizo katika ubunge wetu, hata wale wa Viti maalum. Mbunge Lema, Joyce Mukya na Catheline Magige siwaoni hapa Arusha.

Nadhani wanadhani Ubunge ni kwenda tu Bungeni na kusaini posho na kurudi. Leo ukiwauliza kuna shule ngapi na vituo vya afya vingapi na maendeleo yake hawajui. Tuna wabunge ambao hawajitambui na hawajui wajibu wao. Kwa mantiki hii ni bora kuchagua Mbunge yoyote anayejitambua na kujua majukumu yake bila kujali anatoka chama gani''.

Video ya alichokisema Diwani Isaya Doita.
moshi kama huo unanikumbusha kipindi Lowassa anazunguka na yale mabasi yake akiwa na kampani nzima ya wana kaskazini wenzake
 
Hilo Jimbo linachukuliwa na LEMA anajua sasa cha kujisumbua ni nini, mwache ale hela zake za Ubunge pole pole
 
Mkuu, hivi Diwani ana mamlaka kweli ya kuitisha kikao cha chama? Nadhani kwa hili utakua umemuonea. Viongozi wa kanda na Mkoa kama alivyoshauri ndiyo wanawajibika kuitisha hivyo vikao vya maridhiano. Kukimbilia kurekodiwa ni sehemu tu ya kutoa maoni yake kwasisi ambao tunahitaji kujua Arusha kulikoni? Mbona madiwani wanahama?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
diwani akayasemee hayo kwenye vikao vya chama, sio kuitisha kikao au kutengeneza video!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutojadili Uzi haiwezi kubadilisha ukweli au hali halisi ya mtifuano unaoendelea ndani ya chama chao!

Zamani walikuwa wanajificha kwenye dhana ya ''WANANUNULIWA'' lakini kwa sasa ukweli umeanza kuchomoza!

Ukweli umeanza kubainisha kuwa Arusha na Moshi kunafukuta moshi wa mapambano ndani ya CHADEMA!
Unashangilia kweli, kwa taarifa yako mgogoro unaousema CDM haupo, unajiliwaza tu hapa, na hao wabunge uliowataja nyendo zao zinafahamika kitambo, sijui mtaendelea kujipa moyo CDM inakufa mpk lini!, mlianza toka 2010 km sijakosea, mpk leo bado mnaota tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom