CHADEMA ANGALIENI HILI KWA JICHO LA TAI (tai aliweza tizama/ona leo kabla ya jana!)

Kilimo

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
777
192
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ndani ya CDM kuna mapandikizi ambao kiukweli ni mamluki wa CCM, hivi itakuwaje 2015 kabla tu ya uchaguzi ambapo baadhi ya viongozi/kiongozi wa CDM watajiondoa/atajiondoa ilimradi akidhoofishe CDM ktk uchaguzi hasa uchaguzi wa rais, hivi ni taadhari gani inapaswa kuchukuliwa ndani ya CDM?? kwa wale wapenda mabadiliko toeni mapendekezo yenu ili yasaidie vyama vyote vya upinzani kwa mustakabali wa nchi yetu (hii ni casestudy kwa CDM ili isaidie na kwa vyama vingine vya upinzani)
 
Hapo kwenye undelined red; Mkuu hivyo vyama viko vingapi Tz? Tafadhali rekebisha maelezo yako yasomeke "chama cha upinzani".
 
Hapo kwenye undelined red; Mkuu hivyo vyama viko vingapi Tz? Tafadhali rekebisha maelezo yako yasomeke "chama cha upinzani".

halo dudus, vyama vya upinzani vipo vingi tanzania, kama CUF, NCCR-mageuzi, TADEA, ADC, UMD, CHADEMA NA VINGINEVYO.
 
Mamluki ni yupi mkuu Yule anayetangaza nia ya kugombea kupitia chama chake.Au Yule anayemwogopa kiongozi wa chama hata kama ametoa maamuzi ya kumshirikisha mchumba wake ndani ya chama.Nafurahi jibu umepata
 
halo dudus, vyama vya upinzani vipo vingi tanzania, kama CUF, NCCR-mageuzi, TADEA, ADC, UMD, CHADEMA NA VINGINEVYO.

Chama cha upinzani ni kimoja tu angalia wekundu hapo juu. Vingine hivyo ulivyvitaja ni mawakala wa Magamba
 
Mamluki ni yupi mkuu Yule anayetangaza nia ya kugombea kupitia chama chake.Au Yule anayemwogopa kiongozi wa chama hata kama ametoa maamuzi ya kumshirikisha mchumba wake ndani ya chama.Nafurahi jibu umepata

Nimekusoma awadhi2009, ni hivi, mamluki ni yule atakayejiondoa ktk chama na kwenda sehemu nyigine purposely for weakening his/her previous party in our coming, 2015, country's general election for his/her unilateral interests. Kwa mtu anayetangaza nia siyo mamluki vile akipata au akikosa kwenye hiyo nia yake hawezi kuondoka ktk chama kwa lengo la kukidhoofisha.
 
Ndugu zangu, watanzania wengi tumechoka sana na wizi wa CCM ambao kwa sasa Taifa limedhoofu lakini bado kuna watanzania wanaochekelea huki watoto wao wakishindwa kusoma na hata wengine kupoteza maisha ndani ya hospitali ambazo hazina dawa!!!!!
 
CDM ijipange kuhakikisha nyadhifa ilizonazo hazipotei. Namaanisha nafasi za ubunge, udiwani, uwenyekiti serikali za mitaa, umeya nk. Hili lishaanza kuonyesha dalili mbaya baada ya kupoteza umeya Mwanza.

Wasiwasi wangu ni kuwa CDM inapigana vita hii blindly na hakuna mabadiliko yatakayotokea 2015 hali ikiendelea hivi.

Ushauri wangu ni kuwa CDM itengeneze intelligence unit (kama haipo) ambayo ni imara itakayoweza kuwafichua vipandikizi wa MAGAMBA na kuwatupa nje ya ulingo bila aibu. Aidha itasaidia kuiga au kubuni mikakati madhubuti itakayoweza kuwashawishi waTZ wengi kuliko ilivyo sasa ambapo inaonekana kama tayari CDM ishakuwa na wafuasi wengi lakini kumbe ni kama wanavokwenda kumshabikia mwanamuziki Diamond halafu wanaonunua kopi halisi ni 0.0001%
 
Watanzania ngoja niwape fact naamini kabisa kama kuna mapandikizi ya magamba ndani ya CDM wako wachache na hawana nguvu ya kukiyumbisha wala kukipotezea umaarufu na kasi yake katika kuleta mabadiliko katika nchi hii na endapo kuna pandikizi mmoja atatoka maelfu ya watu watajiunga
 
Kwa kuwa haya ni mapambano, CDM wasitegemee kupewa haki katika kikombe cha chai.

Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha mnajipanga kimkakati kwa njia mbalimbali, hata ikibidi kuweka mapandikizi yenu pia katika magamba.

Hakuna tena muda wa kupoteza kwa kulia lia.
 
Back
Top Bottom