Chadema ajiri makatibu wa mikoa na wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema ajiri makatibu wa mikoa na wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FreedomTZ, Oct 30, 2012.

 1. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Katika uchaguzi wa udiwani kata 29 ulifanyika hivi karibuni CHADEMA imeambulia viti 5 kati ya 29. Pamoja na kwamba chama hiki kimepata kata mpya 3, bado kazi ya ziada inahitajika ili kiweze kupata ridhaa ya kuongoza nchi ifikapo mwaka 2015 kama ambavyo watu wengi wapenda mabadiliko ya uongozi tunavyotaka. Ili kufikia malengo ya kushika dola ni muhimu CHADEMA ifanye tathmini ya kina na kuchukua hatua madhubuti. Nafikiri chama kinahitaji kuwa na mfumo wa utendaji/uongozi wa mikoa na wilaya ambao wameajiriwa; namaanisha chama kiajiri au kiwalipe mshahara makatibu wa mikoa na wilaya. Kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa na watendaji wasomi ambao kazi yao kubwa itakuwa ni kusimamia utendaji kazi wa chama wa siku hadi siku na kubuni njia bora za kujenga na kuimarisha chama katika maeneo yao ya kazi.

  Nafikiri kwa sasa chama kinaweza kupata fedha za kuajiri makatibu wa mikoa na wilaya zote Tanzania ili kuimarisha mtandao wa chama. Kazi ya kujenga na kuimarisha chama isitegemee viongozi wa makao makuu tu. Haya ni mawazo yangu yenye nia ya kuona mwaka 2015 serikali inaongozwa na Chama makini chenye watu makini wanaojali maisha ya watanzania. Naomba tuchangie kwa nia ya kusaidia watanzania
   
 2. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naweza kukubaliana na wewe. Hata kama si ajira lakini wafikirie kuwa na posho hata ya kutosha kwa makatibu wa mikoa na Wilaya. Sijui kama huwa wanapata posho kwa sasa.
   
 3. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wazo lako zuri sana,Chadema tukifanya hivyo sidhani kama kuna jimbo litachukuliwa na CCM,hapo mwanzo chama kilikuwa hakina pesa lakini sasa kuna pesa hata kama hazitoshi chama kijaribu kujenga organisation itakayowezesha kuchukua dora 2015.
  Mabadiliko ni lazima katika nchi hii.
   
 4. R

  Rweza Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe 100% kwa sasa makatibu wa mikoa bado ni wale wa kujitolea. Kwa wilayani ndo usiseme na wengine wako majimboni lakini bado ni yaleyale. Kuna wengine ambao kwasababu ya njaa zao bado wanaabudu viongozi wa Magamba hasa wabunge kwenye wilaya zenye wabunge wa ccm. Wazo la kuwa na makatibu wa kuajiriwa ni la maana sana na hasa ukizingatia kuwa hiki ni chama kinachotarajiwa kushika dola 2015.
   
 5. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  sawa Du Bois, angalau hata posho itawapa morali ya kutenda kazi kwa bidii. Wanaofahamu kama makatibu wa CDM(W) na Mikoa wanalipwa posho watujulishe

  Ni muhimu sana kuhakikisha 2015 tunafanya mabadiliko ya uongozi na sera
   
 6. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  FreedomTZ,
  Wanachokifanya CCM ni Lazma na Chadema wakifanye? anyway Kuna makatibu wa majimbo mpaka sasa!
  Hii inatoka wapi? kwa hoja ya kupata kata3? sie waTZ?

  Majungu ya kwenye vyama vya mipira naona mnataka kuweka kwenye siasa duh?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wewe ni Gamba huna lolote, inamaana umefanya UTAFITI na kuona tatizo ni UONGOZI?
  Conclusion, Fikra hizi ni mbaya sana na kamwe zisipewe nafasi,
   
 8. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa CDM kwa kucopy na kupest
   
 9. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  DR. Slaa, Mbowe, zitto, Arfi, Mnyika zingatieni mawazo mazuri ya wadau wa CDM na wapenda mabadiliko. Chukueni hatua sasa kwa kuajiri makatibu wa mikoa na wilaya; kama katiba ya chama hairuhusu fanyeni mabadiliko
   
 10. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Unavyofikiria sivyo. Tujadili hoja na siyo matusi. Hakuna gamba hapa, kama ambayo wewe unapenda CDM ishinde ndivyo mimi pia nilivyo; isipokuwa tunatofautiana mtizamo. Haiwezekani wote tukawa na fikra zinazofanana. Nimejaribu kutafakari na kudadisi; nikagundua kuwa organisation ya uongozi siyo nzuri kwa nchi nzima.
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wapi kuna TUSI, ama hulijui!?
  Ipo wapi HOJA? Mkuu katafute CCM halisi....
   
 12. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ni sawa kabisa,chadema ijijenge tangu kwenye matawi
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  FreedomTz

  where is the money gonna come from to pay for all these people?

  au unamaanisha chama kisimamishe shughuli nyingine zote za kisiasa zianze kulipa watu mishahara
   
 14. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hawalipwi!!
   
 15. p

  ppkalumba Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli CDM tunataka kuchukua dola katika chaguzi za diwani zilizopita ni fundisho kwetu tujipange namna yakufanya kampeni na kuendelea kujiimarisha vijijini ambako ndiko magamba wanajivunia.Ninaimani na mwenyekiti pamoja na kamati yake wataka chini nakutafakari ni wapi pakuanzia.Muda umeisha mwakani ndo mwaka wakujiimarisha mwakakeshokutwa mtihani wakuelekea ikulu.Pamoja.
   
 16. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja%
   
 17. Man 4 M4C

  Man 4 M4C JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 737
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tunayo safari ndefu, tambueni kuwa sishiem kwa sasa uhai wao unategemea upendaji pesa wa wapinzanji hususani viongozi wao au wagombea, ngalia kule Nzega wamegawa hadi magodoro ili washinde, angalia mvomero mtibwa wamenunua vitambulisho,wanunuaji wamekamatwa wakapelekwa polisi hata masaa 3 hayajafika polisi wanaachia watuhumiwa. Hivyo penye umuhimu wa pesa na tuchangie na sio lazima chama
  • Kumbukeni tunahitaji

  1. vyombo vya muziki
  2. Bendera
  3. Kadi
  4. Vipeperushi
  5. Mlipuko wa wananchi kila kona ambao kuwafikia ni pesa
  6. Magali
  7. Mafuta
  8. Mafunzo ya viongozi na wanachama
  9. Fedha za kampeni kwa majimbo,kata na serikali za mitaa.

  Kimsingi sishiemu ina pesa nyingi sana, <Mungu atusaidie na kutufanyia wepesi cdm
   
 18. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Penye nia pana njia. Ijapokuwa sijui chama kina kiasi gani cha fedha, nafikiri fedha zitokane na vyanzo halali vilivyopo mfano ruzuku kutoka serikalini, ada na michango ya wanachama na wahisani mbalimbali. Pia viongozi wabuni vyanzo vingine vya fedha. Tutaendelea kuchangia kupitia M-pesa ya M4C
   
 19. F

  FreedomTZ JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 1,088
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pompo, nguvu ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache pekee haiwezi kuleta mabadiliko tunayohitaji. usitake watu wenye fikra tofauti na zako wasichangie chochote katk kujenga nchi yetu. Mawazo mgando siku zote hayasaidii kutatua matatizo ya watanzania.
   
 20. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sijui ANC PAC TANU KANU ZANU na vyama vya aina hiyo vilipata wapi fedha za kujiendesha kwa mapambano wakati mwingine makali kwa First Liberation ya Afrika?

  Kinachotangulia ni ile nia ya ndani ya kuleta mabadiliko kutoka kwenye grassroots!

  Je Jumamosi zote WATANZANIA kwa Dar peke yake, tunaharibu Milioni Mia ngapi kwa sherehe,na Jumapili kwa Vikao vya kuandaa sherehe?

  Hiyo amana ikihamishiwa kwenye mageuzi,au elimu au kingine chochote kama kuwezesha majimbo yetu na kata na vitongoji kujiendesha hili lisingependeza?

  Tuwe na vipaumbele sasa tuangalie lipi lenye maslahi mapana,tuwezeshane ili kujenga walau uwezo wa kuimarisha CDM kama tunataka kufanya vizuri zaidi uchaguzi wowote ujao.

  Tujitoe kwa hali na mali,msisahau UHURU NI KAZI!HAKI HAIPATIKANI KWENYE SINIA LA DHAHABU,HUPIGANIWA!
   
Loading...