CHADEMA ahidini kutatua kero za Waislam

Status
Not open for further replies.

nofal

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
220
23
serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua kero mbalimbali za waislam nchini,
Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa CHADEMA kina mtizamo hasi katika mambo ya Waislam,
sasa maoni yangu ni kuwa CHADEMA ahidini kutatua kero za waislam ili kuondoa fikra hizo,
na pia kuongeza wapiga kura wengi zaidi wa chama hicho.
 
sio ushauri mzuri huo mkuu,cdm haitakiwa kuegemea upande wowote,huwezi kutatua matatizo ya kundi moja naukaacha kundi jingine likilalamika,kukubwa ni kutoa haki sawa kwa wote,wanachokita wao wapewe na wenzao nao kama wanamaombi yoyote wapewe,na sio kuambiwa wakrsto na waislam wakutane wakae na watatue matatizo yao,hahahahah hii serikali bwana"ukiwauliza waislam kama wanatatizo na wakristo wanakwambia hapana hatuna problee kabisa" sasa hili beef linalotengenezwa limetoka wapi? wakristo nao wakiwauliza wanakwambia hatuna tatizo na waislam.

"Kuna mda maona ya masoud kipanya yanaingia na kutoka kichwani"
 
Tatizo kero nyingi za waislamu ni ngumu kuzitekeleza!
Nilishamsikiaga ponda kwenye kongamano fulani anasema wanataka bungeni kuwe asilimia 50 wakristo, asilimia 50 waislamu

pia akasema ikishindikana kabisa basi wajitenge mikoa ya pwani iwe ya waislamu na sehemu nyingine ya bara wakristo!

Sasa kuahidi kuwasaidia kwenye hoja za namna hii si kujibebesha msalaba ambao hutaweza kuubeba mbeleni???
 
sisi tunawaahidi watanzania wote, hatubagui kama wewe ni mdemba, mbabagaigi, mwislam, mkiristo, mpagani, nk as long as umezaliwa Tanzania, unaishi Tanzania basi una haki stahiki zote.
 
serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua kero mbalimbali za waislam nchini,
Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa chadema kina mtizamo hasi katika mambo ya waislam,
sasa maoni yangu ni kuwa chadema ahidini kutatua kero za waislam ili kuondoa fikra hizo,
na pia kuongeza wapiga kura wengi zaidi wa chama hicho.

Sishauri...wacha wanaoegemea huko na kuwadnganya waumini waendelee....chadema kaeni mbali na haya mambo ya kidini...kwanza kero za waislamu ndo nini? Mie ndhani unazungumzia kero za wananchi. Acha kuwaza mambo ya kusadikika.

Ungewashauri waahidi kutatua kero za WATANZANIA ningekuunga mkono...
 
Kwani CDM imekuwa BAKWATA?

Hivi kero za WAISLAMU ni zipi ambazo ni TOFAUTI na za Watanzania wengine?
 
serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua kero mbalimbali za waislam nchini,
Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa chadema kina mtizamo hasi katika mambo ya waislam,
sasa maoni yangu ni kuwa chadema ahidini kutatua kero za waislam ili kuondoa fikra hizo,
na pia kuongeza wapiga kura wengi zaidi wa chama hicho.

Kwani waislam wanatakiwa kutatuliwa kero zao na Serikali? Mimi nijuavyo Serikali inabidi ijikite zaidi kutatua Kero za Wajawazito mahospitalini, kero za usafiri kwa watoto wa Shule, Kero ya Foleni Mijini na kadhalika, Kero za Waislam na wakristo nadhani kuna vyombo husika kama vile Bwakwata, TEC au jumuia za kikristo Tanzania, tuache kuibebesha Serikali mizigo ya kipumbavu pumbavu
 
serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua kero mbalimbali za waislam nchini,
Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa chadema kina mtizamo hasi katika mambo ya waislam,
sasa maoni yangu ni kuwa chadema ahidini kutatua kero za waislam ili kuondoa fikra hizo,
na pia kuongeza wapiga kura wengi zaidi wa chama hicho.
Hivi siku wewe ukapewa nafasi ya kuandika sera za chama chochote, utaandika namna uatkavyotatua matatizo ya waislamu au ya wananchi wote?...
 
Khaa!! kwani waliwahi kuahidi kutatua kero za wakristo?? Ndiyo maana issues zisizo na maana kama za kuchinja na zinawasumbua. Haya mambo ya dini waachieni Mashehe na Mapadre:heh:
 
serikali ya CCM imeshindwa kabisa kutatua kero mbalimbali za waislam nchini,
Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa chadema kina mtizamo hasi katika mambo ya waislam,
sasa maoni yangu ni kuwa chadema ahidini kutatua kero za waislam ili kuondoa fikra hizo,
na pia kuongeza wapiga kura wengi zaidi wa chama hicho.
Ndugu yangu NOFAL, chama chochote hakipaswi kutetea haki za waumini wa dini fulani!Chama chochote kinapaswa kutetea HAKI za watanzania pasipo kujali DINI au Kutokuwa na dini! Kero za DINI zinatatuliwa na MWENYEZI MUNGU (Allah), ILA kero za wananchi zinatatuliwa na serikali makini. Uombe CHADEMA iunde SERIKALI MAKINI isiyopendelea!
Ndugu yangu, DINI zote zinailalamikia SERIKALI....! Mimi ninachoweza kuishauri CHADEMA ikiwa watanzania wataamua kuipa madaraka, IJITOE kwenye shughuli za KIDINI! Iwaache waislamu waunde taasisi zao maana BAKWATA inatuhumiwa kuwa ya CCM! Vinginevyo, kujihusisha na mambo ya dini ni kukaribisha UDINI nchini....SERIKALI itatue KERO za watanzania ambamo WAISLAMU,WAHINDU,WAKRISTO na WASIO na DINI wamo..!
 
Huyo itakuwa mujahidna, anawaza kijahidina na wala haelewi kama kuna tofauti ya chama cha siasa na taasisi/jumuiya na/au vyama vya kidini. Anatkiwa aelimishwe tu.
 
Sijui umetumwa na CUF kutesti upepo baada ya Prof. Lipumba kulikoroga? Lakini majibu umeyapata, kwamba chama cha siasa kinatakiwa kushughulika na matatizo ya wananchi, sio matatizo ya waumini.
 
kwa hiyo chdm hakihitaji kura za waislamu? siyo vibaya chama cha siasa kusikiliza matatizo ya makundi mbalimbali ktk jamii yakiwemo makundi ya kidini. ubaya uko wapi kwa mbowe, slaa na viongozi waandamizi kumtembelea mufti na kubadilishana nae mawazo. kuwatembelea viongozi wa kanisa katoliki, anglikana, kkkt, makanisa ya kilokole, wasabato...... mimi sioni tatizo na hili. kote ulimwenguni kura na kuungwa mkono hutafutwa kwa kuonana na makundi maalumu. kuihusisha cuf na waislamu sidhani kama ni suluhisho. jambo hilo linaendelea kuwafanya waislamu wakione cuf kama chama chao. idadi ya waislamu wanayoiunga cuf itazidi kuongezeka. siasa hufanywa kwa kumvuta mtu upande wako siyo kumkimbia na kumbeza. IJULIKANE KUWA BILA KUUNGWA MKONO NA WAISLAMU, CHDM KAMWE HAKIWEZI KUINGIA IKULU. kwa wanao juwa idadi ya waislamu hapa nchini watakubaliana na mimi. huo ni ushauri wangu wa bure.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom