CHADEMA, ACT tambueni ligi hainogi bila uwepo wa Yanga au Simba na mshindi hapo hawezi kuwa na raha

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,383
2,000
Nawashauri mapema kabisa muanze zoezi la kufuatilia kujua picha na majina ya wagombea na vyama vyao katika karatasi za kupigia kura.

Nasema hivi kwasababu mnaweza kukuta kuna wagombea msiowatambua na mkichelewa watawambia muda umeshapita hizo karatasi hawawezi kuzibadilisha tena.

Vile vile iulizeni Tume kwa maandishi kama kuna mtu amewapelekea document yoyote ile akidai ni kutoka kwenye vyama vyenu ikimuidhinisha kugombea nafasi yoyoye ile kwa sasa.

Nawaahauri waandikieni Tume barua mapema kabisa na nakala mzisambaze kwenye vyombo vya habari.

Mkichelewa mnaweza shangaa karatasi za kupigia kura zina wagombea wa vyama vyenu na siku ya uchaguzi mtashangaa na kura wamepigiwa.

Hili nililihisi mara tu baada ya nyinyi kutangaza kususia uchaguzi.

Tambueni Ligi hainogi bila uwepo wa Yanga au Simba na yoyote atakaeishinda hapo hawezi kuwa na raha kama mmoja anakosekana.

Nafikiri mmenielewa.
 

gwa myetu

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
4,396
2,000
Chadema hatushiriki uchaguzi wa kise.nge , mapanga yameshanolewa yanatusubiri vituoni, madc ,rpc, wakurugenzi wote wanahasira na sisi ,ni heri kutoshiriki kunusuru roho za wafuasi wetu maana kwa mazingira haya hatuwezi shinda.
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,361
2,000
Igwe wanaJF!

Nichukue fursa hii kuwapongeza ndugu Mbowe na Zitto kwa kutoa maazimio ya vyama vyao ambayo kimsingi yameonyesha kukubali utendaji wa Raisi JPM na CCM yake katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Naam, Chadema na ACT wazalendo wameamua kuachana na siasa za kupinga kila kitu na sasa wameamua kutowapinga wagombea wa CCM katika uchaguzi mdogo hapo januari 2018.

Kudos Mbowe, Kudos Zitto.
 

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,050
2,000
Chadema hatushiriki uchaguzi wa kise.nge , mapanga yameshanolewa yanatusubiri vituoni, madc ,rpc, wakurugenzi wote wanahasira na sisi ,ni heri kutoshiriki kunusuru roho za wafuasi wetu maana kwa mazingira haya hatuwezi shinda.
Kwani ndiyo mmegundua leo? Miaka ishirini mnashiriki kama wendawazimu vile pamoja na wafuasi kukosa uwezo wa kuhoji mmekua kama ndondocha kesho wakisema tutashriki mnakua wa kwanza kuwapigia makofi na kuwaita makamanda.

Jiangalieni kama haea viongozi wrnu wa maana
 

steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
7,771
2,000
Swadakta mtoa mada,hebu wakumbushe tena hiyo misukule ya mabeberu ingawa post ni ya zamani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom