CHADEMA acheni woga toleeni maamuzi ya rufaa za kina Halima Mdee na wenzake

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,356
2,000
CHADEMA ni chama kinachojinasibu kufuata demokrasia na haki si afya kwa wanachama wanakata rufaa ndani ya chama mnataka mchukue mwaka mmoja kutolea maamuzi hii siyo haki.

Au mnataka kuigeuza ajenda ya kisiasa maana nimeona baadhi ya wanachadema wanasema Rais Samia Suluhu alitolee tamko hili seriously? Hebu tuwe serious basi kwanini Rais alitolee tamko jambo ambalo hata chama hakijafanya uamuzi wa mwisho? Vipi leo Samia au bunge liwafukuze ubunge kina Mdee halafu baadaye washinde rufaa zao kwenye chama? Mtaomba wawarejeshe? Halafu nani ana uhakika Kama Spika amepewa barua za kuwafukuza hao wanachama? Na chadema haiwezi kupeleka barua bungeni wakati imewapa nafasi ya kukata rufaa zao.

Kiufupi akina Mdee ni wabunge wa chadema mpaka chama kitakapofanya maamuzi ya mwisho, maamuzi ambayo chama hakitaki kuyafanya mpaka sasa
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,170
2,000
Wewe nani? Uko wapi? Naona upo nyuma ya wakati sana.

Habari ya mjini leo ni hotuba ya mama SSH wewe unakuja na ngonjera za chadema. Ya chadema waachie chadema wenyewe.
 

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
589
1,000
Hata akikutana anataka wajadili jinsi ya kufanya siasa zenye tija kwa nchi.

Maana yake baada ya kukutana hatutarajii kuwaona akina Lisu wakiponda ATCL, SGR, bwawa la Nyerere kuwa ni miradi ya hovyo badala yake wataanza kusema hiyo ni miradi ya Watanzania.

Kwa akili zao wanahisi mama ataenda kuwaruhusu kufanya maandamano kila siku.
 

Whiteman confusing

JF-Expert Member
Sep 12, 2020
205
250
Kwa mjipu ipi useme wakina Halima na wenzake wawe na ualisia wa kukaa bungeni.

Chama imeshawatimua uanachama bado unan'gan'gana kusema wana sifa ya ubunge.

Kwa msingi ipi kisheria
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom