Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,173
- 3,345
CHADEMA baada ya kuona hali si shwari na kuwa kwenye maji ya shingo, wameanza matumizi ya maneno ya 'kujifariji' ili wapate huruma ya wananchi.
Kumbukumbu zangu zinasema CHADEMA ni chama cha vuguvugu, yani 'mikikimikiki ya mabadiliko' ndio moto wao huu, sasa iweje leo chama hiki kianze kutumia maneno ya huruma na upole?
Utakuta siku hizi katika matamko ya CHADEMA wameweka porojo zao nyingi halafu mwisho wanamaliza kwa kuandika "TUMEANZA NA MUNGU TUTAMALIZA NA MUNGU", sasa hii ndio nini?
CHADEMA niwakumbushe, hapa hatufanyi kazi ya kanisa wala msikiti, tupo hapa kufanya siasa, hakuna habari ya kutafuta huruma kwa wananchi hapa, kwahiyo hakuna tija yoyote kutumia maneno hayo kwenye matamko yenu dharimu.
Kachukue buku saba umeifurahisha kamati ya Lumumba.