Mulama
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 3,018
- 1,791
Mkuu nakuunga mkono mia kwa mia, maana kwenye kampeini za uchaguzi mdogo tumeshuhudia uungwaji mkono was vyama vya upinzani kwa kiwango cha juu sana kiasi kwamba ccm ikaamua kuua mtoto was shule kwa hasira ya kukataliwa.Mkuu wala sikufichi, kwa aina ya siasa waliyoamua kufanya ccm chini ya mwenyekiti wake, ni dhahiri umma sasa umeanza kuona picha halisi ya ccm mpya. Ukijaribu kuangalia miaka miwili ya awamu hii ya tano kulijaribu kujengwa propaganda kubwa kwamba sasa Tz imepata kiongozi iliyemtaka. Kwa bahati mbaya inaoenakana mgema kasifiwa na sasa tembo kalitia maji. Ni ukweli usiofichika uchumi unadondoka kwa kasi, ajira hakuna na dalili ya kuwepo kwake zinazidi kutoweka. Halafu kwa haya mauaji na uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, naona watu wakibadilika kwa kasi.
Jaribu kutazama lugha za viongozi wa dini kuelekea serekali hii, nidhamu ya woga iliyokuwa imejengeka ndani ya miaka hii miwili inapungua kwa kasi ya mwanga na sasa watu wanaongea ukweli. Ile miradi iliyopigiwa debe sasa wananchi wanaweza kujionea wenyewe ukweli na uongo wake Sijui ni kipi kitaendelea mpaka 2020, lakini nakuhakikishia kwa kasi hii ya watu kubadilika ikifika kipindi hicho tutashuhudia umwagaji mkubwa wa damu iil ccm iendelee kubaki madarkani. Dalili za haya ninayoyasema tumeziona kwenye chaguzi hizi zilizopita ambapo ccm ilitakiwa ishinde kirahisi na kihalali lakini imekuwa kinyume chake.
Haya yanatendeka ikiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili mfululizo ccm imetumia kila aina ya nyenzo kukashifu, kuponda, kubeza na kuumiza upinzani mbele ya raia ikitegemea kwa kufanya hivyo ingeungwa mkono!