Uchaguzi 2020 CHADEMA achaneni na sera ya Majimbo, sera ya ukata itafaa zaidi

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Kwa mujibu wa TUME ya UCHAGUZI Tanzania ina jumla ya KATA 5350.

Kama kila kitu ikitengewa bajeti ya TZS BILION moja KWA MWAKA Itakuwa ni Trilioni Tano nukta 3 kwa Kata zote TANZANIA. Hii Bilion Moja ikitumika vizuri ndani ya mwaka kata zetu zitakuwa ni ULAYA kwani Kila mwezi itapokea Milioni 100 ambapo itaamua tu kipamubele ni nini. Leseni zote za biashara zitolewe ofisi za kata. Usajili wa biashara zote ufanyike ofisi za kata. Vibali vyote vitolewe ofisi za kata.

Kwa kufanya hivyo zitazalisha jumla ya ajira 53,500 kwa kada za kuwahudumia wananchi kama vile watoa leseni wasajili wa biashara,etc. Kwa kufanya hivyo huduma zitafika kwa mwananchi kwa umbali wa kutembea kwa miguu. Kwa kufanya hivyo makusanyo yote ya kodi yataratibiwa katika ngazi ya KATA. UKATA utaleta maendeleo kwa wananchi moja kwa moja na kuleta maendeleo shirikishi au maendeleo ya watu.

Nimeeleza kwa kifupi ila wale wenye akili fupi waelewe kwa ufupi.
 
Nchi nyingi utawala wa Majimbo unagawanywa ki jiografia. South-East, North-West, North-East nk

Majimbo yanajitegemea kuanzia huduma za umeme, maji, barabara kila jimbo linakua na kampuni yake. Pia Kuna ushindani wa kutaka kufanya vizuri kama jimbo la North-East mfano.
 
Nchi nyingi utawala wa majimbo unagawanywa ki jiografia. South-East, North-West, North-East nk
Majimbo yanajitegemea kuanzia huduma za umeme, maji, barabara kila jimbo lina kampuni yake. Pia Kuna ushindani wa kutaka kufanya vizuri kama jimbo la North-East.
Kama China hawa si wanajifanya wanaiga mambo ua china au wao wanaiga udikiteta tu?
 
Nchi nyingi utawala wa majimbo unagawanywa ki jiografia. South-East, North-West, North-East nk
Majimbo yanajitegemea kuanzia huduma za umeme, maji, barabara kila jimbo lina kampuni yake. Pia Kuna ushindani wa kutaka kufanya vizuri kama jimbo la North-East.
Majimbo yataongeza gharama za uendeshaji bila kuongeza ufanisi.Kata zitaongeza vyote.Mwananchi atwaweza kupata huduma zote kwa kutemblea ofisi ya KATA na kupewa majibu hapo hapo.
 
Majimbo yataongeza gharama za uendeshaji bila kuongeza ufanisi.Kata zitaongeza vyote.Mwananchi atwaweza kupata huduma zote kwa kutemblea ofisi ya KATA na kupewa majibu hapo hapo.
Majimbo yanarahisisha huduma kutoka serikali kuu, yanazalisha ajira, leseni za biashara zinapatikana majimboni hata vibali vya kuvunia misitu mfano. Mzunguko wa pesa unaongezeka.
 
Majimbo yataongeza gharama za uendeshaji bila kuongeza ufanisi.Kata zitaongeza vyote.Mwananchi atwaweza kupata huduma zote kwa kutemblea ofisi ya KATA na kupewa majibu hapo hapo.
Hapana. Dhana ya majimbo ya namna hii ndiyo ya kukata nchi vipande vipande. Sema ya kwako ya vi kata kata ni afadhali kwa kuwa haviwezi kuwa na nguvu ya kufifisha utaifa.

Dhana ya Majimbo ya kikanda, kama asemavyo Eclat hapo juu, ni mbaya. Inaleta nchi kuto-ongozeka. Hii ndiyo dhana ya zamani ya Mbowe ya majimbo. Dhana ya majimbo ya Lissu ni tofauti kabisa.

Ni ya kugatua madaraka ya uamuzi kutoka hodhi ya Urais, na ni ya kuwachagua wenye maamuzi makubwa ya utawala na maendeleo ili wawajibike kwa wananchi. Watu hao ni wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri (ma DED). Wananchi wasiletewe tu watu hawa kuwatawala. Wawapigie kura! Labda tuongezee na watendaji wa kata humo! Mikoa, Wilaya, Halmashauri zaweza kubaki zilivyo sasa, lakini viongozi wake wapigiwe kura!
 
Hapana. Dhana ya majimbo ya namna hii ndiyo ya kukata nchi vipande vipande. Sema ya kwako ya vi kata kata ni afadhali kwa kuwa haviwezi kuwa na nguvu ya kufifisha utaifa. Dhana ya majimbo ya kikanda, kama asemavyo Eclat hapo juu, ni mbaya. Inaleta nchi kuto-ongozeka. Hii ndiyo dhana ya zamani ya Mbowe ya majimbo. Dhana ya majimbo ya Lissu ni tofauti kabisa.

Ni ya kugatua madaraka ya uamuzi kutoka hodhi ya Urais, na ni ya kuwachagua wenye maamuzi makubwa ya utawala na maendeleo ili wawajibike kwa wananchi. Watu hao ni wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri (ma DED). Wananchi wasiletewe tu watu hawa kuwatawala. Wawapigie kura! Labda tuongezee na watendaji wa kata humo! Mikoa, Wilaya, Halmashauri zaweza kubaki zilivyo sasa, lakini viongozi wake wapigiwe kura!
Mpaka sasa hii tunawapigia kura wabunge,wameleta tofauti gani?Huwa muda wa kukaa kuchagua wabunge,madiwani,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,etc unatoka wapi?Nafikir ungesema labda wabunge wapanidhwe vyeo wawe na some executive POWER mfano.Wakiweka sharti kwamba Mapato yote na Matumizi ya Jimbo lazima yaidhinishwe na Mbunge tayari tutakuwa tumesolve pakubwa.Au unaonaje?
 
Nchi nyingi utawala wa Majimbo unagawanywa ki jiografia. South-East, North-West, North-East nk

Majimbo yanajitegemea kuanzia huduma za umeme, maji, barabara kila jimbo lina kampuni yake. Pia Kuna ushindani wa kutaka kufanya vizuri kama jimbo la North-East mfano.
Katika hizi kanda kuna makabila mbali mbali, mengine makubwa vingine vidogo. Sisi wa vikabila vidogo si ndo tutamezwa kabisa. Kila kura za kuchagua mkuu wa mkoa kabila kubwa wanashinda. Sisi vikabila vidogo hata kazi za ufagizi tutakosa.
 
Majimbo yataongeza gharama za uendeshaji bila kuongeza ufanisi.Kata zitaongeza vyote.Mwananchi atwaweza kupata huduma zote kwa kutemblea ofisi ya KATA na kupewa majibu hapo hapo.
Yataongezaje gharama?? Embu fafanua?
 
Ni maajabu hata hujui "SERA YA MAJIMBO" ni kitu gani...

Sijui mnakulaga ugoro wa wapi aisee....

Nonsense kabisa
 
Sera ya kupunguza mzigo wa Kodi haswa VAT na utitiri mwingine wa kodi ni Sera muruaa kabisa
 
Back
Top Bottom