CHADEMA 2010: Kutoka "Hapa" mpaka "kule"

Mkandara,

Mawazo mazuri hayo.

Kuhusu Usalama wa Taifa, kwa muda mrefu sana wamekuwa wanaogopa kwamba ikiwa Zanzibar itapewa uhuru au nafasi zaidi ya kufanya wanachotaka, visiwa hivyo vitakuwa ni springboard and a haven for subversive elements who could threaten the union pamoja na usalama wa nchi. Ni sababu moja kubwa, kati ya sababu zingine, kwa nini CCM, ambacho ni chama cha Tanzania bara, have maintained a tight grip on the former island nation.

CCM wanacho sahau, au wanacho puuza makusudi, ni kwamba wakiendelea kuwakandamiza Wazanzibari, that's exactly what will happen: they will continue to infuriate Zanzibaris, and Zanzibar will become a breeding ground for the very elements the union government claims it fears.

Kuhusu vyama, ni kweli CUF hawana chochote Tanzania bara. Ni chama cha visiwani. Na CCM wanatumia mabavu tu kutawala visiwani.

Pia ni muhimu kwamba Chadema iahidi kubadili katiba ya nchi kuridhisha pande zote mbili za Muungano: bara na visiwani.

Kuhusu Zanzibar kujiunga na OIC, sioni tatizo lolote. Hata nchi nzima ikijiunga na OIC siyo tatizo. Haimanishi kwamba Tanzania will become a theocratic state - (Islamic); it will remain a secular state.

Chadema inaweza kuahidi itatimiza hayo yote kujenga msingi wa maendeleo, ambao hatuna, kuimarisha Muungano, na kuwaridhisha wananchi wa Tanzania bara na visiwani.
 
CUF imepungua nguvu kwa kuwa ilikuwa ikimtegemea mtu mmoja kwa ajili ya umaarufu wake, na hili lilitokea si kwa kupenda. Lilitokea kwa sababu vyama vya upinzani vimebanwa mbavu, kufanya shughuli zao imekuwa kama vile ni wavunjifu wa sheria. Ikabidi wategemee kukuru kakara za maalim ili wapate kusikika, zimewasaidiaa kwa kipindi chote hiki. Na kama isingekuwa kubanwa mbavu kwa hapa walipofikia isingekuwa ngumu tena kwenda mbele wao wenyewe, lakini wakitaka kusema na wananchi watatumia chombo gani? wakitaka kueleza mikakati mbadala watatumia chombo gani?. Ili mradi mazingira yamejengwa kiasi ukitaka kukaribia karibia na kuona kuna nini huku, uonekane wewe ni msaliti na umeanza ukorofi. Wajanja wakaona njia rahisi ni kumfanya rafiki ili wanaomfuata na kunufaika na umaarufu wake waachwe solemba, ndio yaliyowakuta CUF. Dawa pekee ni kwa sisi wananchi kudai mazingira sawa kwa vyama vyote ili viweze kufanya kazi yao ya siasa kwa uhuru, vyama hivi ni vya watanzania hakuna sababu ya kuwanyima haki wengine na wengine kutamba kama wafalme.
 
Shedafa,
Hiyo hali haiwezi kupatikana ikiwa Dr.Slaa na Chadema hawataweza kuweka Upinzani wa kutosha kama CUF huko Zanzibar miaka iliyopita. Tatizo ni kwamba CCM will never bowdown to anyone, hata hao CUF wamewapa ahadi ambayo nina hakika haiwezi kuleta mabadiliko kwa wananchi zaidi ya kuondoa Uhasama wa viongozi wao wa CUF na baraza la mapinduzi. Wanachoshindwa kuelewa CUF ni kwamba hata ndani ya CCM baraza la Mapinduzi kuna makundi hawakubaliani wote, hivyo nasubiri kuona matokeo baada ya uchaguzi.

I strongly believe to never shake hands with a devil mwache yeye asilimu (abatizwe) ndipo maelewano yanaweza kuja ili kizazi kijacho kiwe na imani moja. CCM walikuwa ktk wakati mgumu sana wakati Mwinyi alipokuwa rais, na Zanzibar as one walidai kwa nguvu moja haki zao hadi Nyerere akaingilia kati maanake Mwinyi kimba lilimbana..sasa maadam CCM survived that, I'm 100% sure CUF haiwezi kuwa tishio kabisa la Muungano hata kama wamefikia muafaka sasa hivi.

Maelezo ya Mwanakijiji kwa mapana yake kuna mengi ya kujifunza, lakini pia mengi ya kutazama kwa ukaribu zaidi na kupima kulingana na siasa za Bongo. Kosa moja tu CCM wanaweza kulikuza na kulipa sauti kubwa sana wakitumia kuhatarisha Amani na Utulivu. Nadhani katika yote Mwanakijiji hakugusia zaidi mbinu za CCM dhidi ya mahitaji mengi ya Chadema aliyoorodhesha kwani sifa ya CCM ni kama Simba. CCM ndiye Simba porini mwenye njaa ktk uchaguzi huu na hakuna Simba wawili kuwindana kula nyama. We ought to kill the beast!

Maadam Simba hutafuta mnyama anayelegalega na kumkaba koo kuondoa pumzi zake. Chadema hawatakiwi kuiga mbinu za CCM kuua mnyama, isipokuwa huyu Simba (CCM) anatakiwa kuwekewa chambo iwe mbuzi au ng'ombe huku akisubiriwa na marksman mwenye powerful rifle. Tusitegemee compromise baina ya Simba, mnyama na binadamu ktk mbuga za serengeti..Only the strong one will survive!
 
,then its ok to stew him a little bit,but it should be in the manner that I would not take vote away from him.
The next president of Tanzania himself (Slaa)has accept the challenges which will make the part even stronger,na kukuza demokrasia.

kura haziji kama zawadi; zinastahiliwa. Na mtu ambaye hawesti kuhimili joto, asikae jikoni.
 
Kinachnifurahisha ni kuwa leo hii tunahamaki na kuhoji timing ya maandiko haya, je tulipoanza kuyaandika kwa naman moja au nyingine baada ya Kikwete kuapishwa December 21 2005, hatukuona umu8himu wa kuelewa linalosemwa?

Kama kuna Chama kilichofagiliwa kw akukosolewa kama njia ya kuonyeshwa njia bora baada ya CCM, ni CHADEMA, lakini hapa ndani tumekuwa na mvutano wa watu kupenda watafuniwe kila kitu.

Leo hoja ya kujenga Itikadi inaonekana mali, kisa imandikwa kwa nadharia na mifano myepesi, lakini lilipoongelewa miaka na mara kadhaa zilizopita, si majibu ya kejeli na kudharauliana yalikuja na kudai Watanzania hawawezi kuishi kwa Itikadi, bali CCM iondoke kwanza madarakani?

Ukweli ni kuwa sasa kwa lugha ingine, Mzee Mwanakijiji kabainisha yale ya Focus 2010, Chadema must Reform, Udhaifu wa Operesheni Sangara, What next na realit inaingia vichwa ni kuwa kiu yetu ya kuleta mabadiliko inaweza ikafulia kwa kushindwa kuituliza hiyo kiu inavyopaswa.

What I am reading from people reaction is the fear of unknown and realization that the task is not as easy as desired and failure to be organized and gave a careful thought, mey end up being a disaster!

Muda bado upo mkubwa sana na badala ya kulumbana kwa nini haliuandikwa hili mwaka juzi, focus iwe ni vipi tutafanikisha kilichoandikwa na si kujutia muda!

Siasa ni lazima undavaundava na ubabe utumike, sasa ni wakati CHADEMA waamue kwenda vitani wakishikilia mabua na pamba au wawe na mawe, singe na rungu!
 
Nimerudi kusoma hiki tena na ninaamini inahitaji kuangaliwa sasa hivi zaidi kuliko nilipoandika mwaka jana.
 
Nimerudi kusoma hiki tena na ninaamini inahitaji kuangaliwa sasa hivi zaidi kuliko nilipoandika mwaka jana.

Mkuu MMKj;Kwa ruksa yako!

Hii andiko kwa asilimia kubwa 70% imetulia na amini pale Makao makuu ya CDM kwa muda huu miaka mitatu inaelekea kuisha watakuwa wamechukua hatua!


Mimi nichangie maeneo madogo!

Hoja hii hapa chini si salama hata kidogo na sintafafanua wacha kila shabiki na asiyeshabiki aitazame kwa upeo wa kufikiri na mapenzi yake!


Chadema inapokutana kumtangaza mgombea wake wa Urais ni muhimu vile vile itangaze wakati huo huo kuwa mheshimiwa mmoja atakaposhinda basi atakuwa Waziri Mkuu. Ahadi hii ni lazima ieleweke kwa wananchi kuwa endapo wananchi wanaamini Chadema imefanya kazi nzuri miaka hii michache iliyopita basi iko tayari kuwapatia taifa Waziri Mkuu. Na hilo litawezekana tu endapo Watanzania watachagua wagombea wa Chadema wa Ubunge kwa wingi zaidi.


Hoja hii hapa nakubaliana nawe kwa 100%.Tumekuwa tukilalamika sana na suala la ucheleweshaji wa maamuzi kisa ikiwa mlolongo wa kada ya utawala!


Kwa upande wa Chadema muundo wake wa vikao ni kama ifuatavyo:

1. Ngazi ya Msingi

2. Tawi

3. Kata/Wadi

4. Jimbo/Wilaya

5. Mkoa

6. Jimbo.

7. Taifa
Mfumo uliopo sasa ni mzuri kama chama ni kimoja, kwenye mfumo wa vyama vingi huu ni utiriri wa vikao vingi visivyo vya lazima. Kwa mfano, kwanini kusingekuwa na kikao cha mwanzo kabisa kuwa ni kikao cha Kata (ambacho kinaunganisha kikao cha msingi a.k.a shinda, kata na tawi) na kikao kinachofuatia kiwe ni kile cha Jimbo na Wilaya (ambaho chaweza kuwa ni cha jimbo la uchaguzi au wilaya ya utawala) na kika cha mkoa na kile cha taifa? Kwa mtindo huo uongozi wa chama unakuwa na ngazi nne tu.

Mkuu siku utakapoji rudia kusoma andiko hii labda utakumbua na hili


Siku moja nitafunua hiyo nguvu ambayo imewabana viongozi wetu na ambayo ndiyo siri hasa ya utajiri wao mkubwa wa muda mfupi


Ni kweli kabisa katika hili wamekuwa wakisuasua na bado kuna mengi ambayo yanafaa yafikishwe mbele ya Mahakama mara nyingi haitoshi kulalamikia Sheria majukwaani bila ya kufikisha madai mbele ya Mahakama.


Kutokana na kutokuwa na fikra za kuwa wanataka kutawala Chadema ilipoteza nafasi nyingi katika suala hili ili kuonesha kuwa ni kweli kinapiga vita ufisadi.


4. Pamoja na hilo la tatu Chadema imeshindwa aidha kwa kutotaka au kwa kutokuwa na nia ya kuonesha kuwa ina maslahi katika mwelekeo na matokeo ya kesi hizi mbalimbali kuomba kuwa rafiki wa mahakama (amicus curiae) na hivyo kupata nafasi ya kusikilizwa. Hili ni muhimu kwa sababu katika kesi hizi Chadema ina maslahi kwa sababu kimepigia vita ufisadi katika maneno lakini katika vitendo kilihitaji kuonesha kuwa kinafutilia kwa karibu.

5. Chadema kama chama cha kisiasa kingeweza kabisa hata kuleta mashtaka binafsi (sheria yetu inatambua) kuhusu mambo au taasisi mbalimbali kwa muda wote huu. Yangeweza kuwa ni mashtaka ya kikatiba au vinginevyo na kuweza kuifanya Chadema iwe kweli chama kinachopigania haki na demokrasia. Leo hii katika masuala ya haki na demokrasia mchango mkubwa haupelekwi kwa Chadema bali kwa Mchg. Christopher Mtikila. Kwa chama chenye ujiko mkubwa wa kisiasa kama Chadema huu ni udhaifu


Kwenye hoja ya Sera kusema kweli kazi bado ni kubwa na inafaa ipewe timu ya Wataalamu waliobobea kwenye kazi hii na inafaa kazi hii. kama kuna nia njema iwetayari kabla ya Sept.2014


Sera ya Makazi Sera ya Wanawake na Watoto Sera ya Diplomasia Sera ya Sheria Sera ya Habari na Mawasiliano Sera ya Usalama wa Taifa (wanatumia sentensi moja katika sera ya Utawala Bora na hivyo wanalichukulia Usalama wa Taifa kama sehemu ya “utawala bora” badala ya kuwa sehemu ya ulinzi na usalama.)


Sera ya Ulinzi ya Chadema: Majeshi yetu tumeyarithi kutoka kwa mkoloni na kwa bahati mbaya baadhi yao bado yana ule mfumo wa utiifu (blind obedience) aliyekuwa anatarajia mkoloni kutoka kwao! Hisia za wananchi kwa baadhi ya vyombo hivi hasa Polisi na Magereza zimebaki kama ilivyokuwa kabla ya uhuru kwamba vyombo hivyo ni adui wa raia! Wananchi wanashambuliwa na polisi kwa maagizo ya wakubwa wao wa kazi wanaopokea amri zenye mnuko wa kisiasa kuliko ule wa kisheria. Sera ya CHADEMA inajaribu kubadilisha imani, mwelekeo na maadili ya vyombo hivi ili imani ya wananchi irudi kuwa vyombo hivi vipo kwa manufaa yao na siyo kwa sababu tu ya kuwasumbua, kuwaumiza na kuwaswaga kifungoni kila wapendapo au wanapoamriwa. Vilevile inakusudia kuboresha hali duni ya wafanyakazi wa vyomho hivi. Afisa mwenye njaa kali hataacha kutumia cheo na wadhifa wake kudai na kupata rushwa kutoka kwa mwananchi. Vipi basi mwananchi huyu ataamini kuwa Afisa huyo na jeshi lake ni RAFIKI WA RAIA? Hii ni sera ya ulinzi ya chama ambacho kinataka kutawala watu milioni zaidi ya 40. Je, tunaweza kuwapa watu nafasi ya kuunda serikali wakati hawatuelezi ni nini wanachotaka katika ulinzi wa taifa letu na ni nadharia gani inawaongoza katika mambo ya ulinzi. Je, wataongeza idadi ya wapiganaji wetu au watapunguza na kwa nini? Je, JKT na majeshi mengine yana nafasi gani katika ulinzi na ujenzi wa taifa?
Hotuba kama hii inafaa kuwa sehemu ya mikakati ya kuhamasisha Umma lakini ni muhimu kukumbuka watanzania kusoma maandishi ni shida kubwa hiyo ujumbe hautafika na namna bora nikutafuta na kuwa na Sauti /Audio.
Matumizi ya hotuba kama hizi kabla na wakati wa mikutano ya umma ni uhamasihaji tosha katika vita dhidi ya Ufisadi!






“Ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi katika nchi wakati wa amani kuliko vita. Naamini ufisadi katika nchi ni lazima ushughulikiwe kama vile ambavyo tungeshughulikia uhaini. Kama watu hawawezi kuwa na imani na serikali yao, kama watu wanaona kuwa haki inaweza kununuliwa, watu hao wanaachiwa tumaini gani?” - Bungeni, 1960



Hapa pengeine kuna ukweli lakini inategemea!
Wataalamu/wasomi wengi wamekuwa Wanasiasa tena wa waziwazi katika mazingira ya namna hii unaweza kuona utapata ushauri wa aina gani!

Chukulia hata ushauri/mtazamo kama huu wa kwako hauwezi kuwa jibu mia kwa mia.Mkuu MMKJ kama ulivyodadavua Sayansi inafaa kutumika kwenye siasa lakini uhalisia wa Jamii ya maeneo husika na muda bado ni vitu muhimu na ndiyo maana wanasiasa wamekuwa sehemu ya mikakati hii na nami kwa mtazamo wangu na kubaliana kushirikisha Sayansi kwenye maeneo hasa ya Sera .
Tuna haja ya kujitambua kuwa bado maeneo mengi ya Nchi yetu uelewa wa jamii kuhusu haki,uhuru wao bado ni kitendawili kwa hili unaweza kuona ugumu wa kazi hii/mikakati.


Kosa kubwa la Chadema kwa muda mrefu ni kuacha mikakati yake ya kisiasa iendelee kupangwa na wanasiasa wenyewe na viongozi hasa. Mipango na mikakati hiyo wakati mwingine imefanya vizuri lakini vile vile imewadumaza kifikra. Changamoto kubwa ni jinsi gani itaweza kuwahusisha mashabiki wake nje ya Chadema katika utaratibu unaoeleweka na hasa kuunda kwa mfano timu ya mikakati na ushauri ambayo haihusishi wanasiasa ambao ni wagombea. Timu ya namna hiyo inaweza kuundwa na kufanya kazi katika mfumo wa ushauri wa kisayansi wa hatua mbalimbali.
Kwa mfano, kwa muda wa miaka zaidi ya 15 tangu iundwe ikiwa na wabunge wa kutosha tu ni kwanini Chadema haijaweza kujenga Jengo la kisasa la ofisi zake? Ni kwa nini kwa mfano pamoja na kupigia kelele utendaji wa serikali Chadema imeshindwa hata kuanzisha shule moja ya msingi au ya sekondari ya mfano ambayo ingemalikiwa na wanachadema wenyewe? Maswali mengine yanaweza kuulizwa vile vile.





Mwisho natumai Dr.Slaa na timu yake bado hii kitu wanaifanyia kazi na hajaiweka kwenye makabati panya wakiigeuza jumba la kuzaliana!
 
Last edited by a moderator:
Thanks! A must read article
View attachment 11896

YALIYOMO
UTANGULIZI
HAPA
SURA YA 1: Kutoka Upinzani kueleka Utawala
Nani anataka kutawala? … Uk. 5

SURA YA 2: Kushika madaraka ya nchi
Kutawala si si lele mama................Uk. 8

SURA YA 3: Mfumo na Muundo wa Chadema
Tatizo lile lile?..................... Uk. 11

SURA YA 4: Chadema na historia ya Mapambano dhidi ya ufisadi
Mashujaa wako wapi? ………………Uk.18

SURA YA 5: Chadema na chuki dhidi ya CCM
Chuki pekee haitoshi……….Uk. 27

SURA YA 6: Chadema na ujumbe wa matumaini
Nani atapiga mbiu ya vita...Uk. 31

SURA YA 7: Mahusiano ya Itikadi, Sera, na Ilani za chama cha siasa
Kujua mambo ya msingi………………….Uk. 35

SURA YA 8: Sera za Chadema kuelekea uchaguzi mkuu-
Ni sera au ilani?........Uk. 42

KULE

SURA YA 9: Tulipo “hapa” na tunakokwenda “kule”
Tutapiga kambi au tutaondoka?............Uk. 50

SURA YA 10: Kuleta Mapinduzi Baridi
Kutangaza wagombea Urais, Uwaziri Mkuu na Spika….Uk. 58

SURA YA 11: Kutoka “hapa” mpaka “kule”
Ushindi huletwa, hauji wenyewe………….Uk. 64

NENO LA MWISHO……………………...Uk. 69

Kwa heshima ya wale mashujaa wetu ambao juu ya mabega yao nasi twasimama

UTANGULIZI

Historia ya maisha ya mwanadamu tangu uumbaji wake ni historia ya kuhama. Kutoka utoto kuelekea uzee, kutoka sehemu moja ya jiografia kwenda nyingine na kutoka hali moja ya maisha kwenda nyingine. Mwanadamu amefanikiwa pale tu alipoweza kufahamu haja hii iliyo ndani yake ya kutotosheka na pale alipo na hivyo kutaka kwenda katika ngazi fulani. Historia ya kisiasa nayo ni hivyo hivyo. Tumetoka katika hali mbalimbali za kuanzia Ujima hadi maisha ya kisasa. Jamii ya watu iliyojaribu kubakia katika hali yake ya zamani imejikuta ikipigwa na jamii nyingine.

Nimetaka kuandika kwa muda mrefu sasa kuhusu Chadema lakini kwa muda mrefu nimekuwa nikisika nikisubiri muda muda muafaka. Kutokana na hilo utaona sijaandika mengi kuhusu Chadema kama chama licha ya matukio mbalimbali ambayo yaliwafanya wengine waandike juu yake. Hata hivyo naamini huu ni wakati muafaka kufanya hivyo kuweza kuandika kiyakinifu na kibunifu juu ya uwezekano kuwa Chama cha Demokrasia chaweza kuwa ndicho chama kitakachotimiza unabii wa kuanguka CCM ambao niliuandika juu yake mapema mwaka 2007.

Nilianza kuandika juu ya hili baada ya sakata la Buzwagi lakini mara zote nimejikuta nikikwama kufikia hatima yake na hivyo nimevuta muda taratibu hadi nimefikia hapa. Wakati huu umefika kuwa ni muafaka kwa sababu ya matukio makubwa mawili. Kwanza, watu wengi walishangazwa na mimi kuunga mkono chama kichanga kabisa cha CCJ katika kuongeza mwamko wa siasa za upinzani Tanzania, kitu ambacho wengi hawakukielewa na labda kwa kiasi watakaponisoma humu wataelewa kidogo. Pili, ni baada ya kutambua pasipo shaka kabisa kuwa CCM haina ajenda ya kushughulikia ufisadi wala kutambua kuwa ufisadi ndiyo adui mkubwa kabisa wa maendeleo yetu kuliko maradhi, ujinga na umaskini. Hili limethibitika katika Mkutano Mkuu wa CCM ambapo CCM imeshindwa kujisafisha na badala yake majinamizi ya zamani yameruhusiwa kufuliwa tena. Ni lazima tuwe na njia ya kutokea.

Hivyo, “Chadema 2010” ni sehemu ya mchango wangu mdogo katika kukoleza kampeni za uchaguzi mkuu lakini zaidi kwa ajili ya kukipima CHADEMA kama kiko katika hali ya kuweza kudhaminiwa utawala wa taifa letu. Kwa vile utawala wa taifa si jambo dogo hata kidogo na kwa vile kubadilisha uongozi mzima wa nchi siyo jambo la kufanyia majaribio nimejaribu kukipitisha chama hiki kwenye tanuru ya moto wa fikra mbadala na kuona kama kinaweza kutupeleka huko tunakotaka au tuendelee kutumaini chama kingine.

Hivyo, kazi hii imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni ile ninayoiita “Hapa” na sehemu ya pili ni ile ya “Kule”. “Hapa” ni kuangalia hali ilivyo ndani ya Chadema na siasa za Tanzania na ni kwanini Chadema haiwezi kutuongoza hadi itakapokuwa tayari kuhama toka “hapa”. Sehemu hii ywa kwanza inaweza kuwa chungu kidogo kwa baadhi ya watu na kusababisha hisia za kukerwa, hasira, na kuona wanasakamwa. Wakivumilia hilo na kupita salama basi wataweza kuendelea na sehemu ya pili. “Kule” ni kule ambapo matamanio yetu wengi ambao tumekuwa tukisimama kama miali ya moto kuimulika serikali na CCM tunataka nchi yetu ipelekwe. Lakini kule vile vile kule ambako Chadema inaweza kwenda. Kwa ufupi basi “hapa” kwa Chadema ni “upinzani” na “kule” kwa Chadema ni “utawala”. Mstari wa kutoka upande mmoja kwenda mwingine umenyoka.

Natumaini kazi hii itawasaidia viongozi, wanachama, mashabiki na wale wote wenye kutaka mabadiliko ya kweli Tanzania kuweza kupata fikra mpya za mabadiliko ambazo zitaongezea au kuchochea fikra ambazo tayari walikuwa nazo. Mengi ninayoyaandika hapa siyo mageni kwa wasomaji wangu wengi na watu wanaofuatilia mijadala mbalimbali ya kisiasa nchini. Natumaini kazi hii itakuwa ni mwinyu tu wa kuchochea fikra hizo.

Katika yote, niseme kuwa kati ya wagombea wote ambao leo wanasimama kutaka kugombea nafasi ya Urais naamini Dr. Wilbroad Slaa aweza kuwa mtu ambaye ataongoza taifa letu kuelekea mafanikio ya kweli. Hata hivyo, ni lazima kwanza awe tayari yeye mwenyewe na wale walio nyuma yake “kutoka hapa” na kuanza kuonesha kuwa wako tayari kwenda “kule”. Hata hivyo, kama zilivyo safari za jamii nyingine za watu, ni rahisi kuzungumzia kutoka “hapa” na kwenda “kule” ni vigumu zaidi kuanza safari hiyo.


M. M. M.
 
Back
Top Bottom