What it if that is the case??
Huwezi kufurahia nia njema aliyo nayo kwa CHADEMA kiasi cha kutotaka warudie kosa mpaka uulize kwanini anamzimia jirani moto wake wakati kwake kuliungua?
[/QUOTE]Umefika wakati tuwe optimistic na sio perssimistic, mbona huko US, UK, Israel, na hata kwa jirani zetu Kenya wanabadilisha vyama, kwa nini nasi tusifanye hivyo?
In short, had I been a peer reviewer of your article, I would have dismissed it outright!!!!!!!
Go go go Dk Slaa although ungejijenga 2015 ilikua muda muafaka au utaonekana mzee
Mkuu GS,
Mtu anaekueleza mapungufu yako ni mtu mzuri sana na anakutakia mema, kuliko yule anayekuambia sifa nzuri (strengths) ambazo zinaweza kukuvimbisha kichwa na hatimaye ukabweteka ukijua kwamba umekamilika na kumbe kuna wengine waliokamilika zaidi. Siku ukija kupambana nao wanakushinda kirahisi na baada ya hapo unaanza kujuta.
Hiyo kazi ya Mwanakijiji haijachelewa, siku bado zipo, bado kuna muda wa kuyafanyia kazi hayo mapungufu. Unajua wakati mwingine mtu anaweza asijue apeleke wapi mchango wake wa mawazo maana hana uhakika kama mchango wake huo utakubalika ama kupokelewa vipi. Kwa hiyo nina imani kwamba kwa wadhifa/madaraka aliyo nayo Dr. Slaa na kwa kuwa sasa anapeperusha bendera ya CHADEMA, basi atakaa chini na kuchambua kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.
Sijapitia hiyo kazi ya Mwanakijiji, lakini kama kuna criticisms ambazo ameziweka humo, basi mpeni nafasi aseme angekuwa yeye angefanya nini ama angekuwa na mkakati gani ili kuondoa hayo mapungufu. Kama atashindwa kuwapa mawazo yake hapo ndipo ninaweza kusema kwamba hakuwa na sababu ya kuelezea mapungufu, maana ili kitu kionekane kina mapungufu, lazima mtoa kasoro aseme ingekuwa hivi ama vile basi ingekuwa mswano. Then watu wanakaa chini na kuangalia kama wanaweza kurekebisha ama kuchukua hayo mawazo yake.
Siyo kila ushauri lazima ukubaliwe, bali kuna mwingine unaweza kuwa mgumu kuutekeleza kulingana na mazingira, muda/wakati na pia inawezekana ukawa unapingana na mambo mengine ya msingi yaliyo ndani ya chama.
Kwa matazamo wangu Mwanakijiji ametengeza haoja hii kindharia zaidi,practicaaly haiwezekani halafu ana ndoto ambazo haziwezi kutokea mwaka huu.Sisi ndio watu tulioko field tunatambua jinsi hali ilivyo huku.Lakini pili Mwanakijiji analeta siasa za Marekani ambao wenzetu walianza siasa tangu miaka ya 1800 huko.Siasa za eti kila mgombea Urais au Ubunge awe na sera zake.wagombea wenyewe wa Urais wako wapi? siku zote kila chama kimekuwa na mgombea mmoja,wakijitokeza hao wengine huwa wanajifurahisha tu lakini huwa from the beggining inajulikana kabisa nani atakuwa mgombea Urasi.Kwa wagombaea Ubunge nako eti wawe na sera zao,nani kakwambia siasa zetu za Tanzania wapiga kura wanaangalia sera?ni wangapi wanaongalia sera,sijui itikadi,hivi vitu tunavifanya for formalities tu lakini kiukweli wapiga kura wengi wala hawana mpango wa kuangalia sera.Sasa hizi hoja za wagombea kushindanishwa na sera kwa miaka hii wala haina mashiko.Kwanza wagombea wenyewe tunao?ni majimbo mangapi ambapo watu wanpita bila kupingwa?ni machache sana yanyokuwa na mgombea zaidi ya mmoja.Kwa kweli mi bado wala sijamwelewa rafiki yangu mpenzi Mwanakijiji.
Haya mawazo ya kushindwa ni mabaya zaidi kuliko inavyofikiria rafiki yangu, ni mawazo ambayo yanajikatisha tamaa yenyewe. Kama wapo wengi ambao wamepokea hii ndani ya Chadema wakiwa na mawazo haya, basi kweli tuna tatizo kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria.
Mwanakijiji bana....LMAO
NN acha kutuharibia mada yetu..Kwanza mpaka sasa we mtoto bado hujalala tu.Unangoja nini?
Sijalala nakungoja wewe....kwani umeenda wapi?
We tafadhali,unaningoja mimi?excuse me..
Hongera sana M.M.M kwa uchambuzi makini uliotulia. Mungu akubariki kwa kazi nzuri unayoifanya kuamsha taifa hili letu. UBARIKIWE!
Wakati karibu tupate Uhuru, Mangi Thomas Mareale alikwenda Marekani akasema hatujajitayarisha vizuri, ni vema tusibirishe siku ya Uhuru. Sote tunashukuru kwamba Mwalimu hakukubaliana naye.
Mwaka kesho tunafikisha miaka 50 tangu tupate Uhuru. Hali si nzuri, tunataka kubadilisha uongozi kwa dhati. Kubadilisha kabisa chama tawala. Sasa MMKJ anasema hatujafikiria vizuri. Umekuwa Mangi Mareale tena?
Chadema imejitayarisha vizuri sana. Si ya jana. Ina viongozi wanaoweza kabisa kazi ya kusimamia serikali.
Utasemaje lazima wapange hata mawaziri wao kwanza?
Nani anafanya hivyo? CCM?
Wananchi wanajipanga chini ya uongozi wa Chadema. Do not water down their enthusiasm.
Well, kuna wengine wangeweza kusema kuwa tungechelewa kidogo kupata uhuru.. na wakajenga hoja ikaeleweka.
Ooh no.. sijasema hatujafikiria vizuri; nasema tutafanya makosa kama hatutafikiria implication hiyo.
Utaona katika maandishi yangu yote, sikugusa hata sehemu juu ya uwezo wa viongozi wa Chadema. Believe me, ningetaka kugusa huko wala tusingeelewana kabisa. Kwa makusudi kabisa kwa miaka yote hii minne sijaingia kugusa juu ya Uongozi wa Chadema, ningewajeruhi zaidi. Ninajitahidi kuchagua maneno yangu na mada vizuri.
Absolutely! Yaani mtu anataka Urahisi na hajui atapata wapi Mawaziri, Wakuu wa Mikoa. Usiniambie unataka akishaapishwa ndiyo aanze kuuliza nani ashike nafasi gani? That would be the most irresponsible government ever to have come to power. Wasipoweza hata kuziba nafasi za kisiasa za Uwaziri, Unaibu, Ukuu wa Mkoa.. wataweza kweli kuziba za ukuu wa wilaya, Ukurugenzi n.k Au utasema watawataka wateuliwa wa Kikwete waendelee kukaa madarakani wakati Chadema inatafuta watu wa kujaza nafasi hizo?
Absolutely! You didn't know this?
ooh no sir, I'm not watering it down.. I'm just watering it a little bit more.