CHADEMA 2010: Kutoka "Hapa" mpaka "kule"

Mwanakijiji said:
Simba au Chui anapomrukia mnyama kumrarua haendi kung'ata mguu au mkia. Na tena haendi kurukia minofu ya paja au mbavu. Anaenda kwa shingo kwanza ili kumzuia mnyama yule kupumua na kuzuia damu kwa kubana mshipa unarudisha damu kutoka kwenye ubongo (jugular vein).

Mwanakijiji pamoja na mawazo yako mazuri, napinga kitendo chako cha kuwashauri CHADEMA wakimbilie kunga'ta kwenye Jugular Vein ambayo inarudisha damu chafu toka kwenye ubongo. Mimi nashauri wanga'te kwenye shingo hiyo hiyo, lakini wanga'nga'nie kwenye Carotid Artery kwani mishipa hii inapeleka damu safi yenye oksijeni na sukari (glucose) kwenye ubongo, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ubongo. Kwa hiyo kama wataweza kunga'ngania hiyo shingo na kukamata Carotid artery basi huyo mnyama atakuwa kitoweo badala ya dakika chache tuu.......LOL
 
Mwanakijiji Bravo sana.
Ni article ndefu lakini nimejitahidi kuisoma yote ingawa kwa kuungaunga maana na kazi za watu pia lazima zifanyike. binafsi nimeipenda kwa sababu pamoja na kuikosoa Chadema lakini pia umetoa mapendekezo mazuri ambayo kama yakifuatwa yanaweza kubadilisha siasa za Tanzania.
Kuna vitu vingi vimenifungua macho binafsi, kuna wakati nilisoma Sera za Chadema na kimoyomoyo niliona kama zina elea elea sana, haziko deep.

Kwa vile Dr. Slaa ameshasoma na amekiri kuzifanyia kazi, ni imani yangu kwamba kweli atazifanyia kazi na si kuziweka kwenye droo kama viongozi wengi wafanyavyo. Nakubaliana nawe sasa kwamba Chadema lazima iondokane na sera ya Upinzani wa kulalamika na watengeneze sera ya Utawala.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nimekukubali... mabo mengi uloandika yalikuwa kichwani mwangu siku nyingi na hakika ulipogusia UFISADI kuwa adui nambari one mkuu umenigusa sana..Kifupi nitaendelea kukusoma kwani kuna mengi ambayo yapo upande wa pili wa ukuta ambayo wengi hatukuyaona ama tuliyapuuza lakini yana umuhimu mkubwa sana ktk maandilizi ya chama kushika Utawala.
 
Mzee MMKJ

Heshima nyingi tu. Nimesoma kikamilifu bandiko lako na kupata elimu ya kutosha. Siku zote nimekuwa nikikuchukulia kama mtu usiye na subira wala kutambua angalau mchango haba unaotolewa na wenzetu walioamua kujipambanua katika jamii hii iliyozugwa (corrupted) vibaya sana kiasi cha kukubali ufisadi kama sehemu ya maisha. Sasa nimekuelewa kuwa unataka na unaamini katika shari kamili kama njia pekee ya kuikomboa nchi. Huko nyuma sikuamini kwamba kuna mtanzania aliye tayari kwa mhanga wa mapinduzi yenye upeo kamili wa kutokomeza mawakala na mfumo mzima wa ufisadi.

Katika maisha yangu yote tokea nikiwa shule (wakati wa nyerere na Mwinyi) nilishajiaminisha kwamba nchi hii watu wameamua kuishi kwa janjajanja na wizi tu (ilianza taratiibu tokea enzi za JKN na kukomaa kikamilifu miongo ya hivi karibuni). Kutokeza kwa Slaa & co. kukanifanya nianze kuamini katika harakati za kuitingisha system taratiibu kama njia ya hatimaye kubadili mwelekeo. Waweza sema incremental steps hasa kwa kuongeza wabunge makini na majasiri wa upinzani (hata CCM) kuondoa ukiritimba na hatimaye kuifuta sauti ya mafisadi ndani ya chama chao (CCM) na kuwafanya wananchi wajue kuwa kuna namna mbadala ya maisha ya kistaarabu na sio uongo/uzugaji walioaminishwa miaka nenda miaka rudi kwamba ufisadi ni sehemu muhimu ya maisha.

Aidha, baada ya kusoma makala yako nilitamani nikuombe ujitokeze mbele na kuchukua jukumu la kuongoza mapambano, lakini nikakumbuka kuwa kila mtu ana karama yake. (Kwa mfano, mimi binafsi sina uwezo mkubwa wa kupanga mawazo yangu kwa kirefu katika masuala ya umma zaidi ya kufaidi uchambuzi wa wengine!). Ombi kwako sasa ni kutokata tamaa kuwasaidia akina Slaa wafanye kinachotakiwa kwani hata wewe mwenyewe unatambua ujasiri wao wa kuibeba mada ya JF na kuipeleka Mwembe Yanga na kwingineko. Wasingefanya hivyo, wahuni wetu wangeendelea kupuuzia tu haya mambo ya intaneti. Unaweza ukawakosea raha na kudai hawako tayari. Lakini naamini kabisa kama kuna watu wenye kuweza kuyatafsiri mawazo yako mazito kwa vitendo ni akina Slaa na CHADEMA yao. Zaidi yao bado kabisa sijaona wengine.
 
Nia ya MMKJ ni kuipunguzia au kuiongezea nguvu CHADEMA? MMKJ anakubali kwamba CHADEMA inaweza kuing'oa CCM wakati huu au anapinga?

Singependa hata kidogo mchezo wa kuuma na kupuliza.

CHADEMA si kamilifu, lakini CCM imeoza. Kwani wapinzani walioiondoa KANU madarakani, na wale walioiondoa UNIP walisitasita kama anavyotaka tusite huyu mwenzetu? TANU ilipotuongoza kwenye Uhuru 1961 ilisitasita na kusema ngoja tuende kwanza kukutana na Director wa Inteligence? By the way, viongozi wakuu wa UWT watakuwa wanapanga namna ya kushirikiana na Mpendwa wetu Dr Slaa kwa sasa? Slaa anahitaji ulinzi wa CHADEMA.

Ushauri unapotolewa ukichanganywa na hali ya kusita na kupandikiza wasiwasi sio mzuri.

Wenye ushauri mzuri waendelee kuutoa bila kujaribu kupunguza nguvu za wananchi zinazojijenge nyuma ya CHADEMA sasa hivi.
 
Mwalimu Augustino, uamuzi ni mwepesi tu.. Chadema wanaweza kwenda kichwa kichwa kwa sababu wanataka kuingo'a CCM madarakani na wakafanikiwa. Lakini wasipofanikiwa watatamani wangetulia kufikiria kidogo. Mtu aneyesita usimchukulie kama hajui anachofanya, wakati mwingine ni hekima ndiyo inamfanya asite.

Makosa mawili ambayo kwa upande wangu nisingependa Chadema wafanye kwanza ni hamaki na pili kutokutulia. Mtu mwenye hamaki huitikia linapotokea tukio bila kuchukua muda kufikiria sana - mfano wa serikali ya Obama na huyu mama waliyemtimua kazi baada ya kuona clip ya video tu, leo serikali nzima imemuomba radhi- hiyo ilikuwa ni hamaki! Lakini vile vile mtu kutokutulia kufikiria matokeo ya vitendo na maamuzi yake nijambo baya na hasa linapokuja suala la kuongoza taifa.

Yawezekana wewe unapenda CCM iondolewe madarakani haraka na kwa namna yoyote halafu tufikiri consequences baadaye! Mtu mwenye hekima atasita. Si kwa sababu hataki lakini anafikiria implications ya kutoka bila kujali mnatokaje na nini kinafuata badala yake. Ni sawasawa na jengo kubwa ambalo halihitajiki tena. Kwa vile watu hawalitaki wanaamua tu lilipuliwe na kuvunjwa. Wote wanakubaliana kuwa wazo ni zuri. Na wengine wanataka libomolewe kwa haraka kwani linavutia uhalifu n.k n.k

Hatah hivyo, wengine wanasema vipi kuhusu majengo yaliyozunguka jengo hilo, vipi kuhusu vumbi na uchafuzi wa hewa, na wakishalibomoa hayo magofu yataondolewa vipi na kupelekwa wapi. Mimi na wewe tunakubaliana kabisa CCM ni lazima iondolewe madarakani. Wewe unataka iondoke tu bila kujali matokeo yake kwa taifa, jamii na utawala wetu. Mimi natafakari kuwa tukiindoa ni bora tujue kabisa tunataka kufanya nini tusije tukajikuta siyo tu tunaiondoa CCM bali vile vile tunaondoa hata nafasi ya sisi kuingiza tunachotaka badala yake!
 
Vichwa kama cha mm kisipotumiwa kwa tija ni ubadhirifu wa taifa zima. Sio ajabu kisima cha mtu kisimnufaishe mmiliki lakini ikawa ahueni ya majirani na watu kutoka mbali, kama vile nabii asiyeheshimiwa kijijini kwake na mfuga kuku lakini ana utapiamlo Kwashiokor. A very potential asset invisible to the rullers. God bless you MK. You are not loosing the war, there are people who follows up your works and utilise the needful. Sio lazima waseme. Keep it up.:violin:
 
Ahsante sana mkuu. I wish kila mtanzania mwenye mapenzi ya dhati na nchi yake angekuwa member wa Jf na kusoma ujumbe huu. Tunapata mambo mazito sana humu ndani na ni watanzania wachache sana wanaofikiwa na habari kama hizi.
Hongera kwa Chadema kufikia uamuzi huo wa kumteua Dkt. Slaa. Suala kubwa lililo mbele yenu ni kueneza sera yenu kuanzia ngazi ya shina,kata na kuendelea. Wapiga kura wengi ni watanzania waishio vijijini ambako sera yenu bado haijawafikia vya kutosha. Hakika tunahitaji chama mbadala na watanzania wengi tuna matumaini makubwa na Chadema. Rekebisheni kasoro ndogondogo zilizopo na mtapata support ya kutosha.
 
Nimesoma utangulizi na para 1 ya sura ya kwanza na kuishia hapo. Utangulizi wako haujabeba ujumbe unaotaka kutoa - background, problem and significance & recommendations. Ujitahidi kuweka utangulizi mzuri na uwe na executive summary/ abstract kwani wengine hatuna muda wa kusoma kila kitu sisi tunataka 'gist' tu!

Nafikiri lengo kuu la kila chama cha siasa duniani ni kuwatumikia wananchi kupitia serikali wanayouunda. Na kunakuwa na ajila isiyokuwa ya kudumu katika mfumo wa vyama vyingi kama wetu. Waajili ni wananchi na wanaajili wakati wa uchaguzi mkuu kwa vyama kuonesha CV zao, uzoefu wao na waajili wanafuata 'reference' kwa chama ambacho kilikuwa kimeajiliwa. Kwenye ajila unaweza kuajili mtu 'fresh from school' baada ya kuona kuwa ni potential. Sasa nina imani kuwa chama pinzani ni chama tawala mtarajiwa, na chama tawala ni chama pinzani mtarajiwa. Wabunge wa Chadema wamekuwa wenyeviti wa tume za kudumu za bunge, je hawajapata bado uzoefu? Na isitoshe chama cha siasa kikisajiliwa maanake kinaweza kutawala! Na utawala wake utafuata katiba ya nchi!

Umefika wakati tuwe optimistic na sio perssimistic, mbona huko US, UK, Israel, na hata kwa jirani zetu Kenya wanabadilisha vyama, kwa nini nasi tusifanye hivyo?

In short, had I been a peer reviewer of your article, I would have dismissed it outright!!!!!!!
 
well you just did! Ningetaka kuandika article kwa ajili ya peer review nisingeandika hivyo..!
 
Mwanakijiji,
Kuna thread ile nyingine nilikueleza kuwa wamo watu ndani ya CHADEMA ni wasikivu sana. Mmoja wa hao watu ni Dr Slaa. Bila shaka umeliona hili sasa. Nilikuomba pia utimize wajibu wako nawe kama Mtanzania kuandika au kusema kile ambacho ungependa kuona CHADEMA kama chama kinatekeleza ili kuiondoa Tanzania hapa tulipo. Hili umelifanya kwa ufanisi mkubwa kwenye "waraka" wako huu ingawa naamini bado utachangia zaidi.
Sikubaliana sana nawe unapoweka UFISADI kuwa ndio tatizo mama tulilo nalo kwa sasa kama nchi. Hili ni tatizo dogo sana endapo mtu kama Dr Slaa atakuwa Rais. Kagame amechukua muda mfupi tu kupambana nalo na Rwanda sasa hivi inalinganishwa na Nchi za Nordic kwa usafi wa uongozi wake. Shida tuliyonayo kubwa Watanzania ni kutokuwa na sera na mikakati endelevu kwa yaliyo mema. Mwalimu alikuwa mkali sana kwa wala rushwa. Kumbe alikuwa peke yake. Alipoondoka madarakani tu, hata kabla hajafariki, tukaanza kuona kila kitu kinabadilika. Ndani ya CHADEMA kwa sasa simwoni mtu mwingine anayefanana na Dr Slaa na hasa msimamo wake wa wazi kuhusu UFISADI. Dr Slaa peke yake ndiye aliyethubutu kusema mishahara na posho za Wabunge imekaa kifisadi pia.
 
Wildcard, ninaamini Ufisadi ni tishio kubwa zaidi kwa sababu linatufanya tushindwe kushughulikia mambo mengine yanayotokana na sera. Matokeo yake kuna mahali watu hadi kwenye utekelezaji wa sera wanabajeti na ufisadi.. tumefikia mahali pa kujaribu to work "with the system" a.k.a mfumo wa ufisadi.
 
Ndugu Mwanakijiji.
Waraka wako una leta mkingamo wa mawazo kwa piga kura kitu ambacho nia hatari sana labda kama unania hiyo.
CCM ni cha chama ambacho kinamaovu mengi na kunuka ufisadi na inaelekea kuweka Tz sehemu hatari ya kuishi.Sasa itatufaidi nini kwa hicho kubaki na dola tukitoa waraka controversial kuhoji utayari wa Chadema ,je worst scenario Chadema ikinyanyakuwa dola itakuwa mbaya kupita tunaishi nayo sasa chuni ya CCM?

Tatizo ni kuwa you don't know the art of war and you're not war time kind of guy.Mfano mzuri ni CCJ ,najua tunazungumzia Chadema kwa sasa ila tunatumia makosa yaliotokea kwa CCJ kuepuka yanayotaka tokea kwa Chadema.

Kujua nini cha kufanya na muda gani (timing) ndio kitu cha muhimu ktk dunia ambayo time ni unit muhimu.Kuna timining zilikosekana ktk CCJ na kukosa kilichokosa, hii inatokana na kuishi ktk ulimwengu wa dream kuwa kila kitu kiwe perfect na mambo yote yataenda perfect huku kutotilia mkazo other facts and reality which may affect the trend .

Sera,itikadi,mikakati mizuri n.k vinahitajika sana,lakini je itatufaidi nini tukiwa na hivyo vyote vyema na vizuri ila tusichukue dola (chadema) tutakuwa tofauti gani na CCJ.

Nachotaka kusema cha msingi ni kupata ridhaa ya wananchi kupitia kura.Na kila kula ya mwaninch inauzito sawa.So waraka wowote kama unania njema hautakiwi kuwa controversial ili lengo la kupata kura na dola kutimia.

Hotuba nzuri ni ile wasilikizaji/audience wanailelewa,haina maana hata kidogo kama itakuwa inaujumbe muzuri wasiuelewe ama ukaeleweka vibaya.Kuna waTz kama mil.40 say mil 10 wanapiga kura wangapi asilimia ngapi watakao soma waraka wako wataelewa kuwa una maanishisha Chadema haiko tayari na ni bora ikaendelea CCM yasije tokea ya vita kama inchi jirani kama viongozi wa CCM wanavyosema sku zote za uchaguzi.

Ok kwa kifupi haitajiki kusema kuwa mwenye kuelewa ataelewa atakavyoelewa mind kila kura ina uzito sawa na muhimu.Wana inch wanatakiwa kusikia wanachotaka kusikia ili kutoa kura ya ndio ,mwana inch asilimia kubwa hawako tayari kusikia ulio orodhesha hata kama ni muhimu (yes good stuffs)

So wakati unatoa ushauri wako mzuri angalia usitutolee na ushindi wetu kwa maana sera zinaweza kuandaliwa yes kabla ya kuingia madarakani ila can be in under tone ila propaganda za chama wanainchi wanazotakiwa kusikia ndio za msingi,usi dharau umoja wa watu ktk kutaka kuingoa CCM ambao utatoa ushindi, na ukasema tukazane what next …tukikazana na what next na ushindi usipatikane kama CCJ(nikuwa hiari tayari kuwa mwanachama) itatufaidi nini?

Hakuna ubaya na ni muhimu kujua what next kama ulivyo bainisha ila isi athiri ushindi these two thing must be handled with nice and good timing.Avoid controversial statement unless you meant to do that.
 
Nakubaliana nawe kuwa sasa tuna-ubajeti ufisadi pia. Na sio hivyo tu, ufisadi ulitupatia Rais tuliyenaye sasa na yeye nadhani kwa kujua alipatikana kwa njia ile akateua mafisadi wengi tu serikalini na ndani ya CCM taifa. Nikwambie tu jambo moja: OVU lolote lile huwa halina mizizi ya maana hivyo kuling'oa ni rahisi tu. Uliona ilivyokuwa rahisi kumng'oa Lowasa.
 
Mwalimu Augustino, uamuzi ni mwepesi tu.. Chadema wanaweza kwenda kichwa kichwa kwa sababu wanataka kuingo'a CCM madarakani na wakafanikiwa. Lakini wasipofanikiwa watatamani wangetulia kufikiria kidogo. Mtu aneyesita usimchukulie kama hajui anachofanya, wakati mwingine ni hekima ndiyo inamfanya asite.

Makosa mawili ambayo kwa upande wangu nisingependa Chadema wafanye kwanza ni hamaki na pili kutokutulia. Mtu mwenye hamaki huitikia linapotokea tukio bila kuchukua muda kufikiria sana - mfano wa serikali ya Obama na huyu mama waliyemtimua kazi baada ya kuona clip ya video tu, leo serikali nzima imemuomba radhi- hiyo ilikuwa ni hamaki! Lakini vile vile mtu kutokutulia kufikiria matokeo ya vitendo na maamuzi yake nijambo baya na hasa linapokuja suala la kuongoza taifa.

Yawezekana wewe unapenda CCM iondolewe madarakani haraka na kwa namna yoyote halafu tufikiri consequences baadaye! Mtu mwenye hekima atasita. Si kwa sababu hataki lakini anafikiria implications ya kutoka bila kujali mnatokaje na nini kinafuata badala yake. Ni sawasawa na jengo kubwa ambalo halihitajiki tena. Kwa vile watu hawalitaki wanaamua tu lilipuliwe na kuvunjwa. Wote wanakubaliana kuwa wazo ni zuri. Na wengine wanataka libomolewe kwa haraka kwani linavutia uhalifu n.k n.k

Hatah hivyo, wengine wanasema vipi kuhusu majengo yaliyozunguka jengo hilo, vipi kuhusu vumbi na uchafuzi wa hewa, na wakishalibomoa hayo magofu yataondolewa vipi na kupelekwa wapi. Mimi na wewe tunakubaliana kabisa CCM ni lazima iondolewe madarakani. Wewe unataka iondoke tu bila kujali matokeo yake kwa taifa, jamii na utawala wetu. Mimi natafakari kuwa tukiindoa ni bora tujue kabisa tunataka kufanya nini tusije tukajikuta siyo tu tunaiondoa CCM bali vile vile tunaondoa hata nafasi ya sisi kuingiza tunachotaka badala yake!

hili la kuhamaki na kutotulia umejifunza kutoka CCJ nini? Ninawaza, inakuwaje haya mawazo yote yanakuja sasa ivi na hukuwauliza watu wa CCJ? Just curious!
 
hili la kuhamaki na kutotulia umejifunza kutoka CCJ nini? Ninawaza, inakuwaje haya mawazo yote yanakuja sasa ivi na hukuwauliza watu wa CCJ? Just curious!

What it if that is the case??
Huwezi kufurahia nia njema aliyo nayo kwa CHADEMA kiasi cha kutotaka warudie kosa mpaka uulize kwanini anamzimia jirani moto wake wakati kwake kuliungua?
 
MMKJ.

Nakupongeza kwa uchambuzi makini. hakika nimetumia muda wa kutosha kisoma document yote, nakubaliana na wengi wanoiangalia document hii in a positiveway. Changamoto kwa Chadema zipo na ni muhimu zitolewe ili pale ambapo wanaweza kurekebisha, wafanye hivyo siyo kitu kibaya.

Pg 52 umeongele kwa kirefu vipimo vya utendaji (KPI's). hiki ni kitu muhimu kwa yeyote anayetaka kufikia mafanio fulani, kwa nchi yetu hili halijulikanai kabisa, tunajiendesha tu bila mwelekeo.

Pg 55. Kuwashungulikia viongozi mafisadi hasa waliopita. Hili nahisi kama lilitakiwa libaki kama WAZO kwenye moyo wa Dr Slaa, vinginevyo litamlete maadui wengi sana na hata baadhi ya wapiga kura wataondoka kabisa kwenye njia yake. Nchi yetu haijafikia hivyo viwango vikubwa namna hiyo vya uelewa na uwajibikaji. Watanzania wengi sana wameshasahau kilichotokea mpaka balali akaenda kufia ulaya. Kwa hiyo hili wazo likitoka watu watamwita chinjachinja.

Pg 59. Kutangaza majina ya wtu watakaochukua Uwaziri mkuu na uspika endapo watanzania watakubali kuwapa Chademaa wabunge wengi. Weledi wa mambo ya siasa watusaidie hapa ila kwa upeo wangu sioni kama kuna shida yoyote, naona faida zaidi kuliko shida pengine kwa sababu ya namna navyoliangalia.

Kutembelea Viongozi wa mashirika ya umma.
Sina hakika kama hili ni jambo rahisi hasa ukizingatia mfumo wa upatikanaji wao na siasa zetu za viongozi wa mashirika haya kujipendekeza. Dr Slaa anaweza kuomba nafasi ya kumwona mkurugenzi wa Tanesco na sipate hiyo nafasi mpaka uchaguzi unaisha.

Kupata Ulinzi.
Hili nalipinga kwa sababu moja kubwa, Ukitoa hiyo room kwa watu wa serikali basi ndiyo CCM watakuwa wamekubandika tape recorder mgongoni ya kujua kila unachofanya. Labda nimefinya uelewa wangu juu ya hili, niko tayari kuelimika zaidi.

Ninao mchango zaidi ila kwa sasa naomba utambue kuwa nimeupenda waraka huu.

Respect Mkuu.
 
Kazi nzuri sana hongera mkuu! Kwa jinsi nilivyomsikiliza Mnyika jana wakati akihojiwa katika kipindi cha kurunzi yetu kinachorushwa na Mlimani TV, na hakika mambo haya kama watayapata na naamini wameshayapata, watayafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom