CHADEMA 2010: Kutoka "Hapa" mpaka "kule"

CHADEMA has to pay for this service ila we are not profit-making org. Sorry but it is excellent job for benefits of all Tanzanians. Kodus MMKJ
 
Nimependa wazo la mgombea kuwa na ajenda yake, inawezesha wananchi kupima mawazo ya kiongozi wao kuhusu changamoto zilizopo. Nimependa pia 'mapambano dhidi ya ufisadi kuwa' ajenda kuu ya Dr Slaa. Mimi ningeongeza 'watanzania hawawezi ku-afford miaka mingine mitano ya uongozi legelege wa Kikwete'. Hii ilimsaidia sana Obama pale aliposisitiza kuwa ' Americans could not afford another five years of Bush's failed leadership'. Of course tayari alishaeleza kuwa MaCain=Bush. Mara nyingi huko nyuma wagombea wa upinzani wanaonyesha mapungufu ya CCM bila kusisitiza mapungufu binafsi ya viongozi. Hili la Kikwete ni jepesi na Dr Slaa alivalie njuga. Huyu mtu hawezi kuwa kiongozi, period.
 
Mimi napenda kumpongeza Dr. W Slaa kwa uamuzi wake. Mheshimiwa utashinda tu. Mungu akupe nguvu watanzania wote wako nawe. natumaini hata wale waliochimba barabara jana wako pamoja nasi kwani hakuna bingwa wa shida, kila siku watoto wetu wagongwe na magari kisa viongozi wasio sikia kilio cha walala ho. hivi angegongwa mtoto wa kule ostebay, kwa akina vigogo si tuta lingewekwa hata kama ni usiku wa manane?

Watanzania wengine waje Moshi waone matunda ya Chadema, matuta si ya kuandamana ni wajibu pale inapoonekana inafaa, lami si za kuuliza zinawekwa kulingana na bajeti, hakuna ujanja ujanja, tukiushtukia tunawabana wanatupa chetu tunasogeza gurudumu la maendeleo. Pia si kwamba tumefanikiwa sana kwani bado CCM wanatubana sana lakini tunataka mwaka huu tuwaondoe wote tujipange Chadema au CUF ili bajeti zetu zioane na maendeleo sio kunenepesha familia za vigogo tu.Kidumu chama cha chadema.
 
Mwanakijiji
Kwanza nikupongeze kwa kutenga muda wako na kuja na hii Hoja.Pili nikuombe radhi kwanza kwa nitakayoyasema ,nimaomba radhi kwa kuwa wewe ni rafiki yangu ninayekupenda sana.kwa ujumla kabla ya kuanza kuchambua kipengele kwa kipengele mpaka pale nilipofikia kusoma nyaraka hii.

Kwa ujumla nimegundua vitu kadhaa kuhusu hoja hii.
1. Huna dhamira ya dhati kuhusu CHADEMA.Mambo mengi uliyoandika humu ni kuponda tu kana kwamba CHADEMA haijafanya lolote..Nikubaliane na wewe kwamba sehemu nyingi uko sahihi kuhusu CHADEMA lakini why now wakati tayari muda umeshakwenda zimebaki siku chache tu kuanza kampeni?ulikuwa wapi kueleza mapungufu haya siku zote hizo?WHY NOW?Na mbona mapugufu tu hivi CHADEMA haina Strengths zozote?Naomba niungane na wale wanaohisi huenda wewe ukawa ni CCM au Usalama wa taifa kwa staili ya aina yake,na wale wanaohisi wewe sio mpiganaji mwenzetu ..Unauma huku unapuliza

2.Unajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa CCJ ionekane ndio chama mbadala baada ya Uchaguzi Mkuu

Huu ndio mtazamo wangu wa ujumla.Niko na wewe kipengele kwa kipengele..stay tuned.
 
MMK,
Asante sana kwa very comprehensive and Constructive analysis.nimesoma yote na nitaendelea kuifanyia analysis hatua kwa hatua, na kuona hatua stahiki zinachukuliwa. Naomba uendelee kutushauri tunavyoendelea na maandalizi yetu. Tanzania ni yetu wote, na Input ya kila mmoja wetu inaweza kututoa tulipo na kwenda tunakotaka. Thanks a lot.


Jemedari.. nyuma yako niko tayari kufuata! Utuongoze vitani!
 
Mwanakijiji
Kwanza nikupongeze kwa kutenga muda wako na kuja na hii Hoja.Pili nikuombe radhi kwanza kwa nitakayoyasema ,nimaomba radhi kwa kuwa wewe ni rafiki yangu ninayekupenda sana.kwa ujumla kabla ya kuanza kuchambua kipengele kwa kipengele mpaka pale nilipofikia kusoma nyaraka hii.

Kwa ujumla nimegundua vitu kadhaa kuhusu hoja hii.
1. Huna dhamira ya dhati kuhusu CHADEMA.Mambo mengi uliyoandika humu ni kuponda tu kana kwamba CHADEMA haijafanya lolote..Nikubaliane na wewe kwamba sehemu nyingi uko sahihi kuhusu CHADEMA lakini why now wakati tayari muda umeshakwenda zimebaki siku chache tu kuanza kampeni?ulikuwa wapi kueleza mapungufu haya siku zote hizo?WHY NOW?Na mbona mapugufu tu hivi CHADEMA haina Strengths zozote?Naomba niungane na wale wanaohisi huenda wewe ukawa ni CCM au Usalama wa taifa kwa staili ya aina yake,na wale wanaohisi wewe sio mpiganaji mwenzetu ..Unauma huku unapuliza

2.Unajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa CCJ ionekane ndio chama mbadala baada ya Uchaguzi Mkuu

Huu ndio mtazamo wangu wa ujumla.Niko na wewe kipengele kwa kipengele..stay tuned.


you are more than wrong! CCJ siyo mama yangu! sina mapenzi kwa chama kiasi cha kupoteza utimamu wangu. Kama imekukwaza rafiki yangu mpendwa basi kusudio langu litakuwa limefanikiwa; lakini ni lazima utoke kwenye kukwazwa na kwenda kwenye kuukumbatia ukweli na kuutumia kwa ufanisi. Hata kidonda ili kitibiwe lazima kisafishwe kwanza! Believe me its not pretty.

Chadema has my tentative support pending the issuing of their manifesto.
 
mmmh.. pa kuitana waongo!?? haya ngoja nipige magoti na kuabudu katika altare ya waipambao sifa za kufurahishana. Kama ndiyo watawala wetu wengine mnatupa dalili hizi naogopa...

Pole dia.Ila kwa jinsi nilivyokusoma kwenye waraka wako naona kama sikuelewi vile.
 
Ni uchambuzi mzuri saana, uliojaa ukweli,,,,ni jambo jema viongozi na mashabiki wa Chadema wakauchukua kama changamoto, na kufanyia kazi kwa haraka kama wana nia ya kufanya mabadiliko ya kweli,,,,,
 
Nimeprint na kusoma, naanza kumwelewa Mwanakijiji maana hoja zake zinamshiko,

Hongera Dr Slaa kwa kusoma nakukubali ushauri, viongozi wengine wa CHADEMA wafuate njia ya Dr Slaa.
 
Kuna sehemu Mwanakijiji anasema ili CHADEMA Itoke kwenye Upinzani nakuwa mtawala basi ibadilishe nadharia zake,falsafa na muundo.Hivi haya yanawezekana kwa siku chache zilizobaki?itawezekanaje?
 
Asante sana Mwanakijiji kwanza kwa uzalendo wako na kwa kutumia muda wako adhimu kutengeneza waraka huu.Nakubaliana na wewe na mengi kama siyo yote uliyoyaeleza katika waraka wako lakini tatizo langu kubwa ni timing ya waraka wako,kwanza unaweza kumpa adui katika hili namaanisha CCM silaha ya kuibomoa CHADEMA lakini pia haikipi CHADEMA muda wa kutosha wa kufanya masahihisho pale inapobidi kabla ya muda wa kampeni kuanza au pengine kabla ya October 31.
 
Kwa mambo yaliyo tokea mwaka 2005-2010 kama vyama vyetu vinge jiandaa na kujiimarisha mapema zaidi basi leo hii tunge kuwa tuna subiria kuingiza chama kingine madarakani. Uchaguzi ungekua tu wa kuhalalisha mshindi. Tatizo sidhani au sijui Chadema au vyama vingine vime jipangaje kwa vile mimi siyo party insider. Anyway nita toa mawazo yangu kadri ya uwezo wangu.

1. Kwanza hongera kwa Chadema. Hakika wamemteua mtu ambae ana umaarufu na personality wa kuweza kushindana na Kikwete. Pia nampongeza Mbowe kwa sababu zozote alizo kuwa nazo za kuto kugombea safari hii maana kaonyesha mfano kwamba mwenyekiti wa chama si lazima awe mgombea kila wakati. It is about doing what's best for the team na hakika ndugu Slaa ndiye anayefaa kugombea kiti hicho cha uraisi. Hiyo ndiyo marks ya kwanza ninayo ipa Chadema. Natumai hata waki bahatika kushinda uraisi vyeo vita pewa kwa kuangalia uwezo wa mtu na ni wapi anapo faa.

2. Mfano walio onyesha kwenye kuteua nafasi ya uraisi natumai ndiyo huo huo watakao fuata katika kuteua wagombea wao wa ubunge. CCM kina advantage moja nayo ni umaarufu wa chama na mizizi ambao ime jikita mpaka kwenye sehemu za ndani za nchi. Njia pekee ya kuondokana na disadvantage hiyo ni kuteua watu ambao wana utashi wa uongozi, upeo wa mambo na falsafa za maendeleo. Uteuzi mmoja wa ubunge ambao binafsi nimeufurahia ni wa John Myika kwa Ubungo.

3. It's a race against time. Hamna muda wa kupoteza. Natumai chama kilisha jipanga vizuri kabla ya hapa. Sasa ni wakati wa kuwa mwagia wananchi mvua za hoja na mahubiri ya maendeleo. Njia nzuri ya kufanya kampeni ni kupitia grassroots. Hakikisheni watu wanapewa ujumbe na majirani zao au ndugu zao au wafanyakazi wenzao ambao ni wanachama wa Chadema au wakereketwa. Mtu hupokea zaidi ujumbe ukitoka kwa mtu wa karibu.

4. Nashauri mgombea awe na kauli mbiu yenye hoja nzito ambayo wananchi wanaweza kushika na kuelewa kirahisi. Ujumbe ni kila kitu kwenye kampeni. After all "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" ilimfikisha Mheshimiwa Kikwete ikulu.

5. Endesha kampeni ambayo utajivunia. Natumai mheshimiwa hauta kuwa wale wale. Onyesha mfano tofauti. hata kama ukishindwa tayari wapenda maendeleo tuna kupongeza kwa hatua uliyo ichukua. Nime furahia uteuzi wako siyo kwa sababu mimi ni Chadema bali kwa sababu naamini wewe ni mgombea tofauti na wengine na natumai utazidi kuji tofautisha na wanasiasa wale wale wenye uozo ule ule.

6. Tumiane vijana kwenye uchaguzi huu. Siyo katika kugombea nafasi mbali mbali tu bali hata kwenye kusaidia kwenye shughuli nyingine za kampeni. Hakuna nguvu kama nguvu za vijana na hakuna mgombea wa uraisi anaye weza kushinda bila support ya vijana. Ndiyo maana hata raisi ali sema hahitaji kura ya wafanyakazi lakini kamwe hawezi kuwa ambia hivyo vijana haswa wale wasomi.

7. Recruit, recruit, recruit! hatuangaliii 2010 tu bali kwenda mbele. Chama chochote kina hitaji vijana wenye vipaji na upeo kusonga mbele. Natumai chama chenu kina jitahidi kutambua vipaji mbali mbali na kujaribu kuwaingiza kwenye system ya chama. Haitoshi tu kuwa na Zitto na Mnyika, bado wengi zaidi wana hitajika kuleta mabadiliko ya kweli. Uhai wa Chadema una tegemea vijana hawa.

8. Vijijini, vijijini, vijijini! Msi sahau wakura wengi zaidi wapo wapi. Ukweli ni kwamba kura nyingi zipo vijijini na siyo mijini na huko ndipo upinzani unapo puuzia. Vyama vingi vya upinzani vime jikita mijini wakati asilimia karibia 80 ya Watanzania ni wakulima. It is a simple matter of knowing where most the votes are. Huko ndipo CCM walipo walipo wazidi kete kwa sana.

9. Lugha! Natambua kuwa wewe msomi na labda pia mngependa kampeni yenu iendeshwe na wasomi ila tambueni hali ya wananchi wenu walio wengi. Nikisema lugha simaanishi tu kiswahili bali pia kuongea na wananchi kwa njia ambayo wata jihisi wao wapo level moja na nyinnyi. Nime gundua kuwa wasomi wengi ama kwa kujua au kuto kujua huongea na watu wa kawaida kwa hali inayo ashiria majivuna na majigambo. Angalieni sana lugha mtakayo tumia.

10. Leave everything on the ring! Msikate tamaa hata hali ikiwa ngumu. Tumieni njia zote zilizo halali, fanyeni kila liwezekanano mpaka pale kipenga cha mwisho kita kapo lia. Kuna watu wengi wata wakatisha tamaa, kuna matokeo mengi yata wakatisha tamaa na kuna propaganda nyingi zita wakatisha tamaa. Nyie fanyeni kazi yenu mkitambua mmebeba matumaini ya Watanzania mabegani mwenu.

Mimi siyo mwana Chadema ila ningeweza ninge shiriki directly kwenye kampeni zenu. Kwa sasa naweza tu toa ushauri wangu na mawazo yangu. Nakutakia kila laheri Mheshimiwa Slaa. I hope the best man wins this time around. Mungu akipenda mwishoni mwa mwaka nita kuwa nakuita Mr. President.
 
Kinyamana...

Nimefikiria kwa kina timing..

a. CCM hawawezi kufanyia kazi jambo hata moja lililomo humu kwa sababu kwa CCM vita dhidi ya ufisadi hawaiangalii jinsi inavyopaswa kuangaliwa hivyo hawawezi kubadilisha mfumo ambao umewaweka na kuwadumisha madarakani.

b. Kwa vile Chadema bado ina vikao muhimu vinakuja na wako rahisi kujiorganize naamini wanaweza kabisa kujipanga upya na kutumia hiii kama nyoongeza ya kile ambacho wanakipanga kukifanya.

c. Chadema kama chama cha siasa kinatakiwa kiwe tayari ku adopt na kuadapt.. chama ambacho kiko rigid kama CCM ni vigumu sana kuweza kushika nafasi ya uongozi. Nimependa majibu ya Dr. Slaa kwa sababu yanaonesha ukomavu wa kuelewa ni wakati gani kupinda na wakati gani kuvunja.

d. Kwa mfano, wakitoka kudhania kuwa "mwanakijiji anaandika kwa sababu hakipendi Chadema, au anataka kutubomoa" watakosa pointi kubwa iliyopo. Ni lazima "watoke hapa" na wawe tayari kwenda kule.. muda wao na nyenzo wanazo..

e. Of course, kuna mambo ambayo nimeyaandika yenye implication ya muda mrefu zaidi katika chama. Na mengine sikuyaandika kabisa kwa sababu they are more dramatic.. haya nitawaandikia pembeni.
 
MMMK mara zote tukiingia ulingoni/uwanjani tunapunguza maswali tunaangalia sana kwenye majibu.

Huwezi kutunga sheria ukiwa uwanjani sasa hivi mpira umeanza tuache theory tutekeleze mambo kwa vitendo
 
MMMK mara zote tukiingia ulingoni/uwanjani tunapunguza maswali tunaangalia sana kwenye majibu.

Huwezi kutunga sheria ukiwa uwanjani sasa hivi mpira umeanza tuache theory tutekeleze mambo kwa vitendo


sasa ucheze tu huku sheria hukubaliane nazo? Wakati mwingine ushindi hutegemea jinsi wewe mwenyewe unavyocheza na kujipanga.. ndio maana kuna formations na mikakati ya kushambulia.. siyo unacheza unabutua tu alimradi mpira unapigwa pigwa.. Utageuka kuwa North Korea kwenye kombe la dunia.
 
Mwanakijiji
Kwanza nikupongeze kwa kutenga muda wako na kuja na hii Hoja.Pili nikuombe radhi kwanza kwa nitakayoyasema ,nimaomba radhi kwa kuwa wewe ni rafiki yangu ninayekupenda sana.kwa ujumla kabla ya kuanza kuchambua kipengele kwa kipengele mpaka pale nilipofikia kusoma nyaraka hii.

Kwa ujumla nimegundua vitu kadhaa kuhusu hoja hii.
1. Huna dhamira ya dhati kuhusu CHADEMA.Mambo mengi uliyoandika humu ni kuponda tu kana kwamba CHADEMA haijafanya lolote..Nikubaliane na wewe kwamba sehemu nyingi uko sahihi kuhusu CHADEMA lakini why now wakati tayari muda umeshakwenda zimebaki siku chache tu kuanza kampeni?ulikuwa wapi kueleza mapungufu haya siku zote hizo?WHY NOW? Na mbona mapugufu tu hivi CHADEMA haina Strengths zozote? Naomba niungane na wale wanaohisi huenda wewe ukawa ni CCM au Usalama wa taifa kwa staili ya aina yake,na wale wanaohisi wewe sio mpiganaji mwenzetu ..Unauma huku unapuliza

2.Unajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa CCJ ionekane ndio chama mbadala baada ya Uchaguzi Mkuu

Huu ndio mtazamo wangu wa ujumla.Niko na wewe kipengele kwa kipengele..stay tuned.

Mkuu GS,

Mtu anaekueleza mapungufu yako ni mtu mzuri sana na anakutakia mema, kuliko yule anayekuambia sifa nzuri (strengths) ambazo zinaweza kukuvimbisha kichwa na hatimaye ukabweteka ukijua kwamba umekamilika na kumbe kuna wengine waliokamilika zaidi. Siku ukija kupambana nao wanakushinda kirahisi na baada ya hapo unaanza kujuta.

Hiyo kazi ya Mwanakijiji haijachelewa, siku bado zipo, bado kuna muda wa kuyafanyia kazi hayo mapungufu. Unajua wakati mwingine mtu anaweza asijue apeleke wapi mchango wake wa mawazo maana hana uhakika kama mchango wake huo utakubalika ama kupokelewa vipi. Kwa hiyo nina imani kwamba kwa wadhifa/madaraka aliyo nayo Dr. Slaa na kwa kuwa sasa anapeperusha bendera ya CHADEMA, basi atakaa chini na kuchambua kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani.

Sijapitia hiyo kazi ya Mwanakijiji, lakini kama kuna criticisms ambazo ameziweka humo, basi mpeni nafasi aseme angekuwa yeye angefanya nini ama angekuwa na mkakati gani ili kuondoa hayo mapungufu. Kama atashindwa kuwapa mawazo yake hapo ndipo ninaweza kusema kwamba hakuwa na sababu ya kuelezea mapungufu, maana ili kitu kionekane kina mapungufu, lazima mtoa kasoro aseme ingekuwa hivi ama vile basi ingekuwa mswano. Then watu wanakaa chini na kuangalia kama wanaweza kurekebisha ama kuchukua hayo mawazo yake.

Siyo kila ushauri lazima ukubaliwe, bali kuna mwingine unaweza kuwa mgumu kuutekeleza kulingana na mazingira, muda/wakati na pia inawezekana ukawa unapingana na mambo mengine ya msingi yaliyo ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom