CHADEMA 2010: Kutoka "Hapa" mpaka "kule" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA 2010: Kutoka "Hapa" mpaka "kule"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 22, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  chadema2010.png

  YALIYOMO
  UTANGULIZI
  HAPA
  SURA YA 1: Kutoka Upinzani kueleka Utawala
  Nani anataka kutawala? … Uk. 5

  SURA YA 2: Kushika madaraka ya nchi
  Kutawala si si lele mama................Uk. 8

  SURA YA 3: Mfumo na Muundo wa Chadema
  Tatizo lile lile?..................... Uk. 11

  SURA YA 4: Chadema na historia ya Mapambano dhidi ya ufisadi
  Mashujaa wako wapi? ………………Uk.18

  SURA YA 5: Chadema na chuki dhidi ya CCM
  Chuki pekee haitoshi……….Uk. 27

  SURA YA 6: Chadema na ujumbe wa matumaini
  Nani atapiga mbiu ya vita...Uk. 31

  SURA YA 7: Mahusiano ya Itikadi, Sera, na Ilani za chama cha siasa
  Kujua mambo ya msingi………………….Uk. 35

  SURA YA 8: Sera za Chadema kuelekea uchaguzi mkuu-
  Ni sera au ilani?........Uk. 42

  KULE

  SURA YA 9: Tulipo “hapa” na tunakokwenda “kule”
  Tutapiga kambi au tutaondoka?............Uk. 50

  SURA YA 10: Kuleta Mapinduzi Baridi
  Kutangaza wagombea Urais, Uwaziri Mkuu na Spika….Uk. 58

  SURA YA 11: Kutoka “hapa” mpaka “kule”
  Ushindi huletwa, hauji wenyewe………….Uk. 64

  NENO LA MWISHO……………………...Uk. 69

  K[FONT=&quot]wa heshima ya wale mashujaa wetu ambao juu ya mabega [/FONT][FONT=&quot]yao[/FONT][FONT=&quot] nasi twasimama[/FONT]​

  UTANGULIZI

  Historia ya maisha ya mwanadamu tangu uumbaji wake ni historia ya kuhama. Kutoka utoto kuelekea uzee, kutoka sehemu moja ya jiografia kwenda nyingine na kutoka hali moja ya maisha kwenda nyingine. Mwanadamu amefanikiwa pale tu alipoweza kufahamu haja hii iliyo ndani yake ya kutotosheka na pale alipo na hivyo kutaka kwenda katika ngazi fulani. Historia ya kisiasa nayo ni hivyo hivyo. Tumetoka katika hali mbalimbali za kuanzia Ujima hadi maisha ya kisasa. Jamii ya watu iliyojaribu kubakia katika hali yake ya zamani imejikuta ikipigwa na jamii nyingine.

  Nimetaka kuandika kwa muda mrefu sasa kuhusu Chadema lakini kwa muda mrefu nimekuwa nikisika nikisubiri muda muda muafaka. Kutokana na hilo utaona sijaandika mengi kuhusu Chadema kama chama licha ya matukio mbalimbali ambayo yaliwafanya wengine waandike juu yake. Hata hivyo naamini huu ni wakati muafaka kufanya hivyo kuweza kuandika kiyakinifu na kibunifu juu ya uwezekano kuwa Chama cha Demokrasia chaweza kuwa ndicho chama kitakachotimiza unabii wa kuanguka CCM ambao niliuandika juu yake mapema mwaka 2007.

  Nilianza kuandika juu ya hili baada ya sakata la Buzwagi lakini mara zote nimejikuta nikikwama kufikia hatima yake na hivyo nimevuta muda taratibu hadi nimefikia hapa. Wakati huu umefika kuwa ni muafaka kwa sababu ya matukio makubwa mawili. Kwanza, watu wengi walishangazwa na mimi kuunga mkono chama kichanga kabisa cha CCJ katika kuongeza mwamko wa siasa za upinzani Tanzania, kitu ambacho wengi hawakukielewa na labda kwa kiasi watakaponisoma humu wataelewa kidogo. Pili, ni baada ya kutambua pasipo shaka kabisa kuwa CCM haina ajenda ya kushughulikia ufisadi wala kutambua kuwa ufisadi ndiyo adui mkubwa kabisa wa maendeleo yetu kuliko maradhi, ujinga na umaskini. Hili limethibitika katika Mkutano Mkuu wa CCM ambapo CCM imeshindwa kujisafisha na badala yake majinamizi ya zamani yameruhusiwa kufuliwa tena. Ni lazima tuwe na njia ya kutokea.

  Hivyo, “Chadema 2010” ni sehemu ya mchango wangu mdogo katika kukoleza kampeni za uchaguzi mkuu lakini zaidi kwa ajili ya kukipima CHADEMA kama kiko katika hali ya kuweza kudhaminiwa utawala wa taifa letu. Kwa vile utawala wa taifa si jambo dogo hata kidogo na kwa vile kubadilisha uongozi mzima wa nchi siyo jambo la kufanyia majaribio nimejaribu kukipitisha chama hiki kwenye tanuru ya moto wa fikra mbadala na kuona kama kinaweza kutupeleka huko tunakotaka au tuendelee kutumaini chama kingine.

  Hivyo, kazi hii imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni ile ninayoiita “Hapa” na sehemu ya pili ni ile ya “Kule”. “Hapa” ni kuangalia hali ilivyo ndani ya Chadema na siasa za Tanzania na ni kwanini Chadema haiwezi kutuongoza hadi itakapokuwa tayari kuhama toka “hapa”. Sehemu hii ywa kwanza inaweza kuwa chungu kidogo kwa baadhi ya watu na kusababisha hisia za kukerwa, hasira, na kuona wanasakamwa. Wakivumilia hilo na kupita salama basi wataweza kuendelea na sehemu ya pili. “Kule” ni kule ambapo matamanio yetu wengi ambao tumekuwa tukisimama kama miali ya moto kuimulika serikali na CCM tunataka nchi yetu ipelekwe. Lakini kule vile vile kule ambako Chadema inaweza kwenda. Kwa ufupi basi “hapa” kwa Chadema ni “upinzani” na “kule” kwa Chadema ni “utawala”. Mstari wa kutoka upande mmoja kwenda mwingine umenyoka.

  Natumaini kazi hii itawasaidia viongozi, wanachama, mashabiki na wale wote wenye kutaka mabadiliko ya kweli Tanzania kuweza kupata fikra mpya za mabadiliko ambazo zitaongezea au kuchochea fikra ambazo tayari walikuwa nazo. Mengi ninayoyaandika hapa siyo mageni kwa wasomaji wangu wengi na watu wanaofuatilia mijadala mbalimbali ya kisiasa nchini. Natumaini kazi hii itakuwa ni mwinyu tu wa kuchochea fikra hizo.

  Katika yote, niseme kuwa kati ya wagombea wote ambao leo wanasimama kutaka kugombea nafasi ya Urais naamini Dr. Wilbroad Slaa aweza kuwa mtu ambaye ataongoza taifa letu kuelekea mafanikio ya kweli. Hata hivyo, ni lazima kwanza awe tayari yeye mwenyewe na wale walio nyuma yake “kutoka hapa” na kuanza kuonesha kuwa wako tayari kwenda “kule”. Hata hivyo, kama zilivyo safari za jamii nyingine za watu, ni rahisi kuzungumzia kutoka “hapa” na kwenda “kule” ni vigumu zaidi kuanza safari hiyo.


  M. M. M.
   

  Attached Files:

 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Anyways, I am knocking off in 15mins, Nimepitia juu juu sounds interesting with some constructive criticism. Too ealry to comment for now. Otherwise congrats!!!!!!!!!!
   
 3. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ngoja niisome, umeiandaa lini?
   
 4. R

  Ramos JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ok.... Hayo ni mawazo yako. Binafsi naamini kutoka ndani ya kundi la zaidi ya vyama 18, CHADEMA wamefanya mambo makubwa na umakini wa kuridhisha ndio maana hadi sasa ndio chama maarufu zaidi. (pengine kuliko hata CCM). Kazi waliobakiza ni ndogo... Bravo CHADEMA...
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  hata kusoma hujasoma unaingia na kuassume..
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  fisadi vs dr slaa 2010 presdential candidate.
  Believe me or not this is what is going to happen 2011,letus give him chance to do miracles.
  The change has come.
  Dont kill!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Fisadi vs Dr Slaa.gif
   
 7. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma MKJJ,

  Ni ujumbe mzito kwenye fikra pevu. Inahitaji zaidi ya uchambuzi kuulewekaaa. kimsingi umegusiaa mambo muhimu ambayo Chadema wameyafanya na muhimu ambayo hawakuyafanya either kwa kutokujua/kutambuaa au kuona fursa hiyo.

  jambo jema ni kwamba bado wanayo nafasi ya kuyafanya tena kwa ufanisi zaidi.

  narudia tena kusoma...

  congrats!!!!
   
 8. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Unaendeleaje na mpango wako wa kusajiri radio TZ ili itumike ipasavyo kipindi hiki cha uchaguzi?

  NN
   
 9. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Mmmmm it sound profesional,najua bado wanao mda wa kuyaangalia mengi uliyoyasema nakubaliana na wewe.
   
 10. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  MH. MM bado ana nongwa ya kifo cha mimba ya ccj
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  :lol::lol::lol::lol::lol::lol:
   
 12. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Go go go Dk Slaa although ungejijenga 2015 ilikua muda muafaka au utaonekana mzee
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Jul 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimeiprint,ngoja niipitie mstari kwa mstari.
   
 14. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #14
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hongera sana M.M.M kwa uchambuzi makini uliotulia. Mungu akubariki kwa kazi nzuri unayoifanya kuamsha taifa hili letu. UBARIKIWE!
   
 15. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ngoja niprint hii issue kwani naona ni nzuri sana,
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Sijasoma ndio nasoma sasa.
   
 17. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #17
  Jul 22, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  MMK,
  Asante sana kwa very comprehensive and Constructive analysis.nimesoma yote na nitaendelea kuifanyia analysis hatua kwa hatua, na kuona hatua stahiki zinachukuliwa. Naomba uendelee kutushauri tunavyoendelea na maandalizi yetu. Tanzania ni yetu wote, na Input ya kila mmoja wetu inaweza kututoa tulipo na kwenda tunakotaka. Thanks a lot.
   
 18. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  sababu ya CCJ kukubalika kwa mda mfupi sio ufisadi bali ndoto za wananchi za kusambaratika kwa CCM, na CCM/nyerere doctrine inayosema upinzani wa kweli utatokana na ccm yenyewe
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dr usitoke hapa, teembelea mara kwa mara na nina uhakika kuwa utapata mambo mengi ya busara pamoja na kuwa kuna wachachewenye mizaha humu!
   
 20. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  thanks kwa haya

  Pia DR slaa ajaribu kwenda nchi kama kenya na Uganda na kuangalia nini kimefanyika huko na networking na viongozi wa huko. Regional Politics ni muhimu sana, Raila na Changarai wanayajua haya na ndio maana mikutano yote ya jirani hawakosi. Wangekuwa strong kwenye regional politics probably wote wawili wangekuwa president wa nchi zao
   
Loading...