Chad: Kiongozi wa waasi Jamhuri ya Afrika ya Kati Abdoulaye Miskine akamatwa N'Djamena

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
671
1,000
Viongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati akiwemo Jenerali Abdoulaye Miskine, mmoja wa watu muhimu katika masuala ya siasa na usalama nchini humo wamekamatwa nchini Chad. Jenerali Abdoulaye Miskine aliwasili N'Djamena Jumatatu jioni.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Chad, Aboulaye Miskine na viongozi wengine watatu wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati waliingia nchini Chad wakipitia Tissi, mji wa Kusini-Mashariki unaopakana na Chad, Sudani na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jenerali Abdoulaye Miskine na wenzake hawakusikilizwa. Ndio maana walipewa hifadhi kwenye majengo ya idara ya ujasusi ya Chad badala ya hoteli kama ilivyokuwa kawaida.

Suala la kuwepo kwa viongozi hawa wa waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini Chad limebua maswali. Wengi wanajiuliza iwapo wametafuta hifadhi baada ya kuzuka kwa mzozo mkubwa wa kikabila katika siku za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika mahojiano na Gazeti la kila wiki la Jeune Afrique wiki iliyopita, rais wa Chad alisema kwamba serikali yake - ambayo mara nyingi imekuwa ikituhumiwa kuchochea machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati - inatarajia kutoa msaada kwa jirani yake wa Kusini kwa kurejesha utulivu.

1574242822498.png

Picha: Jenerali Abdoulaye Miskine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom