IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Enyi Watanzania Badilikine!
Watanzania mna nini humo vichwani mwenu? mnawaza nini? Ni nani anaweza kukujengea nyumba yako mwenyewe huku umesimama pembeni? Mbona tunaishia kupiga kelele tu? mara tumeibiwa, mara mikataba mibovu ooo!!!!! ardhi yetu!!!. Hii tabia ya uoga itaisha lini hapa tanzania?
Napenda watanzania ndugu zangu tusiishie kupiga kelele huku hawa watawala wetu wakichukua vilivyo vyao, wakifanya watakavyo. Ni nani katuroga? maisha yetu yana thamani gani katika taifa letu hili tajiri huku sisi tukiwa maskini wa kutupwa?
MKOA WA MARA, UNAPATIKANA KANDA YA ZIWA,huko ndiko Mwalimu Nyerere alikozaliwa, wakazi wa mkoa huo ni wazalendo, wapenda nchi yao, kujitoa kafara si shida kwao, na ndiyo maana majeshini wamejaa.Siku zote wao hujua 1+1=2 na wala si 3, uongo kwao ni sumu, hawa ndiyo walioleta upinzani wa kweli 1995, walipoamua kuvichagua vyama vya upinzani siku zile mtakumbuka kama si Mwalimu Nyerere siku zile mkoa mzima ungetwaliwa na wapinzani.
Hoja yangu ni hii, kwa kuwa watanzania mumeona jinsi watu wa mara wanavyojitahidi kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini,sasa hamuoni kuwa CHACHU NDOGO HUCHACHUSHA DONGE ZIMA? mikoa yote mna kazi ya kujitutumua ili tukatae unyanyasaji huu wa chama hiki cha ccm? Jiulize ni kwa nini CCM MWAKA HUU WAMEAMUA KUFANYIA VIKAO VYAO HUKO MUSOMA? CCM INAWAJUA WANAMARA,HAWADANGANYWI KWA MKATE.
Ndugu zangu watanzania tunataka mabadiliko, lakini tunajiangusha sisi wenyewe, maneno yamekuwa mengi, nawashukuru KIGOMA, KAGERA ambapo panaonyesha kuwepo kwa mabadiliko.
Mwana wa Mwita nimesema.