Chacha Wangwe Kuyafikisha Mahakamani magazeti Kwa Kumchafulia Jina

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Naomba niwashirikishe taarifa hii ambayo nimeipata jana. Pamoja na kuwa binafsi siungi mkono mtindo wa kuyapeleka mahakamani magazeti(ila naunga mkono kama njia zote zikiwa zimepitiwa na bado ukweli ukashindwa kuandikwa) lakini naamini habari hii itajibu maswali ambayo wajumbe humu waliniuliza siku kadhaa zilizopita baada ya kueleza upande wa pili wa sarafu ya yaliyotokea Tarime. Tuendelee kujadili

Natoweka tena...

JJ

20/10/2007


Att.Mhariri.
Samson Chacha Tarime.

MBUNGE CHACHA WANGWE ADAI KUYAFIKISHA MAHAKAMANIMAGAZETI KWA KUMCHAFULIA JINA.

Mbunge wa jimbola Tarime mkoani Mara,Bw. Chacha Zakayo Wangwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mara na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, amedai kuwa ana nia ya kuyafikisha mahakamani magazeti ya Habari Leo,Uhuru na Mwananchi kwa madai ya kumchafulia jina kuwa yeye ni muongo,mchochezi,mpinga maendeleo na anasomesha watoto wake nje ya nchi,huku watoto wa wananchi wakisoma nchini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya chama cha CHADEMA(W)Tarime-hapo October 20.2007,wakiwepo wajumbe wa serikali ya kijiji cha Nyakunguru ; Bw...Mgaya Maitarya,Mwita Mbang'o,Elias Kelambo,Mniko Mwita Kehogo na Bi.Nyangi Daniel,pia walikuwepo viongozi wa chama hicho(w)Bw.Joseph Antony Katibu (w)Bw.Manyata Mweka hazina(w)Chadema na madiwani Tecla Johanes , Mary Nyagabona, Leticia Ghati Mosore,Tengera Itembe(Makamu Mwenyekiti/Halmashauri (W)Tarime na Nestory Sasi (M/Kiti wa kambi ya upinzani Tarime).

Mbunge huyo Bw.Wangwe alisema kuwa ''Mimi ninawasiliana na mawakili wangu kuangalia ni taratibu zipi tutakazotumia kuyafikisha magazeti hayo mahakamani ili yawajibike kisheria kwa kunichafulia kwa makusudi jina langu zuri kwa umma wa Watanzania bila sababu ya msingi,wakijua kuwa mimi ni kiongozi ninayeaminiwa na wananchi walionichagua pamoja na chama changu kuwawakilisha katika misingi ya haki na kweli''.

Mbunge huyo,alisema kuwa magazeti hayo ni:''Habari Leo'',toleo namba 00302 ,''Uhuru'',toleo namba 19757 na ''Mwananchi','toleo namba 02684,yote ya Alhamisi, tarehe 18 Oktoba 2007. Mbunge huyo anadai kuwa magazeti hayo yalimchafulia jina kwa kuandika kwamba ni mwongo, mchochezi, anasomesha watoto wake nje ya nchi, alizomewa, baada ya kikao hicho alipanda ndege ya Barrick wakiwa na wakili Bw. Tundu Lissu kuelekea Dar es Salaam siku hiyo hiyo, madai ambayo ni uzushi mtupu na uongo uliolenga kumvunjia heshima mbele ya wananchi anaowawakilisha.
Bw.Wangwe alisema kuwa waandishi walioandika habari hizo ni Makubo Haruni na Mathias Marwa ambao kwanza hawakuwepo katika mkutano huo. Walikuwa Tarime mjini umbali wa kilometa 32 kutoka kijiji cha Nyakunguru ambako mkutano huo ulifanyikia.Waandishi waliokuwepo mkutanoni ni Bigambo Jeje, Mabere Makubi na Hamad Kitumbo wote kutoka Musoma mjini.

Alisema kuwa hao waandishi walioandika habari hizo za uzushi walionekana kesho yake ofisini kwa DC Stanley Kolimba wa Tarime, wakiwa na afisa mawasiliano wa Barrick aitwaye Emmanuel Nyasigo, Abel Maginga (aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakunguru aliyeng'olewa madarakani tarehe 26 Septemba 2007 kwa tuhuma mbalimbali). Baada ya mahojiano mafupi, waandishi hao waliondoka na kwenda kutuma habari hizo katika magazeti hayo bila kufanya uchunguzi wowote.

Wajumbe wa serikali ya kijiji hicho cha Nyakunguru wakiongozwa na Mgaya Maitarya, walisema kuwa mkutano mkuu wa tarehe 26 Septemba 2007 uliomng'oa Abel Maginga madarakani haukualikwa na mbunge huyo, bali uliitishwa na mtendaji wa kijiji hicho aitwaye Emmanuel Simangwe kwa maagizo ya mwenyekiti wake.Mbunge alikuwa mwalikwa kama wajumbe wengine.Baada ya taratibu za kisheria kuzingatiwa wajumbe 342 waliohudhuria walimkataa mwenyekiti huyo na kufunga ofisi yao ya kijiji.

Walisema kuwa tuhuma zilizomuondoa madarakani Mwenyekiti Abel Maginga ni pamoja na kuuza ardhi ya kijiji kwa mgodi wa Barrick yenye ukubwa wa ekari 24 zilizokuwa zimetengwa kwa ujenzi wa shule na ofisi ya CCM kwa Tsh.6.2m/= bila idhini ya mkutano mkuu wa kijiji na kuzitumia fedha hizo kwa manufaa yake binafsi, kutowasomea mapato na matumizi kwa muda wa miaka saba tangu achaguliwe.

Wajumbe hao waliendelea kudai kuwa mwenyekiti huyo Abeli Maginga alishawahi kukataliwa na hiyo ilikuwa ni mara ya tano na mkutano mkuu wa kijiji. Mara ya kwanza alikataliwa tarehe 13/2/2006, tarehe 9/4/2007 (mbele ya mbunge Chacha Wangwe), tarehe 19/4/2007(mbele ya DC Stanley Kolimba), tarehe 25/7/2007(mbele ya mtendaji wa kata Maisori Sabai) na tarehe 26/9/2007(mbele ya mbunge Chacha Wangwe).Mkutano huo wa tarehe 26/9/2007 ndio ulioletelezea DC Kolimba kuitisha mkutano wa tarehe 16/10/2007 kwa shinikizo la kampuni ya Barrick akiwa na lengo la kumrejesha madarakani kwa nguvu mwenyekititi huyo aliyeng'olewa.

Walisema kwamba kilichosababisha mzozo katika mkutano huo wa DC Kolimba ni pale DC alipomsimamisha Abel Maginga na kumtaka aendeshe mkutano huo kwa madai kuwa yeye ndiye mwenyekiti halali wa kijiji hicho, jambo lililosababisha wananchi kumpinga Abel Maginga kuendesha kikao hicho kwa sababu yeye ni mtuhumiwa na waliisha mkataa.Hapo ndipo mbunge alipoingilia kati na kumtaka DC aheshimu maamuzi ya wananchi.Hatimaye DC aliafiki maoni ya wananchi na kuchukua jukumu la kuwa mwenyekiti wa mkutano huo yeye mwenyewe na kikao kikaendelea.

Mkurugenzi wa H/W Tarime Trasias Kagenzi akatoa azimio kwamba ofisi ya kijiji ifunguliwe, mtendaji wa kijiji aendelee kuhudumia kijiji kwa siku saba. Wakati huo mikakati ya kuandaa mkutano mwingine wa kijiji wa kumjadili Abel Maginga itekelezwe.Pia aliagiza kuwa kwa hizo siku saba mwenyekiti huyo aliyekataliwa asikanyage ofisini, walisema wajumbe hao wa serikali ya kijiji.

MWISHO.
Simu:0756436446
 
Huu utaratibu wa waandishi kuandika habari bila kuwemo mkutanoni ni kawaida huku bongo wala sioni cha ajabu.

Tatizo ni pale unapoandika habari za uongo!!

GO GO Chacha!
 
Wangwe, kwa mwanasiasa hakimu ni wananchi. Badala ya kusumbuka mahakamani, wewe chapa kazi na wananchi ndio wataamua nani mwongo.

Kuna case chache sana za siasa ambazo kuna umuhimu wa kwenda mahakamani, lakini kadri ninavyoisoma hii case naona kwenda mahakamani ni kupoteza muda tu.

Any way uamuzi ni wa Wangwe mwenyewe, lakini kwa mimi hii trend ya kila mtu kukimbilia mahakamani hata kwa madai ya kisiasa naona ni kupoteza muda tu.
 
Huu utaratibu wa waandishi kuandika habari bila kuwemo mkutanoni ni kawaida huku bongo wala sioni cha ajabu.

Tatizo ni pale unapoandika habari za uongo!!

GO GO Chacha!

Kuandika bila kuhudhuria, nani anakuwa source ya information zako. Utaandika mawazo yanayotokana na msimamo wa anayekusimulia na siyo matukio halisi.

Anyway, ukisoma habari hii na ile iliyotoka awali kuna kutofautiana sana kana kwamba ni matukio tofauti.
Nani anasema kweli na yupi kaongopa?
Akishtaki leo haki yake anaweza kuipata hata mwaka 2011 ndo mambo ya mahakama zetu.

Nadhani kukanusha kunatosha bila kulazimika kwenda mahakamani!
 
Wangwe chapa kazi,wala usiende mahakamani,hayo magazeti yalishaadhibiwa na wananchi,ni magazeti yanayotumiwa na mafisadi.achana nao,siye tulijua huo ulikua udaku tu.
 
...hii mambo ya wanasiasa wetu so called KUCHAFULIWA JINA inaniacha hoi sana,hivi chacha anafikiri nani anajari jina lake eti limechafuliwa? anafikiri wananchi hawana akili mpaka waanze kuangalia jina lake chafu au safi....ni kabunge tuu ka huko sijui tarime kanafikiri kila mtu anakafuatilia na kukaona ka maana sana mpaka kuchafuliwa jina,pumbaf sana chacha na umaarufu hautafutwi magazetini bora tuu uendelee kufanya kazi huu usafi wa jina lako tuachie wananchi wako wa Tarime...kwani press release haitoshi mpaka uende mahakamani? haya mambo ya cheap popularity na kujiona miungu mtu ndio hatuyataki
 
sasa kuchafuliwa majina na waandish eeh, wale wengine mafisadi wameelezwa ukweli.

hapa waandishi wakurupukaji, kule wamepasua jipu
 
We Koba, kutukana siyo vizuri sasa. Wewe toa hoja zako, sisi tutaziona na kuzipima. Mbona unamtukana tena huku ukitambua kuwa ni Mbunge wako? Elewa kuwa kuchaguliwa kwake na wananchi kuwawakilisha ni heshima kubwa.
 
...wewe Si kitiyi hapo juu PUMBAF sio tusi na mjomba wako Chacha wangwe needs to grow up na ugomvi wake na mwenyekiti wa kijiji na magazeti asiende kutujazia kesi zisizo na kichwa wala mguu kwenye mahakama zetu...kwani nakuuliza wewe Si kitiyi PRESS RELEASE haitoshi kwa issue ndogo kama hii mpaka uende mahakamani?
 
Kaka Wangwe,salamu na pole na majukumu,
Ama baada ya salamu napenda kuchangia kuhusu uamuzi wako wa kwenda mahakamani kushtakiwa kuhusu "kuchafuliwa" jina.Binafsi nadhani huna haja ya kwenda mahakamani,kwanza kwa sababu si kila kitu lazima uende mahakamani,pili swala hili sidhani kama lina uzito sana kiasi hicho kama ambavyo baadhi ya watu wanakushari,ebu jaribu kuweka mizani sawia na utazame matokeo,yaani kwenda mahakamni kutakujenga/kukubomoa kiasi gani kuliko kutokwenda?
Kwa sasa nadhani jina lako bado ni safi hivyo huhitaji kulichafua kwa mambo ya kimahakama.Hakimu wenu ni sisi wananchi,tazama mfano wa Zitto Kabwe,Mbunge mwenzio,ni kweli kafukuzwa bungeni kwa kuhoji maslahi ya Taifa,kaiitwa muongo,n.k. lakini hakuonesha reaction yoyote ile bali wananchi ndo wamesimama kwa niaba yake na hali yote ya kisiasa inayoendelea hapa nchini chanzo ni yeye.Hivyo na wewe jaribu kufikiri kwanza,kwenda mahakamani kutapunguza umaarufu wako zaidi ya kukujenga.Isitoshe kwa watu wenye akili hiyo habari wala haikutugusa kwani tulijua kwa nini iliandikwa na ni kwa nini ikawa kwa magazeti hayo na ndo sababu haikupata uzito wowote kabisa.
Wewe chapa kazi 2010 sio mbali wananchi ndio watakaohukumu...kumbuka kina Ditto,Nyali wanavyopeta kutokana na Mahakama hizi hizi...

NAWASILISHA
 
Sawa, hata mimi sishauri kwenda mahakamani sioni umuhimu wowote, kwanza jambo lenyewe siyo zito hadi aamue kwenda mahakamani. Mimi hoja yangu ilikuwa juu ya neno pumbafu, mimi naliona kama tusi. Kama siyo tusi basi sawa.
 
...hii mambo ya wanasiasa wetu so called KUCHAFULIWA JINA inaniacha hoi sana,hivi chacha anafikiri nani anajari jina lake eti limechafuliwa? anafikiri wananchi hawana akili mpaka waanze kuangalia jina lake chafu au safi....ni kabunge tuu ka huko sijui tarime kanafikiri kila mtu anakafuatilia na kukaona ka maana sana mpaka kuchafuliwa jina,pumbaf sana chacha na umaarufu hautafutwi magazetini bora tuu uendelee kufanya kazi huu usafi wa jina lako tuachie wananchi wako wa Tarime...kwani press release haitoshi mpaka uende mahakamani? haya mambo ya cheap popularity na kujiona miungu mtu ndio hatuyataki

Unavunja heshima yako (kama iliwahi kuwepo) kwa kutumia lugha kali ya matusi namna hiyo.
Unaweza kufikisha ujumbe kwa kutumia maneno ambayo yanastahili kwenye sehemu kama forum. Katumie lugha hizo nyumbani kwako na siyo hapa!!!!!!!
 
Unavunja heshima yako (kama iliwahi kuwepo) kwa kutumia lugha kali ya matusi namna hiyo.
Unaweza kufikisha ujumbe kwa kutumia maneno ambayo yanastahili kwenye sehemu kama forum. Katumie lugha hizo nyumbani kwako na siyo hapa!!!!!!!

.....nafikiri kuna kitu unatafuta kutoka kwangu,subiri uone!
 
Hakuna cha kutafutwa hapa, ulichoharibu wewe ni kutumia lugha chafu. Unatakiwa kuwasilisha ujumbe wako kwa kutumia kichwa na si kutumia moyo: Kichwa kinatawaliwa na hekima na busara, bali moyo hutawaliwa na hisia (emotions).
 
hamna hoja nyie...katukanwa EL,JK na mawaziri wote hakuna kitu mlisema leo huyo chachacha kidogo tuu kashtuliwa hapa mnakuja juu kama tsunami...hamna deal nyie wanazi!
 
hamna hoja nyie...katukanwa EL,JK na mawaziri wote hakuna kitu mlisema leo huyo chachacha kidogo tuu kashtuliwa hapa mnakuja juu kama tsunami...hamna deal nyie wanazi!
Kuna tetesi hizo kuwa walimuhonga lakini bado alikuwa na nia ya kuipeleka hoja ya Barrick bungeni.Wakati anaondoka,alienda kumuaga Sitta, ambaye alimwambia awe makini,lakini hakurudi na hoja haikuwakilishwa...Lakini cha ajabu ccm na mapandikizi wanasambaza uzushi.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom