Cha Kujifunza Mwananchi Kutoka Port Harcoat - Rivers United 1 - 0 Young Africans SC

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
6,311
2,000
1. Licha ya usajii mzuri hatukuwa tumeyachukulia serious michuano ya CAF.

2. Mafanikio ya Simba SC ya msimu uliopita yalifanya ionekane ni rahisi zaidi kuweka jitihada zisizo thabiti kufika mbali kwenye michuano ya CAF.

3. Pilika za usajili zilifanya tupoteze focus kwenye kuhakikisha ushiriki wa wachezaji wote wanaosajiliwaili waweze kucheza kikamilifu. Pengo la Djuma, Aucho & Mayele yalikuwa na impact katika kuamua matokeo.

4. Ratiba ya Ligi kuu msimu uliopita ilikuwa siyo rafiki hata ikapelekea kucheleweshwa kuhitimishwa kwa Ligi na kuathiri mapumziko & maandalizi ya timu. (Hii itawaathiri washiriki(timu) nyingi zinazotoka Tanzania zikishiriki michuano ya CAF msimu huu.

5. Substitutions za Prof Nabi hazikuwa na Impact katika kuamua matokeo ya Mechi zote mbili ikiwa factors zote huko juu hazikuzingatiwa.

6. Kitu pekee ambacho tumekifanya vyema nyakati hizi ni kwenye kuongeza ubora wa wachezaji kikosini.

WHAT NEXT?
a. Tunahitaji muda zaidi wa kuwaona hii timu mpya ikiwa pamoja at least for one season. Baada ya hapo tutakuwa kwenye position ya kuwa na matarajio kuhusu Klabu Bingwa.

b. Tuandae recruitment network ambayo itakayo tuakikishia wachezaji bora kwa ajili ya msimu ujao (tusingoje kuchukua wachezaji walio maliza mikataba yao)

c. Ni wakati sasa wa kupeleka jitihada na Focus kwenye LigiKUU Tanzania Bara ili kuhakikisha tunashiriki michuano ya CAF tukitokea kwenye Ubingwa wa LigiKUU.

- Ilikuwa ni wiki mbaya ofisini iliyotokana na kupotea kwa muda mrefu kwenye michuano ya CAF na hata kusahau wajibu na majukumu yetu kama Klabu. -

1111.jpg
 

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
9,087
2,000
Moja kati ya mambo yanayowakwamisha Yanga ni kutaka kushindana na Simba ambayo tayari ina muunganiko na uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Kweli leo uzoefu umeonekana wa kuwakodi kina whozu.
Huo tu ndo tumeuona, new player kibu Denis 😀😀🙌🏾🙌🏾
 

permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
6,236
2,000
Maandalizi mabovu yamechangia kufungwa
Yanga ina uwezo wa kumfunga yoyote kwa sasa, kikubwa wachezaji wazuri wapo, timu ipate muda wa kupata muunganiko mzuri ikizingatiwa kuna wachezaji muhimu tumewakosa kwenye game zote mbili, mwalimu naye aomeshe makali yake.
 

Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,120
2,000
viongozi waache janja janja ambazo zinaikwamisha yanga,pale wamejaa walaji watupu wasio itakia mema yanga
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,296
2,000
Kwahiyo kocha wa kidimbwi Fc kashaanza kufungasha mizigo yake.maana hiyo tarehe 25 mambo yatakua haya haya ya leo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom