Certificate in Pharmaceutical Sciences -Je Wajua?

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,578
7,280
Wana jukwaa leo nilikuwa napitia NACTE Guide Book ya Afya 2018/19 nikijielekeza kwenye Basic Technicians Certificate (Level 4) na Technicians Certificate in Pharmaceutical Sciences. Nilicho ona huko kuna vyuo viwili tu vinavyotoa Basic Certificate-PARADIGMS COLLEGE OF HEALTH SCIENCES - DAR ES SALAAM (REG/BMG/033) - Private na TANDABUI INSTITUTE OF HEALTH SCIENCES AND TECHNOLOGY (REG/HAS/117). Kilachuo kina chukua wanafunzi 200 kwa mwaka mmoja. Ada ni 2.8m na 3.0m. Hawa wanataka 4 passes F4 pamoja na Chemistry na Biology.

Kundi la pili ni la vyuo vitano mwanafunzi anadahiliwa kuchukua Technicians Certificate in Pharmaceutical Sciences (Level 4 and 5 kwa pamoja) kwa miaka 2. Vigezo ni F4 kupasi masomo manne (D's) pamoja na Chemistry na Biology. Ufaulu wa hesabu na english ni added advantage,

Kundi la tatu ni vyuo 14 vinavyotoa Technicians Certificate in Pharmaceutical Sciences (Level 5 NTA) ambavyo ukidahiiwa unatakiwa uwe na (i) Pass 4 pamoja na Chemistry na Biology NA (2) NTA Level 4 Certificate in Pharmaceutical Sciences.

Kwa hiyo hili kundi la tatu (vyuo 14) linategemea wanafunzi kutoka kundi la kwanza kwanza (vyuo 2). Na hii nafikiri ndio inafanya ada za kundi la kwanza kuwa kubwa 2.8-3m kwa mwaka mmoja. Wakuu hii pyramid ya hivi vyuo imekaaje?
 
Write your reply...hivi ukisoma basic technician pharmaceutical science utafanya kazi gan?
 
Write your reply...kwahy bongo nzima vyuo vinavyotoa basic technical certificate ni viwili tu?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom