Barbara Gonzalez Kesi yako Binafsi uliyofunguliwa inahusiana vipi na Taasisi ya Simba SC? Acha kutafuta Huruma ya Simba SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,466
108,621
GENTAMYCINE nimekuwa nikitumia Nguvu Kubwa sana hapa JamiiForums Kuwashaurini na hata kwa Kuwaongoza kwa yale msiyoyajua ila mmekuwa mkinipuuza hivyo sasa acha yakupate na yatupate ili tushike Adabu zetu.

CEO Barbara Gonzalez tafadhali GENTAMYCINE nakuomba acha mara moja Kuiingiza Taasisi ya Simba SC katika Mgogoro wako Binafsi na huyo Afisa wa TFF ( ambaye ni Mwanamke Mwenzako ) na kutafuta Huruma ya Kilazima kutoka Kwetu Mashabiki wa Simba SC na najua wale Mashabiki Wapumbavu ( Mapopoma ) watakuunga mkono ila siyo Kwangu Mimi GENTAMYCINE ( Jeshi la Mru Mmoja ) kutokea Mkoani Mara ( Musoma )

CEO Barbara Gonzalez ukaribu wako wa 'Kibaiolojia' na Mwekezaji Tajiri Mohammed Mo Dewji kumekupa Jeuri, Dharau na Kiburi na kwa Watu tunaoijua Simba SC kabla yako, tuliojitolea Kuipigania, tunaokujua vyema hasa kupitia Watu wako wa karibu katika Menejimenti ya Simba SC tunaposikia kuwa Unatukana Watu au Kuwajibu hovyo hatukushangai kwani ndiyo Ukweli na ndivyo ulivyo 100% pia.

Hivi majuzi hapa hapa JamiiForums niliandika Uzi wa Kuwashtueni Viongozi wa Simba SC kuwa amkeni imarisheni Kitengo chenu cha Umafia kwani tunaumizwa ila kwa Upumbavu ( Upopoma ) wenu hamkunielewa na sasa mnabaki Kulialia tu hovyo.

Usichokjjua CEO Barbara Gonzalez ni kwamba Kiburi chako, Jeuri yako na Dharau zako za Pesa ( Utajiri ) unaopewa na 'Mbaiolojia' Mwenzako Tajiri Mo Dewji ndiyo ANGUKO KUU la Simba SC na hasa katika Kukomolewa Kwetu huku kuhusu Viwanja vya Kuchezea na Ratiba Ngumu kwani TFF ya Karia nayo sasa inakunyoosha 'Kiaina' kwa Hasira za kutaka Kuwatibulia Keki yao ya Tsh Bilioni 2 za Udhamini wa GSM na Uvaaji wa Nembo yao.

Simba SC inakomolewa kwa ajili yako na hiyo Kesi ni sehemu moja tu ya Kukuchanganya Kisaikolojia ( na kwa jinsi nilivyokusikia Ukiongea EFM jana na Maulid Kitenge ) tayari Umeshaanza Kuchanganyikiwa na hapo bado mpaka 'Uuteme' Mwenyewe huo U - CEO wako uliopewa 'kinamna namna' tu.

Halafu CEO Barbara Gonzalez Kauli yako ya kusema kuwa Mwenendo mbaya wa Simba SC kwa 50% unachangiwa na Wewe Kuandamwa Kwako na Vita hii ya TFF, GSM na Wewe waambie Wapuuzi unaofanana nao ila kwa Mimi GENTAMYCINE najua kuwa Wewe na Uongozi wako wa Simba SC ukimuhusisha 'Mbaioloji' Mwenzako Tajiri Mo Dewji mmeacha Kusajili Wachezaji wazuri, mmeshatengeneza Matabaka ndani ya Kikosi cha Simba SC na hamuwalipi vyema Wachezaji hasa Posho zao na Timu nzima imekosa 'morale' huku mkificha kuwa kwa sasa Tajiri Mo Dewji hatoi tena Pesa Klabuni kutokana na kidogo Kuyumba Kibiashara huku GSM sasa Wakiimarika zaidi kutokana na Mfumo wa sasa Kiutawala.

CEO Barbara Gonzalez niliyeandika Uzi huu ni Mimi GENTAMYCINE mwana Simba SC lia lia hivyo usije kudhani labda ni mwana Yanga SC au natumiwa na Yanga SC isipokuwa nimeshindwa Kuuvumilia Upuuzi na Unafiki ambao unaendelea Kushamiri ndani ya Klabu yangu pendwa na Tukuka ya Simba SC.

Hongera ( Hongereni ) sana kwa Kujitutumua Kuicheza kwa Nguvu zote Mechi ya Kesho na Kagera Sugar FC ( huku mkizipuuza zile Mbili za Mbeya City na Mtibwa Sugar FC ) ila msisahau tu kuwa TAKUKURU na Serikali haijalala na ipo macho 24/7.

CEO Barbara Gonzalez nitakuona tu una Akili na upo Makini kama Ukikiri kuwa kwa Msimu huu Watani zetu Yanga SC wako vizuri, wametuzidi Ujanja ( Kete ) na kwamba wana Uwezekano wa Kuwa Mabingwa hivyo Simba SC tujitahidi tu Kupambana nao ila Nguvu yetu Kubwa tuielekeze katika ASFC ( FA ) kama na huko pia tutabahatika nako.

Kwa wale Wote ( hasa wana Simba SC ) ambao mtakereka na Kuchukizwa na huu Uzi wangu Ushauri wangu Kwenu ni ama Kunibloku ( Ignore ) msiwe mnanisoma

GENTAMYCINE ni kama Bahari ambapo huwa sikai na Uchafu na hata kama ukiwa ni Rafiki yangu au Ndugu yangu ukikosea ( ukikengeuka ) tu nitakusema ( nitakukosoa ) bila Aibu au Uwoga ili Ujitathmini na Ubadilike upesi.

Na nina bahati mbaya moja huwa siyo Mnafiki, sipendi Unafiki na sijui Kujipendekeza ( Kujikomba ) kwa Mtu hata akiwa ni Tajiri, Maarufu au ameshawahi Kunisaidia kwa chochote / lolote.

Nimemaliza.
 
Huu uzi umenivuruga,wacha nikanywe supu kwanza nirudi kuusoma taratibu.

Lakini mheshimiwa Gentamycine,embu tuhurumie kidogo,kama haya usemayo ni ya uhakika,na sio hisia,kuna jitihada umefanya mkuu haya usemayo yawafikie wahusika ili tuitetee timu yetu? Nahofia tutasoma hapa na kukomenti na ku like halafu hakutakua na mabadiliko.

Hivi yule mwenyekiti wetu ambaye anatokana na kundi hili la hisa 51% anajua hili?manake naona kama wenye hisa 49% ndo wanahusika na timu kufanya vizuri na kufanya vibaya pia. Nimesema ngoja nikanywe supu. Siku ishaharibika
GENTAMYCINE nimekuwa nikitumia Nguvu Kubwa sana hapa JamiiForums Kuwashaurini na hata kwa Kuwaongoza kwa yale msiyoyajua ila mmekuwa mkinipuuza hivyo sasa acha yakupate na yatupate ili tushike Adabu zetu...
 
GENTAMYCINE nimekuwa nikitumia Nguvu Kubwa sana hapa JamiiForums Kuwashaurini na hata kwa Kuwaongoza kwa yale msiyoyajua ila mmekuwa mkinipuuza hivyo sasa acha yakupate na yatupate ili tushike Adabu zetu...
Sasa nimeanza kuamini manara aliyokuwa anasema kuhusu hako kadada ka kihindi,, kale kadada kanaonekana kana na roho mbaya alafu anaonekana anajisikia sana kwasababu tu ana ukaribu natajiri basi anajiona yeye ndo mwenye Simba..

Alichokifanya pale kumrekod mtu huku anaongea mbovu alitegemea nn??

Ujinga wake binafsi asiihusishe simba, apambane mwenyewe na huyo mwanamke mwenzake
 
Huu uzi umenivuruga,wacha nikanywe supu kwanza nirudi kuusoma taratibu.

Lakini mheshimiwa Gentamycine,embu tuhurumie kidogo,kama haya usemayo ni ya uhakika,na sio hisia,kuna jitihada umefanya mkuu haya usemayo yawafikie wahusika ili tuitetee timu yetu? Nahofia tutasoma hapa na kukomenti na ku like halafu hakutakua na mabadiliko.

Hivi yule mwenyekiti wetu ambaye anatokana na kundi hili la hisa 51% anajua hili?manake naona kama wenye hisa 49% ndo wanahusika na timu kufanya vizuri na kufanya vibaya pia. Nimesema ngoja nikanywe supu. Siku ishaharibika
Mkuu amini tena 100% hakuna ambacho GENTAMYCINE nakiandika hapa JamiiForums halafu Mtu kama Poti wangu kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) Crescetius Magori ( Mshauri Mkuu, Mjumbe na Mdau wa Ufundi Simba SC ), Mwekezaji Mo Dewji, CEO Barbara Gonzalez, Mulamu Ng'ambi na Meneja wa Simba SC Mtani wangu kutoka Mkoani Kagera ( Bukoba ) Patrick Rweymamu hawakisomi, ila basi tu wanapuuza na kudhani Yanga SC ya Safari hii imelala wakisahau kuwa Mbinu zetu zile zile zilizofanya tuwe Mabingwa 'Msaliti Mwandamizi' Haji Manara ameondoka nazo na kwenda kuwaambia Yanga SC na ndiyo hizo hizo wanazitumia sasa na zinawasaidia vilivyo kufikia Malengo yao ya kuwa Mabingwa wa Msimu huu.
 
Sasa nimeanza kuamini manara aliyokuwa anasema kuhusu hako kadada ka kihindi,, kale kadada kanaonekana kana na roho mbaya alafu anaonekana anajisikia sana kwasababu tu ana ukaribu natajiri basi anajiona yeye ndo mwenye Simba..

Alichokifanya pale kumrekod mtu huku anaongea mbovu alitegemea nn??

Ujinga wake binafsi asiihusishe simba, apambane mwenyewe na huyo mwanamke mwenzake
Nashukuru kwa Kunielewa Mkuu na kuhusu aliyekuwa Msemaji wetu Haji Manara kumsema vibaya CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez alikuwa sahihi tena 100% kabisa sena tu akina Sisi Wabobezi na Waandamizi wa Propaganda akina GENTAMYCINE tuliamua tu Kupambana na Manara ili Kutuliza Hali na Kumuweka sawa CEO wetu Barbara Gonzalez ili ajikite zaidi katika Kuipigania Simba SC yetu.

Lakini cha Kushangaza analeta Dharau, Jeuri na Kiburi hata kwa Watu ambao wanamshauri ( tunamshauri ) halafu wala hatutaki Malipo yake yoyote kwani Umasikini wetu tumeshauzoea, ila tuna Mapenzi ya Kweli na ya Kujitoa Mhanga kwa Simba SC yetu.

Mkuu nina Nyeti Mbili ambazo nazihifadhi Kwanza kwa Maslahi mapana ya Simba SC yangu ( yetu ) kwani najua wana Simba SC wakizijua ( zikienda Public ) Moto mkubwa sana utawaka Klabuni.

Wajitahidi mno Kesho Simba SC ishinde.
 
Mambo ya ndani hayo mkuu, msiwaumize hao matajiri, kaeni chini mjipange nyie ni nguvu Moja kumbuka
Mkuu acha GENTAMYCINE niwanyooshe kidogo hapa labda watabadilika upesi kwani wengine Kuuvumilia Udunduna ( Ujinga ) na Upopoma ( Upumbavu ) huwa hatuwezi na Kwetu kusema Ukweli na kutokuwa Mnafiki ndiyo Jadi ( Hulka ) yetu.
 
Back
Top Bottom