CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo acha Kutumika na Yanga SC yako na GSM 'Kuionea' Simba SC yasije kukuta makubwa na usiamini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,858
Ni kwamba Masela ( Wahuni ) wote wa Ubungo ( hasa pale UFI ) pale Manzese na Magomeni ( Migomigo ) tunakujua fika kuwa Wewe ni Yanga SC 'lia lia' na wengine ni 'Mashemeji' zako vile vile kwa Dada zako.

Wana Simba SC tunaokujua tumeshakuvumilia vya Kutosha juu ya 'Hujuma' zako ambazo umeanza kutufanyia Simba SC na sasa tokea uwe katika 'payroll' ya Yanga SC ( hasa kupitia GSM ) ndiyo umekuwa unafanya 'Madudu' tu kila Kukicha.

Wengine Watu wa Mpira ( kama akina GENTAMYCINE ) tuna Taarifa zako nyingi tu za namna unavyopanga na Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC Premier League ili Kutuhujumu Simba SC kwa kila namna ili mradi tu mwaka huu Yanga SC iwe Bingwa japo huo Ubingwa mtaendelea tu Kuusikia katika Bomba na Simba SC itautwaa ( itaubeba ) tena.

Almasi Kasongo ( CEO wa Bodi ya Ligi ) pia akina GENTAMYCINE tuna Taarifa zako za 'Ulivyotuhujumu' Simba SC kwa 'Mapato' tulipocheza Mechi yetu Muhimu ya CAF CL kwa Kushirikiana na 'Wanafiki' wa N-Card pamoja na Mawaziri Wawili 'Waandamizi' wa Rais Samia Mmoja akitokea Kanda ya Ziwa na Mwingine akitokea Nyanda za juu za Kati bila Kumsahau na Katibu Mkuu wa Wizara ambaye Kipindi cha Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na 'Utajiri' wa Vyeo Viwili halafu alikuwa Jeuri na mwenye Dharau nyingi tu.

CEO wa Bodi ya Ligi Kuu Almasi Kasongo nina mengi yakuhusuyo ila nimeona nianze Kwanza na haya machache ila kama Mshabiki 'Kindakindaki' wa Simba SC GENTAMYCINE 'nakuonya' kuwa acha kutumika na Yanga SC yako na GSM yao kwa namna yoyote ile ili 'Kuihujumu' Simba SC bali tenda ( tendeni ) haki na muache 'Vitisho' kwani bahati mbaya wengine 'mnaotutisha' ni 'Mafia' kwelikweli hivyo inaweza Kukugharimu na Ikawagharimu.

Hili Sakata la Udhamini Mwenza wa GSM na jinsi Wewe binafsi CEO Almasi Kasongo ulivyolikabili 'Kimahaba' ya Kuipenda Yanga SC yako ndiyo limekuharibia zaidi japo Watu wa Mpira tunakujua kuwa Wewe ni Mtendaji na Mchapakazi mzuri sana isipokuwa tu ulipoingia hapo TFF na kupata hicho Cheo ukawa 'Fixed' na Wapuuzi akina GSM na sasa umeingia na wanakutumia watakavyo kwa Maslahi yao Kibiashara na ya Yanga SC ndani ya Uwanja.

Ikinipendeza baade GENTAMYCINE nitakuja na Taarifa za chini chini ( nyepe nyepe ) za Kumhusu Mwamuzi ( Referee ) wa Simba na Yanga Jumamosi Hery Ssasii kwani bado naendelea Kuzithibisha kutoka katika Vyanzo vyangu 'Vitiifu' ndani ya Klabu na Kambi ya Yanga SC.

Simba SC hatutovaa Logo ya GSM yenu!!
 
Ni kwamba Masela ( Wahuni ) wote wa Ubungo ( hasa pale UFI ) pale Manzese na Magomeni ( Migomigo ) tunakujua fika kuwa Wewe ni Yanga SC 'lia lia' na wengine ni 'Mashemeji' zako vile vile kwa Dada zako...
kisu kimefika kwenye mfupa mtatapatapa sana mwambieni kanji bai nae azamin ata ligi daraja la pili
 
Haya ndiyo madhara ya kuwekeza kwenye mpira halafu unataka faida na sifa za chap chap.. Gsm yanga ya kimataifa haiji kwa kuweka nembo tu. Ijenge timu matunda baadaye. Be fair Kasongo, sepp blatter yuko wapi?...
 
Huyu kasongo analeta ujuaji kosa la bangala kwenyd ngao ya jamii mpaka leo haijatolea uamuzi, refa wa namungo na yanga mpaka leo kamati haijakaa ila makocha wa ruvu na namungo walipolalamika kamati ilikaa haraka na kuwaadhibu
Kuna swali nikiuliza mnakwepa kujibu. Hivi Morrison atafungiwa lini Kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Namumgo? Au hili haliihusu kamati ya ligi?
 
Jamani wanasimba wenzangu hii tabia ya kulalamika na kutafuta vijisababu tumeianza lini? Yaani baada ya kugundua msimu huu timu yetu ni mbovu tumeamua kutafuta wa kumwangushia jumba bovu mapema hivi?
Duh yaani wabongo tutasubiri sana kwa wakenya yaani mambo hayaendi sawa ubaki kimya
 
Back
Top Bottom