Census: Ina umuhimu gani katika nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Census: Ina umuhimu gani katika nchi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kisoda2, Aug 26, 2009.

 1. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Zoezi zima la kuhesabu watu katika nchi zetu za kiafrica limekuwepo kwa muda mrefu.
  Tukiangalia jirani zetu Kenya jana walipewa offday ile wakahesabiwe,na pia zoezi zima lilifanyika hata nyakati za usiku.
  Mambo yaliyojitokeza katika zoezi hilo na kuwa changanya wananchi ni kama haya:-
  1.Kuulizwa kabila lako.
  2.kutaja kipato chako.
  Na maswali mengine mengi.

  Kutokana na hali hiyo wengi waliohojiwa na kiuo cha redio cha BBC/swahili,walisema hawatohesabiwa na kuna walio hesabiwa walisema hawajui zoezi zima lina maana gani kwao na litawasaidia nini katika kupambana na hali mbaya ya masiha waliyo nayo.

  Natumai hali hii hata hapa kwetu tuli wengi tunahesabiwa tu,kwa kua kasema mtendaji/mjumbe wa nyumba kumi nk.
  Lakini kiukweli hatujui kunafaida gani katika kuhesabiwa huko,na kama kupo mbona maisha yanazidi kuwa duni kila kukicha na kuhesabiwa kuko palepale?

  Wadau naomba kujuzwa hili.kwa faida ya wengi pia.

  Naomba kuwakilisha.
   
Loading...