Celtel-Zain-Airtel-.., Vodacom (PamojaDaima)-Vodacom (Kazi ni Kwako)...Shamba la Bibi

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Ndiyo hivyo jamani, kama shamba lisilo na mwenyewe vile! Wajanja wanakuja na mbegu chache lakini wanazalisha na kuvuna kwa kutumia watumishi walewale na shamba lilelile kisha wanakula, wanashiba halafu wanaondoka na mbegu nyingi mara dufu ya kiasi walichokuja nacho. Kabla ya kuondoka wanawapigia miluzi wajanja wenzao wengine kuashiria kwamba wao wamevimbiwa. Hao nao wakija wanatumia shamba lilelile na watumishi walewale kwa staili ileile mpaka wanavimbiwa na kuondoka. Kila anapoingia mjanja mpya lazima amwalike kiongozi mkuu wa wamiliki wa shamba kwenye hafla ya kubadilishana uendeshaji wa shamba na wamiliki wanashangilia na kugonganisha bilauli zilizojaa vinywaji vya bei mbaya!
 
Hujamaliza, ongeza Sheraton-sasa moven pick, jina moven pick nafikiri ni la sita toka sheraton, wamiliki ni walewale majina tu ndio yanabadirika ili kulamba tax-holiday. Serikali ikifuta hiyo kitu tax-holiday hutaona tene huo ujinga wa celtel-zain-airtel, wala sheraton to movenpick. Tatizo rushwa kwa watendaji wa serikali kwa kuwa siamini kwamba eti hawajui mchezo huu, ipo siku watayajibu haya mahakamani.Tumechoka kuwa shamba la bibi, tena hawa ni bibi wale wa zamani , maana bibi wa siku hizi angalau wanachapa fimbo kidogo, hakuna mjukuu kudekadeka.
 
haki ya baba hawa washenzi lazima tuje tuwavute kwa minyororo haiwezekani wawe wanauza nchi yetu tu kwa dhamana tuliyo wapa ya uongozi ****** chunga sana historia haifutiki wewe ponda raha sasa siku zako zinahesabika
 
Back
Top Bottom