Cell Standby na Screen kwanini Zinatumia % ya chaji

Mbishi Uswazi

Senior Member
Feb 7, 2020
142
249
Habari wanaJF,

Wajuzi wa haya mambo mnijuze kwanini hivyo vitu vinatumia sana chaji na kufanya battery kuishiwa chaji haraka

Ni nini na vinafanyaje kazi pia naomba kujua ninawezaje kuzuia zisifanye kazi au zipunguze kula chaji?

IMG_20200623_132231_011.jpg
 
Cell standby inakula moto mdogo sana, kitoke hali kama yako,basi huenda haupo eneo zuri lenye mtandao. Hivyo basi simu yako inatumia moto mwingi kusaka na kumaintain signal..

Sasa jiulize eneo ulilopo lina network fresh?
 
Cell standby inakula moto mdogo sana...ikitoke hali kama yako,basi huenda haupo eneo zuri lenye mtandao,hivyo basi simu yako inatumia moto mwing kusaka na kumaintain signal..

Sasa jiulize eneo ulilopo lina network fresh?
Itakua kweli mkuu nipo Maeneo Ambayo Mtandao unasoma E..
 
Iko hivi, ukiichaji simu leo ukaiacha hapo usiitumie, au ukaitumia kidogo sana lakini ikawa muda mwingi imekaa bila kutumika, basi ukiangalia kwenye matumizi utaona cell standby inaongoza hata uwe ndani ya ofisi za service provider ambapo network ni strong.

Hii ni kwasababu battery usage inakuonesha jinsi battery yako ilivyotumika, na simu ili ibaki standby lazima chaji iwemo, tofauti na hapo itazima.

Nikijibu swali lako la "kwanini cell standby inakula chaji? Ni kwasababu simu kuwa standby nayo ni sehemu ya matumizi ya battery, japo hii inatumia chaji kidogo sana.
 
Back
Top Bottom